Kama nafsi/roho huendelea kuishi baada ya kifo, Ndoto yangu niufahamu ukweli kuhusu ulimwengu

Kama nafsi/roho huendelea kuishi baada ya kifo, Ndoto yangu niufahamu ukweli kuhusu ulimwengu

Joseph Gadiel

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2022
Posts
452
Reaction score
765
download (51).jpeg

Kama baada ya kifo nafsi/roho huendelea kuishi na kupata fursa ya kuonana na muumbaji wa ulimwengu, basi ndoto yangu na ombi langu kuu mbele ya muumbaji ni kupata fursa ya tour. Yaani deep time travel tour back in time miaka bilioni 15 iliyopita, nishuhudie nini kilikuwepo kabla ya Big bang, jinsi big bang ilivyotokea, ndoto yangu nishuhudie haya yote, mpaka jinsi Space & time zinavyoumbwa, Niweze kusafiri kwa zaidi ya speed ya mwanga, nijionee formation of Galaxies, Nyota na Takataka zote za ulimwengu na kama kuna other multi verses niweze kuziona, Nishuhudie origin of life. Nione na nizishuhudie dark energy na dark matters.

Kufikia tu nyota ya karibu kwa kutumia chombo chenye kasi zaidi kama voyager chenye speed ya 17.3km/s inachukua takribani miaka 73,000 hapo haujazungumzia kukatiza tu katikati ya galaxy yetu ambayo kwa chombo hicho hicho itachukua miaka zaidi ya bilioni 2 kukatiza tu katikati. Jambo ambalo haliwezekani. Na hapo tunazungumzia galaxy yetu tu! Bado hatujaongelea mabilioni na mabilioni ya galaxy zingine zilizopo pamoja ma takataka zingine huko! Kwa hiyo utagundua ni jambo lisilowezekana kabisa kimwili!

Hivyo ombi langu na hamu yangu kubwa ni kufikia huko kote na kujionea kwa macho yangu, kote mpaka pembezoni mwa ulimwengu wote na miisho na mwisho wa dahari huko pakoje.
 
Mkuu ukifa hutoenda mbali. Utaliwa na nyenyere hapo futi tano tu chini ya ardhi na shughuli yako itakuwa imeisha.
 
Hakuna next episode kwenye kifo, ukifa unakuwa msosi wa wadudu huko chini nothing more.
Expire date YAKO ikifika ndo kwaheri
 
Back
Top Bottom