Kama ndo ukweli huu! Siungi mkono Beno kurejea Jangwani maana alimdharau Kocha

Kama ndo ukweli huu! Siungi mkono Beno kurejea Jangwani maana alimdharau Kocha

Mkuu nafkiri sentensi ya kwanza inaonyesha kuwa najibu collectively hoja zenu humu na sio yako specifically. Sababu wewe binafsi sijaona ukizungumzia kabisa suala la wajibu wa mkataba unakimbilia kushauri subjectively bila kuangalia upande wa mkataba kisheria unasemaje..... Nilitegemea wwe uwe mstari wa mbele kumshauri awashtaki Yanga FIFA alipwe pesa zake kwa kukiuka mkataba we unashauri avumilie kucheza bila kulipwa kama kina Adebayor?? Ilihali muda huo kuna viongozi wa Yanga wananufaika na pesa za timu na kufuja??

Inachopaswa ni washabiki wote kuwaambia Yanga waombe radhi na wamlipe hela zake maana ndio wajibu wao kwenye mkataba ila contrary naona mnataka ashauriwe vizuri na sio kusimamia msimamo wa sasa??
Mbaya zaidi kuna mwingine anashauri eti Benno ndio aombe radhi kisa kudai haki zake!! Hivi hatujui kama mtu amekiuka mkataba una haki ya kuvunja mkataba?? Yaani mambo ya kisheria mnataka muingizie busara cjui ujuaji mwingi wakati wanasaini mkataba Benno alipewa Masharti kibao ambayo naye angekiuka angetimuliwa ila sioni humu mtu akisema Benno kacheza nafasi yake wote ni lawama tu hivi mpira wetu utafika kokote??

Hakuna kuzunguka wote kwa sauti mmoja inatakiwa tumsupport beno sio kuingiza maoni yetu wakati yye anaumia na njaa it ain't fair kabisa
Acha maneno mingi ...ameshavunja mkataba aende mbele zaidi anapoona panamfaa lakini sio Yanga tena
 
Na shida ndio inaanzia hapa kwamba waliombwa?? Mi nikajua kuna commitment clause walisainishwa kuwa walipwe wasilipwe wasiache kucheza...... Kumbe ni maneno tu na sio sheria?? Sasa umeona wapi watu wanakubaliana kwa maneno?? Hivi leo nikisema Benno hakukubali hilo utakataaje ilihali hawakusaini mkataba wowote utakaowafunga kisheria kiasi kwamba wakikiuka watatimuliwa?? Sasa kama klabu zetu zinaongowa kiswahili hivi kwa maneno ya korido tutafika kweli??

Nimeshatoa mfano Leeds iliokuwa timu tishio Uingereza ilipokuwa inafilisika iliamua kuuza wachezaji wake mastaa sababu ingekosa hata mishahara sasa kwanini Yanga wasiige?? Kwanini msiuze hao mastaa wenye mishahara mikubwa mkaenda kusajili wachezaji wakujitolea ndio muwasainishe commitment clauses kuwa anacheza ila hakuna kulipwa? Kwanini hamko formal na washabiki hamuwaelezi ukweli viongozi wenu kuwa wamefeli kuendesha timu??

Actually timu ina umri mkubwa kuliko hata Tanzania ila inashindwa kuwa na assets za kuiendesha club wakati wa crisis kma hizi?? Hata uwanja tu mmeshindwa kujenga leo hii Azam ana uwanja na financial capacity kuliko timu zenu kongwe?? Badala mshauri mabadiliko mmekalia kuleta mahaba kwa timu..... Hii haisaidii kabisa.

Wachezaji kususa ni kawaida mkuu hata Diego Costa aliweka mgomo baridi kusikia griezmann analipwa mara 4 kuliko yeye ila muhimu muwape haki zao kma hamuwezi muwauze sio kuwatesa hivi alafu wakishindwa mnaanza kuwatukana

Huyo zahera haelewi mpira wa bongo siku akikosa ligi na simba ikamfunga kma 6-0 kama naona mtakavyomgeuka na kumtimua na matusi juu.... Yetu macho na masikio
Hakuna mtu aliyesainishwa .eti lazima acheze. Mchezaji yeyote anaweza kuamua kuacha na kuondoka hata wachezaji wa Simba wakitaka. Hakuna contract isiyoweza vunjwa, as long as terms are met.
Coastal Union ni timu kongwe pia, mbona hailipi vizuri?
Pia, tusilazimishe kuwa mfumo fulani ndio effective, mbona hatuoni results za hizi major investments?
 
Hakuna mtu aliyesainishwa .eti lazima acheze. Mchezaji yeyote anaweza kuamua kuacha na kuondoka hata wachezaji wa Simba wakitaka. Hakuna contract isiyoweza vunjwa, as long as terms are met.
Coastal Union ni timu kongwe pia, mbona hailipi vizuri?
Pia, tusilazimishe kuwa mfumo fulani ndio effective, mbona hatuoni results za hizi major investments?
Then, soka la Bongo halijawa biashara kiivo ndo maana bingwa napewa million 70-80 lakini unasikia anasajiliwa mchezaji million 100
 
Etoo akiwa kapteni wa timu ya taifa alishawahi kuongoza mgomo kwa sababu malipo
Eto alikuwa anatoa hela yake kwaajili ya wenzake alichokifanya ni kuwapinga viongozi wa shirikisho kutotoa posho wakati hela ipo
 
Stori yake ipo hadharani mpaka sasa... Inajulikana ni msaliti na msaliti ni msaliti tu....

Si tunamsikiza na kumsuport kocha wetu.....! Akisamehewa tutamsamehe pia asiposamehewa na Zaera si atumtaki kusiwe na nguvu ya kulazimisha arudi adi kocha azidiwe......!

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa akimsamehe mtatulia sio
 
Kwahiyo mtu asidai haki zake kisa atakosa maslahi fulani ya muda mrefu?? Kubalini kwamba yanga ilikosea kuahidi kumlipa ilihali haina pesa sio mnamdhulumu mtu na pesa zake hamumpi.... Trust me akienda FIFA kama yule mkenya wa Yanga enzi hizo aliyewalipisha million 40 ndio mtaelewa kwamba dawa ya Deni ni kulipa sio kelele kelele na uswahili.

Nikuulize swali hivi mchezaji asipofuata mkataba mngemtetea hivi?? Kwanini timu isipofuata mnawatetea?? Hizi double standards zitawapeleka wapi??

Mwingine anakuja na hoja eti wengine hawadai?? Kwahiyo kwa kuwa wengine wamekubali kutapeliwa basi inajustify beno kutapeliwa pia??

Tubadilike kama tunataka kusaidia mpira wetu ukue otherwise tutaendelea kuwa wasindikizaji tu
Kwa kurudi yanga ndiyo haki yake imetendeka? Mimi nadhani watetezi wake wange mshauri kutumia vyombo husika kadiri ya mkataba wake, badala ya kushinda mnalia humu kwenye mitandao.
Ombeni awaonyeshe mkataba unaosema usipolipwa gomea mechi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwakukaa Nje muda mrefu kama Ana akili ya kutambua hilo itamuadhiri Kiwango chake bora hata kipa mwenzake Ivo mapunda alimshauri aangalie kwanza kiwango maslahi baadae , bado kijana mdogo akiwa na kiwango bora atatajirika tatizo wachezaji wengi wa bongo sio wote hawana tabia ya kusubiri mafanikio na kuwa na Malengo ya muda mrefu.
Je wakati anasajiliwa na Yanga alikuwa na huyo meneja wake aliyemshauri kutoroka kambi?
Atatajirikaje wakati timu yake haimpi pesa zake halali ?
 
Thanks...Ila Beno kamwe hawezi kurudi Yanga...inavyoonekana meneja wake ambaye ni kiongozi wa Simba alikula njama na wanasimba wenzake kuhakikisha Yanga inahujumiwa ...Kwa hiyo huyo meneja atalazimika kumtafutia timu huyo anayeitwa Beno..na ni vema asajiliwe Simba, ila kwa Yanga hawezi kurudi tena...Yanga wana msimamo..mamluki hawatakiwi kabisa ndani ya Yanga...Na kwa kusema ukweli huo ndiyo mwisho wa soka ya Beno...hakuna mchezaji aliyewahi kuisaliti Yanga na akaendelea kuwika huko aendako...Hovyo kabisa huyo Beno...alijua kuwa yeye ni mtu mhimu ndani ya kikosi kutokana na alivyodaka siku ya mechi ya dhidi ya Simba..magazeti yakampamba na akavimbishwa kichwa..ma-simba yakaona kuwa huo ndio ulikuwa wakati wa kuihujumu Yanga kwa hiyo wakamshawishi aisaliti timu...awaulize akina Munishi, Niyonzima na Bartez...Munishi au Dida sasa anashindwa kudaka hata mpira uliopigwa mita 30...huyo Bartez toka alivyofungwa goli la 'kinamna' la Kichuya la mpira wa kona, ndiyo basi tena...huyo Niyonzima akairingia Yanga pamoja na ukweli ilimsaidia mno pamoja na mmoja wa wazazi wake, akaenda Simba sasa huko anakula wa 'chuya'...list ya walioisaliti Yanga na wakaharibikiwa ni wengi...
Acha kumtishia Simba wa kuchora wewe mpira siku hizi pesa sasa mtu anadai chake mnamuita msaliti ??
 
Acha kumtishia Simba wa kuchora wewe mpira siku hizi pesa sasa mtu anadai chake mnamuita msaliti ??

Jibu lake ni rahisi...kwa wapenzi wa Simba Beno siyo msaliti ila kwa wanajangwani Beno ni msaliti na hawezi kurudishwa Yanga...kama mnamtaka nyie Simba mchukueni...
 
Jibu lake ni rahisi...kwa wapenzi wa Simba Beno siyo msilati ila kwa wanajangwani Beno ni msaliti na hawezi kurudishwa Yanga...kama mnamtaka nyie Simba mchukueni...
Hii ni dunia ya kibepari pesa ndo kila kitu kwa hiyo mnamkosea heshima Kakolanya kudai hela zake !!!!
 
Hii ni dunia ya kibepari pesa ndo kila kitu kwa hiyo mnamkosea heshima Kakolanya kudai hela zake !!!!

Yaani huyo Kakolanya alikuwaq ana hela zake Yanga??!! This is interesting....Aliziachaje huko??? Anyway tukija kwenye point yako ni ubepari wa wapi unaosema kuwa 'unaruhusiwa' kugoma?...Ubepari ninaoufahamu mimi umeweka njia za kutatua kama ipo migogoro ...kama una madai mahali basi unafuata procedures...unatumia ngazi zilizopo...kwa upande wa mpira unaweza kwenda kwenye ngazi ya TFF na pengine hata baadhi ya vyombo vya dola..au ukiona TFF inakusumbua unaenda huko kwenye vyombo vya FIFA kutatua tatizo lililopo...ubepari hautaki migomo ya kijinga...sasa huyo Beno 'wenu' akadanganywa na huyo meneja wake...timu imo kambini yeye meneja wake inasemekana akaenda huko usiku wa manane akawa anamsubiri kwenye gari...inawezekana mi-simba ilikula njama ikaona njia ya kuihujumu Yanga ni kumshawishi huyo Beno agome au asusie timu ili kushinikiza kinachoitwa madai yake...This is against capitalism...sasa Yanga wakaona isiwe neno wakamwacha...sasa huyo Beno hawezi kupata madai yake, kwani amegoma which is against sheria za kazi...
 
hivi umeshawaona wale wachezaji wa zamani waliocheza mpira kwa mapenzi hali zao zikoje, Benno kachagua mpira kuwa ajira yake na nyinyi mnatakiwa kumlipa sio kuanza kukoroma wakati pesa hamna.Hivi hapa nani anaweza kufanya kazi bila kulipwa hao watumishi wa serikali ikifika tarehe 25 mshahara haujatoka utaona post kibao za kulaumu serikali lakini nyie mnamshutumu bila kujua huyu mtu ana majukumu yake na familia yake nyinyi mnaomshutumu ndio nyinyi ambao mtamcheka baadae wakati amefulia mnyonge mnyongeni haki yake mpeni
Mchukue ukamtafutie timu yenye pesa yanga hawamtaki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anayejua annajua tu,ndio maana utumwa hauishi duniani.Wasomi mnajadili kama vichaa,Benno hakuzaliwa na yanga ana haki kukipigania kipaji na haki yake kwa ngivu zote.Atachezea timu zingine au hata akifa masikini kuliko kuwatumikia hao wachumia tumbo wa yanga.Siungi mkono hoja ya kubembeleza masikini.Na mkuu ukitaka kujua watanzania sisi wapuuzi subiri tetesi zitoke anaenda simba uone.Hakuna tunalolijua.
Mbona anatuma watu kuomba harudishwe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom