Nimejiuliza sana yafuatayo:-
Hivi anatudharau watanzania anatuona hatuna akili?
Amelewa madaraka?
Yupo kwenye kipindi kigumu kisaikolojia anapitia hali fulani mbaya?
Waliomteua walikosa mtu mwingine katika watanzania milioni 60 na kitu?
Anatafakari kwa kina kabla ya kuongea?
Anafuatilia taarifa muhimu zinazo tolewa na vyombo vya dola au za taasisi mbalimbali za serikali kabla hajaongea majukwaani?
Atapoteza nini akiacha mambo mengine upepo wake upite kwanza?
Kwanini anakimbilia kuongelea mambo makubwa na ya hatari au sensitive kwa jamii bila kuwa na ujuzi wa mawasiliano kwa umma?
Angewaacha wenye taaluma ya usemaji wawatetee, yeye kila akifungua mdomo anaharibu hali ya hewa.