Kama ndo ukweli huu! Siungi mkono Beno kurejea Jangwani maana alimdharau Kocha

Mpira ni ajira na siyo kufanya hisani,utachezaje wakati familia inalala njaa....
Aangalie future yake,pale jangwani njaa na longolongo mob

Sent using Jamii Forums mobile app
Alichokosea Benno ni kutaka kurudi tena mahali waliposhindwa kumlipa mshahara. Nilitegemea wakati huu atakuwa kwenye mahakama za michezo akisaka haki zake. Yanga haina pesa kwa sasa ana uhakika gani kwamba wakati huu atalipwa.
 

Thanks...Ila Beno kamwe hawezi kurudi Yanga...inavyoonekana meneja wake ambaye ni kiongozi wa Simba alikula njama na wanasimba wenzake kuhakikisha Yanga inahujumiwa ...Kwa hiyo huyo meneja atalazimika kumtafutia timu huyo anayeitwa Beno..na ni vema asajiliwe Simba, ila kwa Yanga hawezi kurudi tena...Yanga wana msimamo..mamluki hawatakiwi kabisa ndani ya Yanga...Na kwa kusema ukweli huo ndiyo mwisho wa soka ya Beno...hakuna mchezaji aliyewahi kuisaliti Yanga na akaendelea kuwika huko aendako...Hovyo kabisa huyo Beno...alijua kuwa yeye ni mtu mhimu ndani ya kikosi kutokana na alivyodaka siku ya mechi ya dhidi ya Simba..magazeti yakampamba na akavimbishwa kichwa..ma-simba yakaona kuwa huo ndio ulikuwa wakati wa kuihujumu Yanga kwa hiyo wakamshawishi aisaliti timu...awaulize akina Munishi, Niyonzima na Bartez...Munishi au Dida sasa anashindwa kudaka hata mpira uliopigwa mita 30...huyo Bartez toka alivyofungwa goli la 'kinamna' la Kichuya la mpira wa kona, ndiyo basi tena...huyo Niyonzima akairingia Yanga pamoja na ukweli ilimsaidia mno pamoja na mmoja wa wazazi wake, akaenda Simba sasa huko anakula wa 'chuya'...list ya walioisaliti Yanga na wakaharibikiwa ni wengi...
 
National team asahau kucheza tena labda kocha atangaziwe kikosi na tff,na Simba wenyewe waliomshawishi wanaweza kumuacha mitaani, maana wabongo huwa wanafanya mambo kwa maslahi yao tu
 
hivi umeshawaona wale wachezaji wa zamani waliocheza mpira kwa mapenzi hali zao zikoje, Benno kachagua mpira kuwa ajira yake na nyinyi mnatakiwa kumlipa sio kuanza kukoroma wakati pesa hamna.Hivi hapa nani anaweza kufanya kazi bila kulipwa hao watumishi wa serikali ikifika tarehe 25 mshahara haujatoka utaona post kibao za kulaumu serikali lakini nyie mnamshutumu bila kujua huyu mtu ana majukumu yake na familia yake nyinyi mnaomshutumu ndio nyinyi ambao mtamcheka baadae wakati amefulia mnyonge mnyongeni haki yake mpeni
 
Maslahi ya Mchezaji ni miongoni mwa vipengele muhimu kwenye mkataba, endapo mchezaji hajatimiziwa matakwa yake kimkataba ilaumiwe klabu si mchezaji kama mnavupmzodoa Benno. Punguzeni mahaba mjaddili bila kuegemea popote.
 
Kweli kabisa mkuu
 
Reactions: Oxx
Maslahi ya Mchezaji ni miongoni mwa vipengele muhimu kwenye mkataba, endapo mchezaji hajatimiziwa matakwa yake kimkataba ilaumiwe klabu si mchezaji kama mnavupmzodoa Benno. Punguzeni mahaba mjaddili bila kuegemea popote.
Usidhani kila mafanikio hayana changamoto mkuu,ni karibia timu nzima inamadai na kocha alishakaa nao na kuwapa msimamo wao,why hakuondoka pale? Kwasoka la Bongo atastrugle sana
 
Yanga haiwezi kumlipa na alishaondoka sasa anarudi wapi?
 
Anayejua annajua tu,ndio maana utumwa hauishi duniani.Wasomi mnajadili kama vichaa,Benno hakuzaliwa na yanga ana haki kukipigania kipaji na haki yake kwa ngivu zote.Atachezea timu zingine au hata akifa masikini kuliko kuwatumikia hao wachumia tumbo wa yanga.Siungi mkono hoja ya kubembeleza masikini.Na mkuu ukitaka kujua watanzania sisi wapuuzi subiri tetesi zitoke anaenda simba uone.Hakuna tunalolijua.
 
Mkuu kilichopo wachezaji wa Yanga wamekubali kuishi nje ya utaratibu( wamekubali kucheza bila maslahi). Beno yeye kwa vile anategemea mpira na hawezi tena kusubiti kupata maslahi yake hakutakiwa kugeuka nyuma tangu siku alipojiengua kambini. Yanga haijamnyima Beno haki yake isipokuwa hali ni ngumu ndani ya klabu. Beno alichotakiwa kufanya ni kwenda mbele zaidi kudai haki yake hadi kieleweke. Unaporudi tena mahali uliposaliti harakati za wenzako tukuelewe vipi? Ndio kudai haki kwenyewe ndio huko?!
 
Kwa hiyo ninyi huwa mnawaroga wanaowasaliti.
 
Kawe wewe kipa uzibe pengo lake acheni haki zake.mbona wewe hukua kipa.
 
Umesahahau mkuu kuweka wazi, kwamba Meneja wake aliyemtoa kambini pia ni kiongozi wa mikia a.k.a vibonde wa Mashujaa



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…