Kama nchi tumefeli kwenye Ufunguzi wa African Football League

Habari za wakati huu wakuu,

Jana ilikuwa siku muhimu sana katika Historia ya Soka la Tanzania na Africa kwa ujumla baada ya Ufunguzi wa African Football League katika Uwanja wa Benjamin william Mkapa mechi ambayo iliisha kwa sare ya goli mbili.

Wadhamini wakubwa wa mashindano haya ni Saudia na Rwanda, ambapo wakati mechi inaendelea maneno kama Visit Rwanda na Visit Saudia yalionekana, ambayo kiuhalisia hiyo nafasi ilitakiwa iwe yetu.

Inamaana kuanzia zanzibar na Tanzania bara hawakuona umuhimu wa kutafuta kitu cha kututangaza kama nchi mpaka Rwanda na Saudia wanachangamkia fursa sisi tupo tumelala usingizi wa pono! Hapo kama nchi tumefeli.

Kwa tukio la jana ambalo watu maarufu na viongozi mbalimbali wa mpira Duniani walikuwa uwanjani akiwemo Rais wa FIFA na aliyekuwa Kocha wa zamani wa Arsenal, Mzee Arsene Wenger ilikuwa fursa adhimu ya kuonyesha vipaji mbalimbali tulivyonavyo katika nchi yetu.

Hivyo nilitegemea wachezaji wa Timu ya Wanawake ya Simba na wachezaji vijana wa Simba kucheza mechi za ufunguzi kabla ya mechi rasmi, kwasababu jana kulikuwa na football agents kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Kweli mtu amuangalie Kibu Denis na Saido Ntibazonkiza hata kama ni wachezaji wazuri atawapeleka wapi kwa umri wao? Kosa kama hilo tulifanya walivyokuja Sevilla kutoka Spain, walisema wachezaji wa Simba ni wazuri ila umri ndio ilikuwa tatizo.

Wenzetu hutumia fursa kama hizi kama njia ya kuonyesha vipaji walivyonavyo na kuonyesha uwezo wa wachezaji wadogo kama njia na fursa ya kusakata kabumbu nje ya Bara la Afrika na Tanzania kiujumla, ila na hapo pia tumefeli kama nchi na kama club.

Simba kwa kushirikiana na serikali walitakiwa waingie makubaluano katika mashindano haya makubwa kwa ngazi ya vilabu Barani Africa, nilishangaa kuona M-Bet badala ya Visit Tanzanka kwenye kifua wakati mkataba wa M-Bet ulikuwa ni CAF Champions League kwa Level za Kimataifa na Mashindano yote ya ndani, nilishangaa kuona na hili pia linatupita kama nchi tumefeli kwenye hili tena.

Kuteleza si kuanguka, ila wakati mwingine tutumie haya mashindano kibiashara zaidi kuliko kuangulia tu matokea. Bado hatujachelewa, tujipange tena kwenye Maandalizi ya AFCON, tusichezee fursa wakati zipo mlangoni mpaka majirani wanazichangamkia.

Tatizo tunaangalia kila kitu kisiasa na kiushabiki, ndio maana kila siku tunakumbuka shuka kumekucha! Tuamke wazee, Dunia ya 1980 sio ya leo 2023, next time tujipange.

Alamsik.
Umeeleza vizuri, ila kuna mambo ya kuwekana sawa kidogo. Mechi ile ya ufunguzi wala haikuwa ya Simba, ila ilikuwa ya CAF na FIFA, na wao ndiyo waliamua kila kitu kuhusu ile mechi.

Ndiyo maana tunaona mshirika wa FIFA, ambaye ni EA Sport ndiyo aliyepanga kila kitu kuhusu sherehe ya ufunguzi itakavyokuwa na kwa muda upi.

Na hata kazi ya kurekodi mechi ile ilisimamiwa nao wakitumia vifaa vya Azam na kuwakodi watendaji wa Azam. Camera zilipangwa kwa maelekezo yao.

Hata idadi ya camera zilizokuwepo uwanjani iliwekwa kwa matakwa yao. Zilikuwa mara mbili ya ambazo Azam huwa wanatumia kwa kawaida yao. Na alama zote za Azam zilifunikwa.

Hivyo, suala kama la Simba Queen kucheza mechi pale halikuwa na nafasi kwa CAF na FIFA. Hata Simba yenyewe ililazimika hadi kuwanunulia tiketi baadhi ya watu wake ili kuingia uwanjani.

Kwa kuwa kwenye mashindano haya kuna Visit Rwanda na Visit Saudia, moja kwa moja Simba inapoteza haki ya kuvaa jezi ya Visit Tanzania hata kama ingekuwa na mkataba na Simba.

Tanzania imeshawahi kutangaza vivutio vyake CNN, kwenye gazeti la Mirror na hata kwenye EPL kupitia uwanja wa soka wa klabu ya Everton, na juzi tu kwenye Royal Tour.

Haya bado ni mashindano mapya, yana mechi chache bado, nadhani ni sawa pia kujipa muda wa kuona kwanza mrejesho wake kabla na sisi kuweka hela.

Tanzania kama nchi kwa ufunguzi kufanyika Tanzania, imepata faida. FIFA na CAF walitumia hela wakiwa Tanzania, tena siyo hela kidogo. Hivyo, ule uhaba dola unaweza kupoa kidogo kwa sasa.

Ova
 
Ufunguzi wa AFL ulisimamiwa na wenyewe waandaaji wa AFL, mwanzo mpaka mwisho. Tanzania ilikuwa inatwa support tu.
 
Habari za wakati huu wakuu,

Jana ilikuwa siku muhimu sana katika Historia ya Soka la Tanzania na Africa kwa ujumla baada ya Ufunguzi wa African Football League katika Uwanja wa Benjamin william Mkapa mechi ambayo iliisha kwa sare ya goli mbili.

Wadhamini wakubwa wa mashindano haya ni Saudia na Rwanda, ambapo wakati mechi inaendelea maneno kama Visit Rwanda na Visit Saudia yalionekana, ambayo kiuhalisia hiyo nafasi ilitakiwa iwe yetu.

Inamaana kuanzia zanzibar na Tanzania bara hawakuona umuhimu wa kutafuta kitu cha kututangaza kama nchi mpaka Rwanda na Saudia wanachangamkia fursa sisi tupo tumelala usingizi wa pono! Hapo kama nchi tumefeli.

Kwa tukio la jana ambalo watu maarufu na viongozi mbalimbali wa mpira Duniani walikuwa uwanjani akiwemo Rais wa FIFA na aliyekuwa Kocha wa zamani wa Arsenal, Mzee Arsene Wenger ilikuwa fursa adhimu ya kuonyesha vipaji mbalimbali tulivyonavyo katika nchi yetu.

Hivyo nilitegemea wachezaji wa Timu ya Wanawake ya Simba na wachezaji vijana wa Simba kucheza mechi za ufunguzi kabla ya mechi rasmi, kwasababu jana kulikuwa na football agents kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Kweli mtu amuangalie Kibu Denis na Saido Ntibazonkiza hata kama ni wachezaji wazuri atawapeleka wapi kwa umri wao? Kosa kama hilo tulifanya walivyokuja Sevilla kutoka Spain, walisema wachezaji wa Simba ni wazuri ila umri ndio ilikuwa tatizo.

Wenzetu hutumia fursa kama hizi kama njia ya kuonyesha vipaji walivyonavyo na kuonyesha uwezo wa wachezaji wadogo kama njia na fursa ya kusakata kabumbu nje ya Bara la Afrika na Tanzania kiujumla, ila na hapo pia tumefeli kama nchi na kama club.

Simba kwa kushirikiana na serikali walitakiwa waingie makubaluano katika mashindano haya makubwa kwa ngazi ya vilabu Barani Africa, nilishangaa kuona M-Bet badala ya Visit Tanzanka kwenye kifua wakati mkataba wa M-Bet ulikuwa ni CAF Champions League kwa Level za Kimataifa na Mashindano yote ya ndani, nilishangaa kuona na hili pia linatupita kama nchi tumefeli kwenye hili tena.

Kuteleza si kuanguka, ila wakati mwingine tutumie haya mashindano kibiashara zaidi kuliko kuangulia tu matokea. Bado hatujachelewa, tujipange tena kwenye Maandalizi ya AFCON, tusichezee fursa wakati zipo mlangoni mpaka majirani wanazichangamkia.

Tatizo tunaangalia kila kitu kisiasa na kiushabiki, ndio maana kila siku tunakumbuka shuka kumekucha! Tuamke wazee, Dunia ya 1980 sio ya leo 2023, next time tujipange.

Alamsik.
Unajua gharama za hayo matangazo lakini au unalaumu tu.
Mm naona tumefanikiwa maana Africa zima inaizungumzia Tanzania kwa sasa..

Ninachoomba serikali itumie hizi fursa za michezo na burudani vizuri sana kuvutia wawekezaji kiuchumi.
Mfano. Serikali inaweza kuwekeza kwenye kumbi za burudani ili tuhost matamasha makubwa mbalimbali.
Pia serikali inaweza kuwezesha miundombinu ya michezo mbalimbali.

Secta ya michezo na burudani ikitendewa haki tutafika mbali sana
 
Una point japo wasiwasi wangu ni terms za mikataba kati ya hao wadhamini Visit Rwanda na Visit Saudi so isingewezekana mnyama kuwa na Visit Tanzania ila kama nchi ingetakiwa kuwapa Offer ya kuwapeleka Mbugani ile delegate ya FIFA ingesaidia sana kuutangaza utalii wetu.
hiki kitu hata mimi nilikiwaza, mikataba ingewahiwa mwanzo kabisa tungepata display nzuri tu
 
Hivi unajua kwamba yale ni mashindano chini ya uangalizi wa CAF na sio TFF wala Simba?

Unajua kwamba ile haikuwa mechi ya hisani au testimonial match...?
Anajiropokea tu,msameheni.
 
Caf wanamjua ali kiba?
Kwa nn ile nafasi ya alikiba kutumbuiza wasingewapa team za academy
Kwahyo unataka kusema hapo misri alikiba hajulikani?? ..unajua kuwa wimbo aliotumbuiza ali alipangiwa na caf?
 
Acha uongo Caf na FIFA wanaijua sumu aliambiwa asi perform nyimbo inayohusiana na team yoyote katika zile mbili ila hakuambiwa nyimbo ya ku perform tumia akili kidogo.
 
Anajiropokea tu,msameheni.
Nyinyi ndio mnadandia gari kwa mbele unasoma tu title ya thread halafu una type utopolo ungesoma nilichoandika chote sidhani kama ungeandika hizo pumba zako.
 
Back
Top Bottom