Midimay
JF-Expert Member
- Apr 12, 2015
- 3,036
- 5,039
Vita ya jirani sio ya hardware tena. Hii milumbano yetu ya kiumbeya umbeya hadi ya wakuu wa mihimili tayari ni failure kwetu na ndio njia kupotezwa focus.Andiko hili na walione wahusika.
Pamoja na siasa zetu za kunyukana mara Sukuma gang,Msoga na wana kuupiga mwingi lakini kama Nchi tutambue tunalo tishio lililo bayana kabisa la yule 'dogo' naamini wengi mmenielewa hakika anakuja juu sana kimedani.
Si wa kupuuzwa tena!
Amewekeza sana kwenye u-sasa na kila kitu chake sasa ni cha kisasa.
Shime linapokuja suala lihusulo uzalendo tujadili kizalendo.
Kwanini marais wetu wanapenda kujibu wakikosolewa? Kwanini wasisonge mbele na maamuzi yao badala ya kujibizana na watu ambao kimsingi hawawezi kumzuia kufanya lolote.
Kuanzia sasa, waache tabia ya kuwajibu wanaowakosoa. Rais ni mtu mkubwa sana. Awaache watu wapige kelele zao bila kuwajibu.
Kuwe na kiwango cha criticism ambayo Rais anaweza kuitolea ufafanuzi.
Marais wetu hawajiamini kabisa wakati katiba inawalinda to its best.