Kama ndo ukweli huu! Siungi mkono Beno kurejea Jangwani maana alimdharau Kocha

Kama ndo ukweli huu! Siungi mkono Beno kurejea Jangwani maana alimdharau Kocha

Kawe wewe kipa uzibe pengo lake acheni haki zake.mbona wewe hukua kipa.
Kwani kipa yuko peke ake Mzee.....? Si kashavunja mkataba tayari? Anataka nini tena? Mchukueni nyinyi mumpe hizo staiki zake, kwan anaedai staiki zake yuko peke yake....? Anataka kuvuruga team tu, Ata sisi uku tulipo tunadai zetu uku tunachapa mzigo kama kawaida Mzee!.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio msitupigie lelele hapa,kama akiomba msamaha akisamehewa utasemaje.Huruhusiwi kuhukumu jambo ambalo hujui mustakali wake.Hata kwenye siasa kuna maandamano.muacheni akija mfukuzeni.watanzania wengi hujadili jambo kwa mitizamo binafsi pekee badala ya kuchanganya na ya kijamii.
 
BENNO KAKOLANYA SIMAMA WEWE MWENYEWE.

Mambo yaliharibika zaidi mara baada ya kuondoka George Lwandamina, timu ikawa chini ya Noel Mwandila akisaidiwa na Shadrack Nsajigwa 'Fusso' . . wachezaji kugoma ikawa kawaida, hadi anawasili Mwinyi Zahera hiyo tabia iliendelea! Yanga SC ikawa ina unga unga kikosi, si unakumbuka ile safari ya Algeria kucheza na USM Alger? timu ilipowasili JKNIA kocha wetu alishangazwa sana na jinsi timu inavoenda kienyeji licha ya kuwa Yanga ni timu kubwa.

Baada ya michuano ya SportPesa kule Kenya kumalizika ndipo kwa mara ya kwanza Mwinyi Zahera aliwaita wachezaji wake , namnukuu

"Hii ni kazi na mnapaswa kuiheshimu, mnafahamu fika timu haina hela nataka tukubaliane kama huwezi kucheza bila kulipwa pesa yako basi naomba mapema kabisa nikuruhusu uondoke, ninyi mliomaliza mikataba yenu na bado mnatamani kuendelea hapa ningewashauri nyie sinyeni Yanga hela yenu mtaipata tu japo yawezekana isiwe leo ama kesho "

Baada ya hapo Mwalimu akawapa muda wachezaji wa kufikiri na kwenda kushauriana na watu wao wa karibu, Wachezaji wote waliridhia kuwa wapo tayari kuipigania Yanga licha ya changamoto za kipesa ndipo wengine wakasaini hata bila signing fees! Hapo ndipo Yanga ikawa kitu kimoja pasipo kuangalia sana maslahi ya kifedha, ukiwa na shida ya kipesa unamweleza mwalimu naye anatoa pesa yake na kukupatia, furaha ikarudi na umoja ukajengeka siku hadi siku.

Usiku wa kuamkia tarehe 4 November, 2018 majira ya saa 7 usiku timu ikiwa hotelini kocha mkuu akagongewa mlango na meneja wa timu! hata kabla ya kufungua kocha akasikia " Kocha, Kocha Benno anaondoka" . . . Zahera akafungua mlango haraka kisha akawaambia naomba mwiteni Benno, muwahini haraka! ndipo Benno akarudi na kukaa chumbani kwa kocha kwa maongezi.

"Benno kulikoni unataka kuondoka? tumefanya kikao saa 5 usiku kama una tatizo si ungenambia muda ule iweje usubiri tukiwa tumelala ndipo utoroke? kumbuka kama timu tulikubaliana kuwa tupo tayari kufanya kazi licha ya ukata, iweje utusaliti na unajua fika kesho tuna mechi ngumu dhidi ya Ndanda. . nakuomba baki hapa kama una shida sana tutaongea naomba tufocus kwa mchezo wa ujao kwanza" , Benno aliendelea kushikilia msimamo wake kuwa anaondoka, kuangalia nje kumbe tayari meneja wake amekuja kumchukua.

Simu za viongozi wala kocha akawa hapokei, baada ya wiki meneja wake akajitokeza kuwa anaupa uongozi wa Yanga siku 3 uwe umemlipa mteja wake la sivyo Benno atakuwa mchezaji huru! Siku tatu zikapita kisha wiki ikakatika ndipo Benno kwa kushirikiana na meneja wake wakawasilisha barua ya kuvunja mkataba Yanga SC.

Ghafla mbele ya waandishi wa habari , Benno akakabidhiwa milioni 2 kutoka kwa Cyprian Msiba kisha akaahidi sasa atarejea kambini kuitumikia Yanga ndipo akaonana na rungu zito la Zahera.

Mpaka hapo utaweza kugundua kwanini Mwinyi Zahera anagoma kumrudisha kikosini japo moyoni mwake anatamani sana kuwa na golikipa kama Benno kikosini mwake ila anatambua hasara ya kumpokea ni kubwa kuliko kumkataa, ukizingatia yeye ndiye aliyebeba maono ya timu! vijana wote ambao hawajalipwa lakini maslahi yao wameweka kando nao wanaufuatilia huu mchezo!

USHAURI WANGU!
Mwinyi Zahera ni muwakilishi wa hisia za kikosi chake, Kamwe Benno asitegemee msamaha binafsi kutoka kwa Zahera! Benno amewakosea na kuwasaliti wachezaji wenzie, Benchi la ufundi, viongozi na mashabiki wa Yanga SC! anachopaswa kufanya ajitokeze yeye binafsi na kulisimamia hili swala liishe aache kusemewa, aambatane na ndugu yake wa karibu wakawaombe msamaha wachezaji huko ndipo msamaha wake utaweza kupatikana sio kwa Zahera, wachezaji wakimsamehe kwa dhati wao ndio wataongea na mwalimu! kwa jinsi Zahera anavoishi na wanaye msitegemee akawa mwamuzi katika hili.

Hili jambo sio dogo kama mdhaniavyo, likichukuliwa kirahisi laweza kuleta mpasuko katika kikosi chetu na kuharibu heshima aliyojijengea mwalimu wetu, Benno acha kujiona star na kuamini nguvu ya mashabiki ndio itakayokurejesha kikosini! Omba msamaha wewe binafsi , kwa dhati kabisa watafute wachezaji, benchi la ufundi waombe msamaha amini nakwambia hao ndio wana password za kureset msimamo wa Zahera.

Copy and paste from Mr. Hissan Salum Iddi

"Wagogo wa Jangwani," kwa kweli hii timu ipo siku itakufa tu, kama si wachezaji kugoma basi viongozi wasio na manufaa klabuni watagombana kulilia ugoro wao.
 
Ndio msitupigie lelele hapa,kama akiomba msamaha akisamehewa utasemaje.Huruhusiwi kuhukumu jambo ambalo hujui mustakali wake.Hata kwenye siasa kuna maandamano.muacheni akija mfukuzeni.watanzania wengi hujadili jambo kwa mitizamo binafsi pekee badala ya kuchanganya na ya kijamii.
Stori yake ipo hadharani mpaka sasa... Inajulikana ni msaliti na msaliti ni msaliti tu....

Si tunamsikiza na kumsuport kocha wetu.....! Akisamehewa tutamsamehe pia asiposamehewa na Zaera si atumtaki kusiwe na nguvu ya kulazimisha arudi adi kocha azidiwe......!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio msitupigie lelele hapa,kama akiomba msamaha akisamehewa utasemaje.Huruhusiwi kuhukumu jambo ambalo hujui mustakali wake.Hata kwenye siasa kuna maandamano.muacheni akija mfukuzeni.watanzania wengi hujadili jambo kwa mitizamo binafsi pekee badala ya kuchanganya na ya kijamii.
kuwa mwelewa usiwe mbumbumbu ,kocha alishwambia atafute timu kabla dirisha halijafungwa mambo ya kusamehewa umeleta wewe.
 
Stori yake ipo hadharani mpaka sasa... Inajulikana ni msaliti na msaliti ni msaliti tu....

Si tunamsikiza na kumsuport kocha wetu.....! Akisamehewa tutamsamehe pia asiposamehewa na Zaera si atumtaki kusiwe na nguvu ya kulazimisha arudi adi kocha azidiwe......!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kocha kwanza, Beno baadaye
 
  • Thanks
Reactions: Oxx
Ndio msitupigie lelele hapa,kama akiomba msamaha akisamehewa utasemaje.Huruhusiwi kuhukumu jambo ambalo hujui mustakali wake.Hata kwenye siasa kuna maandamano.muacheni akija mfukuzeni.watanzania wengi hujadili jambo kwa mitizamo binafsi pekee badala ya kuchanganya na ya kijamii.
Hana chake kwa Timu ya wananchi
 
Anayejua annajua tu,ndio maana utumwa hauishi duniani.Wasomi mnajadili kama vichaa,Benno hakuzaliwa na yanga ana haki kukipigania kipaji na haki yake kwa ngivu zote.Atachezea timu zingine au hata akifa masikini kuliko kuwatumikia hao wachumia tumbo wa yanga.Siungi mkono hoja ya kubembeleza masikini.Na mkuu ukitaka kujua watanzania sisi wapuuzi subiri tetesi zitoke anaenda simba uone.Hakuna tunalolijua.
Hapa hapazungumziwi usomi wala u-Yanga. Panazungumziwa namna ya kuvumilia na kustahamili machache ya mpito ili kupata hatma yenye neema zaidi. Mandela hakuzaliwa na ANC, lakini angeweza kutolewa mapema gerezani akawa mtu huru kama tu angekana madai ya ANC ya uhuru wa walio wengi. Alivumilia na kustahamili miaka 27 gerezani na akatoka akiwa mtu bora zaidi na nchi yake ikawa huru. Buffon hakuzaliwa na (timu ya ) Juventus, lakini akakubali kubaki nayo iliposhushwa Daraja na nakisi (deficit) tangulizi ya alama kadhaa za kuanzia Serie B. Matokeo yake akaipandisha tena na kuishia na heshima iliyoambatana na mapato mengi zaidi kuliko aliyoyakosa kwa kucheza Serie B msimu mzima. Fuatilia wafanikiwa wengi, kama siyo wote : Lukaku, Mwalim Nyerere, Diamond, Pele, Mzee Kenyatta, ...... na utabaini wamefikia mafanikio yao kwa kustahamili kwa makusudi adha ambazo kama wangependa wangeweza kuziepuka.
Aidha, hata kiuchezaji ndani ya dakika za mchezo, kunahitajika ustahamilivu wa makusudi ili uwe mchezaji bora zaidi. Huo haupatikani kwa mazoezi ya dawati la ufundi wala kwa kipaji cha mchezo wenyewe, bali hupatikana kwa kuizowesha nafsi kustahamili adha na karaha. Wanaoshindwa, hata wawe timamu kiasi gani kimwili, hata wawe na kipaji kiasi gani, wanashindwa kufikia kilele chao cha mafanikio na kukosesha timu au wapenzi wao na mataifa yao ladha ya uwezo wao. Mwangalie Tyson aliyeshindwa kustahamili adha za mchezoni hadi akaamua kumn’gata sikio Holyfield, ikawaje na amekuwaje? Hakuwa amechezewa rafu za makusudi kweli? Mwangalie Serena Williams aliyeshindwa kuvumilia uonevu wa mwamuzi na kumtolea maneno mabaya kwenye fainali ya US Open ya Tennis, ikawaje? Hakuwa timamu? Hakuwa ameonewa kweli?Mwangalie Zidane alivyoikosesha Ufaransa Kombe la Dunia kwa kushindwa kuhimili udhia. Unadhani hakuwa na timamu kimwili? Au hakuwa na kipaji? Hakuwa ameudhiwa kweli?
Mazoezi ya stahamala na uvumilvu kama huo hayapatikani uwanjani, wala hayanolewi na kauli za ‘nani hakuzaliwa wapi’. Yanapatikana kwa kujifunza kutoka kwa walioweza na walioshindwa, na kwa kuwasaidia vijana wetu pale tunapowaona wanaelekea kwenye kukosa mengi kwa sababu ya machache. Lau Samatta ambaye ‘hakuzaliwa Simba’ asingepewa gari aliyoahidiwa pale alipoamua kurudi timu yake ya mchangani, tungekuwa tunaimba wimbo wake hii leo?
Naomba ujifunze kutoka maisha ya Mahatma Gandhi, Mwasisi wa mataifa ya India, Pakistan na Bangladesh na uirithishe kwa Kakolanya na wenye mtizamo kama wake. Gandhi ametanabahisha kwamba kulipiza jicho kwa jicho kutaishia na dunia ya vipofu watupu (an eye for an eye will make the whole world blind). Wakatabahu.
 
acheni janja janja.walipeni haki yao.
Tatizo lenu yanga uswahili mwingi.
Manji alishawaambia mpeni timu hamtaki mnataka awe mwenyekiti hapo hapo atoe hela zake mfukoni.
Hyo ni biashara KICHAA.
Mnataka timu iwe ya wanachama ila kuchangia hamtaki.
huyo zahera mkianza kufungwa mtakuja kumchukia JAPO leo Mnamuona ni mzalendo

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa Mara ya kwanza Leo umekomenti zaidi ya sentensi moja.
 
Hapa hapazungumziwi usomi wala u-Yanga. Panazungumziwa namna ya kuvumilia na kustahamili machache ya mpito ili kupata hatma yenye neema zaidi. Mandela hakuzaliwa na ANC, lakini angeweza kutolewa mapema gerezani akawa mtu huru kama tu angekana madai ya ANC ya uhuru wa walio wengi. Alivumilia na kustahamili miaka 27 gerezani na akatoka akiwa mtu bora zaidi na nchi yake ikawa huru. Buffon hakuzaliwa na (timu ya ) Juventus, lakini akakubali kubaki nayo iliposhushwa Daraja na nakisi (deficit) tangulizi ya alama kadhaa za kuanzia Serie B. Matokeo yake akaipandisha tena na kuishia na heshima iliyoambatana na mapato mengi zaidi kuliko aliyoyakosa kwa kucheza Serie B msimu mzima. Fuatilia wafanikiwa wengi, kama siyo wote : Lukaku, Mwalim Nyerere, Diamond, Pele, Mzee Kenyatta, ...... na utabaini wamefikia mafanikio yao kwa kustahamili kwa makusudi adha ambazo kama wangependa wangeweza kuziepuka.
Aidha, hata kiuchezaji ndani ya dakika za mchezo, kunahitajika ustahamilivu wa makusudi ili uwe mchezaji bora zaidi. Huo haupatikani kwa mazoezi ya dawati la ufundi wala kwa kipaji cha mchezo wenyewe, bali hupatikana kwa kuizowesha nafsi kustahamili adha na karaha. Wanaoshindwa, hata wawe timamu kiasi gani kimwili, hata wawe na kipaji kiasi gani, wanashindwa kufikia kilele chao cha mafanikio na kukosesha timu au wapenzi wao na mataifa yao ladha ya uwezo wao. Mwangalie Tyson aliyeshindwa kustahamili adha za mchezoni hadi akaamua kumn’gata sikio Holyfield, ikawaje na amekuwaje? Hakuwa amechezewa rafu za makusudi kweli? Mwangalie Serena Williams aliyeshindwa kuvumilia uonevu wa mwamuzi na kumtolea maneno mabaya kwenye fainali ya US Open ya Tennis, ikawaje? Hakuwa timamu? Hakuwa ameonewa kweli?Mwangalie Zidane alivyoikosesha Ufaransa Kombe la Dunia kwa kushindwa kuhimili udhia. Unadhani hakuwa na timamu kimwili? Au hakuwa na kipaji? Hakuwa ameudhiwa kweli?
Mazoezi ya stahamala na uvumilvu kama huo hayapatikani uwanjani, wala hayanolewi na kauli za ‘nani hakuzaliwa wapi’. Yanapatikana kwa kujifunza kutoka kwa walioweza na walioshindwa, na kwa kuwasaidia vijana wetu pale tunapowaona wanaelekea kwenye kukosa mengi kwa sababu ya machache. Lau Samatta ambaye ‘hakuzaliwa Simba’ asingepewa gari aliyoahidiwa pale alipoamua kurudi timu yake ya mchangani, tungekuwa tunaimba wimbo wake hii leo?
Naomba ujifunze kutoka maisha ya Mahatma Gandhi, Mwasisi wa mataifa ya India, Pakistan na Bangladesh na uirithishe kwa Kakolanya na wenye mtizamo kama wake. Gandhi ametanabahisha kwamba kulipiza jicho kwa jicho kutaishia na dunia ya vipofu watupu (an eye for an eye will make the whole world blind). Wakatabahu.
Ha ha ha ha safi ila sio tanzania.
 
Kwa wale wote wanaomuunga mkono kwa dhati Beno, naomba wabaki na muono wao huo mioyoni mwao. Kumlishia Beni msimamo huo ni kumpotosha. Kweli mpira ni ajira, kweli anastahili kulipwa, kweli si vyema familia kulala njaa huku anadai mshiko wake. Lakini msimamo wa kugoma na hatimaye kususiwa ni kujaribu hatimaye yake pana inayomsubiri kwa kutetea sasa yake finyu. Asidhani hao akina Christiano, Samatta, Messi na wengine wanaovuna mamilioni hivi sasa kuwa wanachopata ni mavuno ya juhudi zao pekee. Wanachopata ni mavuno ya kustahamili adha na karaha nyingi za ndani na nje ya uwanja, pengine kubwa kuliko hata hizo za Beno kutolipwa fedha yake; angalau posho la kila mechi alikuwa anapata, angalau alikuwa na mwalimu aliyetambua shida zake na akawa tayari kumsaidia, angalau adha hizo anazipata akiwa nchini kwao, angalau muda wote huo familia yake iko pamoja naye, angalau kuna wenye akili kama zake wanaomchochea na kumuunga mkono. Pitia maisha ya wachezaji kama akina Adebayor, Lukaku, Ronaldo Gaucho (Ronaldinho) na wachezaji wengi hasa wa Kiafrika wanaocheza soka la kulipwa Ulaya na utabaini kumbe hii inayoitwa adha ya Kakolanya si chochote.
Naomba tuwape moyo na Ushauri vijana wetu hawa ili vipawa vyao viwatumikie wao na sisi leo na kesho badala ya kuwaharibu kwa miono a kishabiki ambayo itaishia kutukosesha matunda ya vipawa hivyo sisi kama Taifa lakini zaidi wao kushindwa kunufaika na matunda mengi ya jasho lao jingi kwa kuendekeza kidogo wanachokosa hivi sasa.
Nlichogundua wengi humu mnachangia kwa kuongozwa na ushabiki usio na tija..... Yaani kwa kuwa mna mahaba na timu basi mko tayari kusimama nayo hata wakikosea mkidhani mnasaidia.... Mkataba mnaposaini unaweka majukumu ya pande zote mbili za klabu na mchezaji.... Yeye mchezaji ni kucheza mpira na timu ni kumpa stahiki zake sasa Yanga inapokiuka clause za mkataba inakuaje benno aonekane mbaya ilihali mchezaji akitoroka kambi au akichelewa mazoezini naye huwa amekiuka mkataba na huwa anaadhibiwa licha ya kuwa na sababi za msingi sasa kwanini mnaangalia upande mmoja??

Mtu hajalipwa pesa yake na ana matatizo mlitaka afanyeje?? Ana madeni mlitaka afanyeje?? Kwanini timu isikope imlipe??

Shida watu humu mnaongozwa na mahaba ndio maana mpira wa Tanzania haukuwi.... No wonder hakuna timu ya bongo imewahi fanya vzuri kimataifa maana mmejaa uswahili sana na ubabaishaji na washabiki wenyewe ndio wanafiki hivi hatutofika kokote.
 
Saiz national team tena basi tena,anadhani mafanikio ni rahisi sana
Kwahiyo mtu asidai haki zake kisa atakosa maslahi fulani ya muda mrefu?? Kubalini kwamba yanga ilikosea kuahidi kumlipa ilihali haina pesa sio mnamdhulumu mtu na pesa zake hamumpi.... Trust me akienda FIFA kama yule mkenya wa Yanga enzi hizo aliyewalipisha million 40 ndio mtaelewa kwamba dawa ya Deni ni kulipa sio kelele kelele na uswahili.

Nikuulize swali hivi mchezaji asipofuata mkataba mngemtetea hivi?? Kwanini timu isipofuata mnawatetea?? Hizi double standards zitawapeleka wapi??

Mwingine anakuja na hoja eti wengine hawadai?? Kwahiyo kwa kuwa wengine wamekubali kutapeliwa basi inajustify beno kutapeliwa pia??

Tubadilike kama tunataka kusaidia mpira wetu ukue otherwise tutaendelea kuwa wasindikizaji tu
 
Back
Top Bottom