Kama nchi tuko vibaya, nani mwenye kubeba dhima ya ukombozi wetu?

Kama nchi tuko vibaya, nani mwenye kubeba dhima ya ukombozi wetu?

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Huku tozo, kule kina Simbachawene. Huku dhuluma, watuhumiwa wakuu vyombo vya dola. Haki hamna, masanduku ya kura hayaheshimiwi. Mambo lukumba lukumba, tunatokaje hapa?

Muhimu tukatambua hatutatoka hapa bila kulipa gharama ambayo haitakuwa ndogo. Hatutatoka hapa bila organization wala uongozi uliodhamiria hivyo. Hatutatoka hapa kwa kumsuburia kila mtu kuamka. Hatutatoka hapa kwa kutegeana au kuhoji fulani yuko wapi. Ukombozi huu si jukumu la Mbowe, Lissu au Chadema. Tufike mahali tutambuane na kufanya maamuzi magumu kwa maslahi yetu, watoto wetu, wajukuu zetu na hata watoto wa wajukuu zetu.

"Ni heri kufa tukiipigania nchi kuliko kufa kwa Malaria." - Prof. Azaveli Lwaitama.​
 
Tuipe muda Serikali na watalaam Wetu. Daktari wa Uchumi na timu yake wapo makini watamsaidia Mama kutuvusha
 
Vyovyote vile ila swali langu ni hili; ninapotoa akiba yangu (SAVINGS) ambayo niliwakabidhi benki wanitunzie (na service charge juu) nakua nimeingiza kipato gani cha kustahili kukatwa kodi/tozo? Wataalamu wa kodi mnisaidie
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Usicheke mkuu. Ni wazi kuwa:

"Hatutatoka hapa kwa kutegeana au kuhoji fulani yuko wapi.

Ukombozi huu si jukumu la Mbowe, Lissu au Chadema."

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Ila tozo na makato ya ajabu ajabu yamezidi aisee khaaa

Wamezoea tuko busy na Simba na Yanga huku wao wakiitafuna nchi na kutusokomezea matozo. Tufike mahali tutambuane sasa. Imetosha.
 
Taifa la hovyo hili limejaa waoga na wapenda udaku

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Tunapenda matunda Vila kuwafanyia kazi. Tunataka mema bila kuyapigania. Tunataka kumsubiria Yule ili tuone nini kitamkuta.

Ninakazia:

"Muhimu tukatambua hatutatoka hapa bila kulipa gharama ambayo haitakuwa ndogo. Hatutatoka hapa bila organization wala uongozi uliodhamiria hivyo. Hatutatoka hapa kwa kumsuburia kila mtu kuamka. Hatutatoka hapa kwa kutegeana au kuhoji fulani yuko wapi. Ukombozi huu si jukumu la Mbowe, Lissu au Chadema. Tufike mahali tutambuane na kufanya maamuzi magumu kwa maslahi yetu, watoto wetu, wajukuu zetu na hata watoto wa wajukuu zetu."
 
Back
Top Bottom