Kama ndo unakufa leo ushauri gani ingempa kijana anaemaliza kidato cha nne mwaka 2018

Kama ndo unakufa leo ushauri gani ingempa kijana anaemaliza kidato cha nne mwaka 2018

Tairus

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2013
Posts
676
Reaction score
1,056
Niwe wa kwanza kumshauri bila kupoteza muda.
Apende na azingatie sana MUDA
Kila jambo alifanye kwa muda wake...
Ajali sana matumizi mazuri ya PESA.
Pesa ni kama maua...
Atambue umuhimu wa JAMII inayomzunguka.
Apende kusaidia na kushiriki katika maswala ya jamii...
Awekeze sana kwenye kusoma VITABU
Asome vitu mbalimbali sio vya darasani tuu.
MITANDAO ya kijamii aitumie vizuri.
Ajue kuna kila aina ya watu atakutana nao huko na fursa kibao...
Apende sana kufanya KAZI
Amjue MUNGU wake na asipende VILEVI kwan bado hajafikia level ya kuweka vitu.
Ajifunze kiwa na MALENGO
Ajue anataka kuwa nani maishan
MARAFIKI pia aanglie sana asije ongozana na marafiki wabaya wakampotosha.
Ile ndoto ya kuwa RAISI kama anayo namshauri aachane nayo kwanza kwan haina uhalisia (realistic) awe na ndoto ambayo itampa changamoto za kutatua kwanza matatizo yake ya kila siku.
Apende kuwa MSIKIVU kuliko kuongea


Ushauri ninao mwingi lakini kila mtu najua angesema la kwake kutoka moyoni analoamini litamsaidia kijana huyu anapoingia mtaani.
Nakaribisha japo kwa sentesi moja tuu..mfano,huyo dada/kaka anayezani ndio atakuja kuwa mke/mme wake afikirie mambo mengine kwanza uwezekano ni mdogo sana.
Asanteni.
 
Vp mtihani ulikuaje.. Utafaulu kweli au tukupeleke gereji
Nacheka apa kuona ulivyojingeza kwenye matumizi ya mitandao hii kwa kujiita keki ya harusi upate wateja fasta at least uko smart. but y asking silly questions.Am a professional Accountant CPA T.
 
Nacheka apa kuona ulivyojingeza kwenye matumizi ya mitandao hii kwa kujiita keki ya harusi upate wateja fasta at least uko smart. but y asking silly questions.Am a professional Accountant CPA T.
Hongera professional account Mwenye CPA
 
Mleta uzi ungesema tu tuwape ushauri vijana wetu, kifo kione tu kwa jirani!! Muhimu wajifunze kuwa wazalendo wasiwe kama wale wabunge ambao wanaendelea kutuingiza gharama za kurudia uchaguzi pasipo na sababu
 
Maisha yakimshinda aachane nayo afanye mambo mengine.
 
Huyo bado yupo kwa wazazi, waendelee kumpa malezi bora, akifikia elimu ya juu na kuhitimu tutampa ushauri jinsi ya kukabiliana na mtaa
 
Mwambie ajifunze kuishi bila hisia... the world is fucked up haihitaji watu wa hisia hisia sijui moyo umefanyaje.. aishi kwa akili zaidi lasivo atapata tabu sana
 
Back
Top Bottom