Kama ndo ukweli huu! Siungi mkono Beno kurejea Jangwani maana alimdharau Kocha

Nahisi unahisi watu wote wako na ushabiki maandazi kwa sababu tu na wewe ndivyo ulivyo. Si kila ulivyo wewe ndivyo walivyo wengine. Hebu fuatilia mtiririko wa hoja zangu kwanza halafu unioneshe wapi nimesema Beno ni mbaya. Fuatilia mtiririko wa hoja zangu kama hutaona f nimetamka bila kugegeza kwamba si vyema mchezaji kukutwa na yaliyomkuta Beno. Kama umefuatilia kwa makini hoja zangu utabaini kwamba nimesisitiza Beno na kama yeye asaidiwe kujua namna ya kukabiliana na hali kama hiyo, vinginevyo anaweza kukosa kuvuna matunda ya kipaji chake naTaifa - siyo Yanga unayolazimisha kuwa ndiyo ninayoitetea - litakosa faida ya kipaji chake. Badala ya kukaa na kulaumu Utanzania na Uswahili kuwa ndiyo sumu ya mpira wetu, unaonaje ukaamua kuanza kubadilika wewe kwa kutaka kufahamu hoja kabla ya kuidandia? Kwa sababu naamini wewe tangu mwanzo unauchukuia na kuukataa Utanzania na Uswahili. Siamini kwamba kauli yako hiyo dhidi ya Uswahili na Utanzania imetokana na hoja yangu. Kwa sababu mimi kama ni Mtanzania au Mswahili basi ni mmoja tu. Hao wengine umewapata wapi wanaotosheleza kuharibu mpira wa Tanzania, kama tangu mwanzo hukuwa na mtizamo huo mbaya dhidi ya Watanzania na Waswahili?
 
kila siky huwa nasema Simba na Yanga zinaongozwa na watu ambao typically ni wahuni wa mjini.sishangai kwa haya tunayoyaona
 
Je wote wanaodai wangegoma timu si ingeshuka daraja,wewe hudai? Wewe hudaiwi? Kudaiwa ni utapeli?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nafkiri sentensi ya kwanza inaonyesha kuwa najibu collectively hoja zenu humu na sio yako specifically. Sababu wewe binafsi sijaona ukizungumzia kabisa suala la wajibu wa mkataba unakimbilia kushauri subjectively bila kuangalia upande wa mkataba kisheria unasemaje..... Nilitegemea wwe uwe mstari wa mbele kumshauri awashtaki Yanga FIFA alipwe pesa zake kwa kukiuka mkataba we unashauri avumilie kucheza bila kulipwa kama kina Adebayor?? Ilihali muda huo kuna viongozi wa Yanga wananufaika na pesa za timu na kufuja??

Inachopaswa ni washabiki wote kuwaambia Yanga waombe radhi na wamlipe hela zake maana ndio wajibu wao kwenye mkataba ila contrary naona mnataka ashauriwe vizuri na sio kusimamia msimamo wa sasa??
Mbaya zaidi kuna mwingine anashauri eti Benno ndio aombe radhi kisa kudai haki zake!! Hivi hatujui kama mtu amekiuka mkataba una haki ya kuvunja mkataba?? Yaani mambo ya kisheria mnataka muingizie busara cjui ujuaji mwingi wakati wanasaini mkataba Benno alipewa Masharti kibao ambayo naye angekiuka angetimuliwa ila sioni humu mtu akisema Benno kacheza nafasi yake wote ni lawama tu hivi mpira wetu utafika kokote??

Hakuna kuzunguka wote kwa sauti mmoja inatakiwa tumsupport beno sio kuingiza maoni yetu wakati yye anaumia na njaa it ain't fair kabisa
 
Je wote wanaodai wangegoma timu si ingeshuka daraja,wewe hudai? Wewe hudaiwi? Kudaiwa ni utapeli?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Timu lazima ionyeshe juhudi za kujali wachezaji mfano Borussia Dortmund iliwahi kukaribia kufilisika hata mishahara ya wachezaji ikakaribia kukauka walichofanya walienda kusaidiwa na mahasimu wao Bayern Munich na leo hii ipo vzuri kiuchumi mbona sijaona effort yeyote ya Yanga kulipa hayo madeni?? Klabu ni wachezaji sio majengo ni heri wauze hata assets za timu pesa ipatikani iwalipe wachezaji otherwise ni haki kabisa timu nzima ikigoma maana kisheria mikataba yao imekiukwa na hata wakienda FIFA wanashinda kesi

Let's be realistic guys.... Hata leeds ilipofulia iliuza mastaa wake wote ikaanza upyaa kama Yanga nao hawana pesa si iuze timu nzima iwalipe madeni yao ianze na wachezaji wa ACADEMY?? Kigumu kipi?? Yaani timu haina hela ila inataka ijaze mastaa..... Mkishindwa mnataka wachezaji ndio wateseke

Kwa staili hii mpira wetu huendi kokote
 
Mkuu zito hii nchi watu hawajui mpira ni ushabiki maandazi tu.
 
Beno yupo sahihi hta mbwa wako uliemfuga kama haumpi chakula lzma atakutoroka, na msimu wa kupeleka watoto shule ndio huu, vyura fc hatuwachangii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mpeni hela zake acheni kutafuta vichaka vya kuwanyima haki wachezaji wenu

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndugu yangu Yawezekana uko sahihi kwa kile unachosema. Lakini napenda nikueleze kitu kimoja ambacho wachezaji wengi wa mpira wa miguu wa Afrika Mashariki hawana. Kitu hicho ni uthubutu, kujituma kwa kutoa damu na jasho jingi wakati wa kutafuta mafanikio. Ukisikia simulizi za wachezaji wa Afrika Magharibi waliofanikiwa Ulaya utachoka. Wamepitia Changamoto nyingi sana hata kulala na njaa wakati wakitafuta mafanikio. Lakini leo hii Ulaya nzima imejaa wachezaji wa Afrika Magharibi. Wachezaji kutoka Afrika Mashariki ni kuwahesabu kama McDonald Maliga, Wanyama na Mbwana Samata. Tukubaliane huwezi kufanya kazi bila mshahara lakini inabidi uangalie na mwenendo wa kiuchumi wa firm/company unayofanyia kazi. Hapo ndio kuna kitu kinaitwa kugeuza Changamoto (challenge) kuwa fursa (opportunity). Zaidi jaribu kusoma historia ya mchezaji mmoja anaitwa C. Tiote nina imani utatoa machozi.
 
Mkuu uko sahihi Kuhusu madai ya Benno ila alichokisema Coach Zahera ni njia aliyotumia kudai maslahi. Kwanza Coach alikaa nao akawaeleza hali ya kiuchumi ya Timu na akatoa option kuwa ambaye anaona hawezi kucheza mpira kutokana na hali ilivyo kwenye Timu basi atafute Timu nyingine. Zaidi ya hapo Benno ameondoka usiku wa manane baada ya kupokea ushawishi kutoka next-door. Elimu elimu elimu inahitajika kwa wachezaji wetu. Ndio maana mambo ya mikataba huwa hayamshindi Emmanuel Okwi.
 
Yeah upo sahihi sana,vijana wa kibongo hawana Elimu yoyote, mwashiuya alipokuja yanga akaulizwa tukulipe shilling ngapi akasema laki tatu,wakamwambia tutakupa laki tano akachanganyikiwa kabisa....so hawana watu sahihi wa kuwaongoza
 
Shida ww huna taarifa za kutosha sakata la Beno ndo maana unalaumu,Ungekuwa welo infomudi,usingekuwa unateseka sana,hayo ya kutapeliana waulize ndugu zako waliokula hadi hela ya msiba wa mafisango
 
Mkuu Asprin jamaa kamtaja Mahtma Ghandi.
 
Beno hatukutako tena.

Siyo mtu wa kuhesabia pale unapotaka kuanza naye safari kwani atakuacha katikati ya jangwa. Ni mbinafsi. Anajali furaha yake. Hajali kazi yake. Hata mimi kama shabiki na mwanachama sitaki huyu msaliti arudi pale.
Once a snitch always a snitch.
Let karma hunt his ego. Pumbavu kabisa.
Hata uwe vipi bora kama nidhamu huna tunakutenga tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnachoshindwa kuelewa nyinyi mashabiki wa Simba ni kuwa mkataba unasainiwa kati ya pande mbili au zaidi. Pili, kila mkataba unaweza kuvunjwa wakati wowote ule, ili mradi pande hizo ziafikiane na terms. Kwa hiyo, kuna "terms" za kusaini mkataba na "terms" za kuvunja mkataba. Hilo bila ushabiki wote tunakubaliana.

Baada ya hapo, sasa tujadili issue ya Beno.
Yanga walikiuka "term(s)" za mkataba.kwa kutomlipa Beno, signing bonus. Yanga inawalipa mshahara wachezaji wake ila tatizo kubwa ni signing bonus.
Kuna waliolipwa nusu na kuna ambao hawajalipwa kabisa. Hili ni kosa kwa upande wa Yanga. Na wachezaji wana haki ya kuvunja mkataba na Yanga, na wakaendelea kuwa free agents.
Wakaombwa na kushauriwa na mwalimu, wakakubali kuichezea Yanga kwa sababu mbalimbali iwe kuwapa nafasi Yanga, ku showcase talents zao na kutumia muda huu kuongeza skills, kuwatunzia heshima mashabiki ambao wengine wamewaunga mkono tangu mchangani, na kulinda hadhi ya ligi na soka ya Tanzania kwa ujumla. Kwa hili nawapa heshima sana, na sitawalaumu hata wakifungwa mechi zote zitazofuata.

Kama walikubali hivyo, basi wawe hivyo na akitokea mchezaji au wachezaji wasiotaka kuendelea, basi waondoke watuachie timu yetu sisi tutachukua hata wachezaji wa kichangani. Lakini, kwa kufuata ushauri, wachezaji wengi wameanza kupata fedha na heshima kubwa kutoka kwa mashabiki. Yanga hiyohiyo mnayoita masikini inapanda ndege kuliko karibu timu zote na mzuka wa mashabiki wake hauna mfano.

Beno, amekataa kucheza bila kulipwa kwanza na sisi mashabiki tunakubali. Ila, atuache kwa sasa hivi, hatumtaki na wakimrudisha, wataleta mgogoro. Kwa hiyo bora aende Simba au Azam.
 
Maneno meeengi siasa tupu. Lipa hela ya dogo ana familia yule,mnataka huduma bure?mpira ni ajira,tena ingekuwa mimi nawapeleka mahakamani kabisa
 
Na shida ndio inaanzia hapa kwamba waliombwa?? Mi nikajua kuna commitment clause walisainishwa kuwa walipwe wasilipwe wasiache kucheza...... Kumbe ni maneno tu na sio sheria?? Sasa umeona wapi watu wanakubaliana kwa maneno?? Hivi leo nikisema Benno hakukubali hilo utakataaje ilihali hawakusaini mkataba wowote utakaowafunga kisheria kiasi kwamba wakikiuka watatimuliwa?? Sasa kama klabu zetu zinaongowa kiswahili hivi kwa maneno ya korido tutafika kweli??

Nimeshatoa mfano Leeds iliokuwa timu tishio Uingereza ilipokuwa inafilisika iliamua kuuza wachezaji wake mastaa sababu ingekosa hata mishahara sasa kwanini Yanga wasiige?? Kwanini msiuze hao mastaa wenye mishahara mikubwa mkaenda kusajili wachezaji wakujitolea ndio muwasainishe commitment clauses kuwa anacheza ila hakuna kulipwa? Kwanini hamko formal na washabiki hamuwaelezi ukweli viongozi wenu kuwa wamefeli kuendesha timu??

Actually timu ina umri mkubwa kuliko hata Tanzania ila inashindwa kuwa na assets za kuiendesha club wakati wa crisis kma hizi?? Hata uwanja tu mmeshindwa kujenga leo hii Azam ana uwanja na financial capacity kuliko timu zenu kongwe?? Badala mshauri mabadiliko mmekalia kuleta mahaba kwa timu..... Hii haisaidii kabisa.

Wachezaji kususa ni kawaida mkuu hata Diego Costa aliweka mgomo baridi kusikia griezmann analipwa mara 4 kuliko yeye ila muhimu muwape haki zao kma hamuwezi muwauze sio kuwatesa hivi alafu wakishindwa mnaanza kuwatukana

Huyo zahera haelewi mpira wa bongo siku akikosa ligi na simba ikamfunga kma 6-0 kama naona mtakavyomgeuka na kumtimua na matusi juu.... Yetu macho na masikio
 
Ndio tumeshashindwa kumlipa... Kaandika barua ya kuvunja mkataba ...basis atulie au aende kamati ya hadhi za wachezaji ama mahakama ya michezo lakini sii kurudi tena alipoomba mkataba uvunjwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…