Kama ndo ukweli huu! Siungi mkono Beno kurejea Jangwani maana alimdharau Kocha

Kawe wewe kipa uzibe pengo lake acheni haki zake.mbona wewe hukua kipa.
Kwani kipa yuko peke ake Mzee.....? Si kashavunja mkataba tayari? Anataka nini tena? Mchukueni nyinyi mumpe hizo staiki zake, kwan anaedai staiki zake yuko peke yake....? Anataka kuvuruga team tu, Ata sisi uku tulipo tunadai zetu uku tunachapa mzigo kama kawaida Mzee!.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio msitupigie lelele hapa,kama akiomba msamaha akisamehewa utasemaje.Huruhusiwi kuhukumu jambo ambalo hujui mustakali wake.Hata kwenye siasa kuna maandamano.muacheni akija mfukuzeni.watanzania wengi hujadili jambo kwa mitizamo binafsi pekee badala ya kuchanganya na ya kijamii.
 


"Wagogo wa Jangwani," kwa kweli hii timu ipo siku itakufa tu, kama si wachezaji kugoma basi viongozi wasio na manufaa klabuni watagombana kulilia ugoro wao.
 
Stori yake ipo hadharani mpaka sasa... Inajulikana ni msaliti na msaliti ni msaliti tu....

Si tunamsikiza na kumsuport kocha wetu.....! Akisamehewa tutamsamehe pia asiposamehewa na Zaera si atumtaki kusiwe na nguvu ya kulazimisha arudi adi kocha azidiwe......!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuwa mwelewa usiwe mbumbumbu ,kocha alishwambia atafute timu kabla dirisha halijafungwa mambo ya kusamehewa umeleta wewe.
 
"Wagogo wa Jangwani," kwa kweli hii timu ipo siku itakufa tu, kama si wachezaji kugoma basi viongozi wasio na manufaa klabuni watagombana kulilia ugoro wao.
Umepanic mkuu,Mbona povu la mwaka mpya? Yanga inawatesa sana nyie mikia
 
Kocha kwanza, Beno baadaye
 
Reactions: Oxx
Hana chake kwa Timu ya wananchi
 
Hapa hapazungumziwi usomi wala u-Yanga. Panazungumziwa namna ya kuvumilia na kustahamili machache ya mpito ili kupata hatma yenye neema zaidi. Mandela hakuzaliwa na ANC, lakini angeweza kutolewa mapema gerezani akawa mtu huru kama tu angekana madai ya ANC ya uhuru wa walio wengi. Alivumilia na kustahamili miaka 27 gerezani na akatoka akiwa mtu bora zaidi na nchi yake ikawa huru. Buffon hakuzaliwa na (timu ya ) Juventus, lakini akakubali kubaki nayo iliposhushwa Daraja na nakisi (deficit) tangulizi ya alama kadhaa za kuanzia Serie B. Matokeo yake akaipandisha tena na kuishia na heshima iliyoambatana na mapato mengi zaidi kuliko aliyoyakosa kwa kucheza Serie B msimu mzima. Fuatilia wafanikiwa wengi, kama siyo wote : Lukaku, Mwalim Nyerere, Diamond, Pele, Mzee Kenyatta, ...... na utabaini wamefikia mafanikio yao kwa kustahamili kwa makusudi adha ambazo kama wangependa wangeweza kuziepuka.
Aidha, hata kiuchezaji ndani ya dakika za mchezo, kunahitajika ustahamilivu wa makusudi ili uwe mchezaji bora zaidi. Huo haupatikani kwa mazoezi ya dawati la ufundi wala kwa kipaji cha mchezo wenyewe, bali hupatikana kwa kuizowesha nafsi kustahamili adha na karaha. Wanaoshindwa, hata wawe timamu kiasi gani kimwili, hata wawe na kipaji kiasi gani, wanashindwa kufikia kilele chao cha mafanikio na kukosesha timu au wapenzi wao na mataifa yao ladha ya uwezo wao. Mwangalie Tyson aliyeshindwa kustahamili adha za mchezoni hadi akaamua kumn’gata sikio Holyfield, ikawaje na amekuwaje? Hakuwa amechezewa rafu za makusudi kweli? Mwangalie Serena Williams aliyeshindwa kuvumilia uonevu wa mwamuzi na kumtolea maneno mabaya kwenye fainali ya US Open ya Tennis, ikawaje? Hakuwa timamu? Hakuwa ameonewa kweli?Mwangalie Zidane alivyoikosesha Ufaransa Kombe la Dunia kwa kushindwa kuhimili udhia. Unadhani hakuwa na timamu kimwili? Au hakuwa na kipaji? Hakuwa ameudhiwa kweli?
Mazoezi ya stahamala na uvumilvu kama huo hayapatikani uwanjani, wala hayanolewi na kauli za ‘nani hakuzaliwa wapi’. Yanapatikana kwa kujifunza kutoka kwa walioweza na walioshindwa, na kwa kuwasaidia vijana wetu pale tunapowaona wanaelekea kwenye kukosa mengi kwa sababu ya machache. Lau Samatta ambaye ‘hakuzaliwa Simba’ asingepewa gari aliyoahidiwa pale alipoamua kurudi timu yake ya mchangani, tungekuwa tunaimba wimbo wake hii leo?
Naomba ujifunze kutoka maisha ya Mahatma Gandhi, Mwasisi wa mataifa ya India, Pakistan na Bangladesh na uirithishe kwa Kakolanya na wenye mtizamo kama wake. Gandhi ametanabahisha kwamba kulipiza jicho kwa jicho kutaishia na dunia ya vipofu watupu (an eye for an eye will make the whole world blind). Wakatabahu.
 
Kwa Mara ya kwanza Leo umekomenti zaidi ya sentensi moja.
 
Ha ha ha ha safi ila sio tanzania.
 
Nlichogundua wengi humu mnachangia kwa kuongozwa na ushabiki usio na tija..... Yaani kwa kuwa mna mahaba na timu basi mko tayari kusimama nayo hata wakikosea mkidhani mnasaidia.... Mkataba mnaposaini unaweka majukumu ya pande zote mbili za klabu na mchezaji.... Yeye mchezaji ni kucheza mpira na timu ni kumpa stahiki zake sasa Yanga inapokiuka clause za mkataba inakuaje benno aonekane mbaya ilihali mchezaji akitoroka kambi au akichelewa mazoezini naye huwa amekiuka mkataba na huwa anaadhibiwa licha ya kuwa na sababi za msingi sasa kwanini mnaangalia upande mmoja??

Mtu hajalipwa pesa yake na ana matatizo mlitaka afanyeje?? Ana madeni mlitaka afanyeje?? Kwanini timu isikope imlipe??

Shida watu humu mnaongozwa na mahaba ndio maana mpira wa Tanzania haukuwi.... No wonder hakuna timu ya bongo imewahi fanya vzuri kimataifa maana mmejaa uswahili sana na ubabaishaji na washabiki wenyewe ndio wanafiki hivi hatutofika kokote.
 
Saiz national team tena basi tena,anadhani mafanikio ni rahisi sana
Kwahiyo mtu asidai haki zake kisa atakosa maslahi fulani ya muda mrefu?? Kubalini kwamba yanga ilikosea kuahidi kumlipa ilihali haina pesa sio mnamdhulumu mtu na pesa zake hamumpi.... Trust me akienda FIFA kama yule mkenya wa Yanga enzi hizo aliyewalipisha million 40 ndio mtaelewa kwamba dawa ya Deni ni kulipa sio kelele kelele na uswahili.

Nikuulize swali hivi mchezaji asipofuata mkataba mngemtetea hivi?? Kwanini timu isipofuata mnawatetea?? Hizi double standards zitawapeleka wapi??

Mwingine anakuja na hoja eti wengine hawadai?? Kwahiyo kwa kuwa wengine wamekubali kutapeliwa basi inajustify beno kutapeliwa pia??

Tubadilike kama tunataka kusaidia mpira wetu ukue otherwise tutaendelea kuwa wasindikizaji tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…