Kama mzazi, binti yako ndio amekuja kukuambia kuwa amepata mchumba, ni swali gani la kwanza utamuuliza binti yako?

Ubaguzi huu kabila la nini?
Maswali muhimu ni haya,
1. Ni kabila gani
2. Anafanya kazi gani
3. Mlikutana wapi
4. Mmefahamiana Kwa muda gani
Kama ni mchaga usimlete hapa.
 
ngoja nichukue course ya maswali hapa,yanaweza nisaidia hapo baadae baada ya 20 yrs huko, binti yangu akiniletea hizo nyuzzz🙂
Mmh mbona unajificha kwa binti yako ,chukua mkeka huu maswali ni haya haya na unajibu kama interview
 
1.Binti huyo mchumba wako ni chadema au ccm?
2.unahisi mnaweza vumiliana katika shida na raha?
 
😀😀😀Unauwaaa mkuu.... Kasoongooo wewoooo
 
1: Ni mkristo, if not usimlete kabisa
2: Anafanya kazi gani?
3: Ana elimu kiwango gani?
4: Anakunywa pombe au anavuta sigara au bangi?
5: Una mjua kwa muda gani sasa?
6: Mmepima afya?
7: Ni kabila gani?
 
Kwa ufafanuzi zaidi wa kuongezea kuhusu alichosema mdau kwa maswali muhimu kuuliza, Maswali haya yana malengo muhimu kwa mzazi, hasa kwa kuhakikisha kuwa binti au kijana wake anafanya uamuzi sahihi wa maisha kuhusu ndoa. Haya ndiyo malengo ya kila swali:

1. Anaitwa nani majina yake yote matatu?

Kujua utambulisho kamili wa mchumba wake, kuhakikisha hakuna usiri au utata kuhusu mtu anayehusiana naye.



2. Anatokea wapi?

Kufahamu asili yake na historia ya familia yake, jambo ambalo linaweza kusaidia kuelewa malezi na maadili yake.



3. Baba yake ni nani na familia yake ni ya akina nani?

Kupata taarifa kuhusu familia yake na asili yao, kwani familia inaathiri tabia na malezi ya mtu.



4. Baba yake anajishughulisha na jambo gani au shughuli zake za kiuchumi?

Kujua hali ya kiuchumi ya familia yake na kama itakuwa na athari kwenye ndoa yao.



5. Kwao wapo watoto wangapi na yeye ni mtoto wa ngapi?

Kufahamu muundo wa familia yake, jinsi alivyokuzwa, na mahusiano yake na ndugu zake.



6. Mlikutana wapi na lini?

Kupata mwanga kuhusu namna uhusiano ulivyoanza na kama ulikuwa wa haraka au wa muda mrefu.



7. Umefanya naye chochote hadi sasa kimwili?

Kuhakikisha maadili yamezingatiwa katika uhusiano wao na iwapo kuna athari zozote za kimwili ambazo zinaweza kuathiri mustakabali wao.



8. Amekupa mipango gani kuhusu maisha yake binafsi, yaani kalenga kujishughulisha na jambo gani maishani na wewe unaingia kama nani katika hayo maisha yake?

Kujua kama mchumba ana malengo ya maisha na kama mwanao ana nafasi sahihi ndani ya mipango hiyo.



9. Umekwenda kwao, mara ngapi?

Kupima kiwango cha uhusiano kati ya mwanao na familia ya mchumba wake, na iwapo familia yao inamkubali.



10. Nani anakufahamu kwao au nani wa upande wa kwao mna mawasiliano ya karibu?



Kujua kama kuna mtu wa familia yake anayemtambua mwanao, ili kuhakikisha uhusiano huu si wa kificho.


11. Nani kati yenu alimfuata mwenzake na ni nani hadi sasa anaendelea kushawishi huu uhusiano uwepo?



Kupima nguvu ya uhusiano, nani anaonekana kuwa na juhudi kubwa, na kama kuna usawa katika mapenzi yao.


12. Wewe kama binti unayeingia kwenye mahusiano ya kudumu, unaingia na huyu kijana kwa malengo gani?



Kufahamu iwapo binti yako ana malengo sahihi na yuko tayari kwa ndoa, badala ya kuwa kwenye uhusiano kwa sababu zisizo za msingi.


13. Unayafahamu majukumu anayokuitia mkafanye naye mahusiano au unakwenda kuyajulia mbele ya safari?



Kuhakikisha mwanao anajua majukumu yanayokuja na ndoa, badala ya kuingia bila kuelewa matarajio.


14. MUNGU ana nafasi gani katika uhusiano wenu?



Kupima misingi ya kidini katika mahusiano yao, kama wanazingatia maadili na imani yao.


15. Mpo tayari kufuata maagizo ya MUNGU katika uhusiano wenu?



Kuhakikisha kuwa wataishi kwa misingi ya kiroho na kufuata mafundisho ya dini yao.


16. Mlishakaa na kupanga mnakwenda kuanza mahusiano ya namna gani?



Kujua iwapo wamefanya mpango wa ndoa na wanajua hatua wanazopaswa kuchukua.


17. Umepima afya yako na yake?



Kuangalia afya zao ili kuepuka changamoto za kiafya zinazoweza kuathiri maisha yao ya ndoa.


18. Unazifahamu changamoto za huyu kijana na tabia zake ambazo zinaweza kinzana na wewe, yaani madhaifu yake kama mwanadamu?



Kufahamu kama mwanao anajua udhaifu wa mchumba wake na kama yuko tayari kukabiliana nao katika ndoa.


Maswali haya yana lengo la kuhakikisha mwanao anafanya uamuzi wa busara, yuko tayari kwa ndoa, na anajua majukumu yanayomsubiri. Kama mzazi, haya maswali yanakupa mwanga kuhusu mustakabali wa mwanao katika ndoa.
 
mlete nimfanyie tathmini nimtengenezee mazingira kuwa rafiki kwangu.
 
1.Nitamuuliza huyo mchumba ni ME or KE maana siku hizi mambo ya UPiNDE , mmh!
2. Anampenda?
3.Wana muda gani kwenye mahusiano?
4. Dini
5.Anajishughulisha na nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…