Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
Maandalizi ya Sabato yanasemaje?
1. Ndugu zangu kuna msemo unasema mtu mzima hatishiwi Nyau. Ule msemo unaamana kubwa sana. Ambayo hivi karibuni umetaka kudhihirika machoni petu.
2. Tumeona vyombo vya dola na usalama vikitumia nguvu kubwa kabla na wakati wa uchaguzi. Vitisho, utekaji na sasa yakawa mauaji ya halaiki.
3. Wale watu waliokuwa wakikimbia mabomu na risasi, siku ya tarehe 29 ni watu wazima. Sio kwamba walikimbia kwa kuogopa au kutishika. Walikimbia kwa sababu hawakuwa na silaha. Huo ndio ukweli.
4. Sasa wote tunakubaliana kuwa vitisho sio mbinu pekee inayotosha kuleta utulivu na amani. Isipokuwa kuna njia nyingine muhimu kama mawasiliano na masikilizano.
5. Hata mzazi unaposhika fimbo kumchapa mtoto. Ukimuonea mara kwa mara anaweza mtoto huyo akakudhuru.
6. Vitisho na kuteka na kuua kunaongeza mgogoro na kupanua wahusika ndani ya vita. Hata wale waliofikiri hawatahusika watajikuta wanahusika na kuchagua upande. Na siku zote wananchi watakaa upande wa wananchi wenzao. Maskini watakaa na maskini wenzao.
7. Kuendelea kuua ni kuligawa na kulitia jeshi mashakani na kutaka kuligawa kwani hata ndani ya jeshi baadhi ya wanausalama ndugu zao watakutwa na kisanga na itawauma.
8. Lazima ieleweke kadiri ugomvi unavyokuwa mkubwa ndivyo watawala na vyombo vya dola vitakavyogawanyika na mwisho wa siku vitamtelekeza kiongozi mkuu na yeye ndiye atakuwa responsible. Na atapewa lawama.
9. Kwenye migogoro kama hii waliokuwa kwenye wakati mgumu ni viongozi wa juu kabisa wa maamuzi kwani wao ndio wataachiwa Zigo la misumari na ikiwezekana kushambuliwa na viongozi wa chini na askari wa chini.
10. Ikishatokea situation kama iliyotokea tarehe 29 ambayo mpaka sasa bado naitafakari ilikuwaje kuwaje. Na likatolewa tangazo jingine kubwa kutakuwa na maandamano ya 9/12/2025 inaleta hofu na kuchanganyikiwa sio tuu kwa wananchi bali hata kwa viongozi wa juu na dola.
11. Ni mtu mwenye uelewa mdogo wa saikolojia ya binadamu ambaye ataweza kupuuza mambo kama haya.
12. Mbinu zilizotumika kwenye 29oct bila shaka hazipaswi kufikiriwa tena hata kidogo kuelekea 9/12.
13. Kwa sababu 29oct imeathiri mambo yafuatayo;
a) Watu wengi wamekufa na hii imeongeza wahusika na hasira za watu. So agenda hii pia imeongezeka.
b) Imani ya watu ndani ya jeshi la wananchi, polisi na vyombo vyote vya dola imeshuka sana.
Ninapitia mara kwa mara maoni ya watu kuhusu vyombo vyetu vya dola. Hatuwezi kujidanganya imani ya watu kuhusu vyombo vyetu vya dola imeshuka. Na lazima hilo liangaliwe na liwe sehemu ya agenda kwa vyombo vya dola vijue vinafanya nini kurejesha imani yao kwa watu.
Asitokee mtu akasema ni watu wajinga au wenye chuki binafsi nope! Kuna mambo sio yakuleta siasa. Yale ni maoni ya watanzania na kama yamekuwa zaidi ya watu mia au elfu lazima yafuatiliwe.
Ni hatari wananchi kukosa imani na jeshi lao kwani wao watatafuta namna ya kujilinda jambo ambalo halitakuwa zuri kiusalama hasa kwa taifa.
c) Chuki kwa viongozi hasa wa ccm imeongezeka kwa vijana wa Gen Z.
Ni muhimu ieleweke kwamba kila mtu anahaki ya kuchagua chama cha siasa. Lakini inapotokea chama kimoja kinajipa mamlaka kuliko vyama vingine hiyo huleta mpasuka ndani ya nchi hasa kwa vijana wa Gen Z.
Sio jambo zuri na ni uhalifu kuona vijana wakichoma mali za wanachama wa chama kingine. Lakini lazima tujiulize kwa nini wachome mali hizo? Ni uhalifu ndio lakini kila uhalifu una sababu.
14. Hivyo basi kwa madhara machache hayo yaliyotokea kuna mambo yanatakiwa yafanyike kwa usahihi sana ili kuliweka taifa pamoja na kupunguza hasira za waandamanaji ambao bila shaka wataandamana.
Mambo hayo ni kama ifuatavyo;
a) Viongozi wote wa kisiasa kuachiliwa na waliokamatwa kwenye maandamano kuachiwa.
Hili limefanyika. Hii ni hatua nzuri.
b) Kuzuia MACHAWA wote kujihusisha na siasa au viongozi kwa namna yoyote.
Nataka niwaambie moja ya watu watakaoliletea shida hili taifa ni machawa. Nakuhakikishia machawa wasipopigwa marufuku watatuharibia nchi.
Machawa ni kama malaya fulani hivi ambao wao hupamba viongozi bila kuangalia muktadha.
Machawa wamechangia pakubwa kuongeza mgogoro.
Watu wametekwa, watu wameuawa, mtu analalamika ndugu yake katekwa linatokea jitu huko linakuambia fulani amejiteka, mara fulani kajipiga risasi, sijui blablaa! Serikali ipo kimya. Wananchi wanalalamika mpaka wanabaki wanalia kama samaki majini. Hasira zinajaa. Ndugu zangu acheni masikhara na maisha ya watu.
c) Kustopisha genge la wasiojulikana.
Hakuna mtu hajui wasiojulikana ni kuja nani. Huyo mtu hayupo kwenye nchi hii.
Hivi tuache ushabiki, tujiulize nini sababu ya uwepo wa wasiojulikana? Kwamba sheria za polisi za ukamataji, huko mahakamani hazifanyi kazi ipasavyo mpaka ifikie hatua tutumie njia za kihuni na kihalifu kudhibiti baadhi ya mambo?
Kwamba mtu kamtukana Rais si ndio. Labda ni mtandaoni si ndio.
Kwamba atekwe ndio na isijulikane alipo ndio njia sahihi.
Oooh! TaikonMaster tulia hujui lolote. Tukikamata tutakamata wangapi. Watakuwa wengi. So. Tunateka ili tutishe wengine. Nope! Hiyo sio sawa.
Hii nchi ipo nyuma kwa mambo mengi sana. Haina madarasa, Hospitali ni chache,
Sasa hao vijana kama wanatukana watu ikiwemo viongozi huko mitandaoni si muwakamate, pelekeni mahakamani, kisha wakafyatue matofali au kuzalisha mali au kusafisha maeneo au kulima.
Maana vijana huenda hawana kazi mnataka wafanyaje?
Oooh! Robert bhana Una mawazo ya kijinga. Sasa hao vijana tukiwapa kazi ya kufyatua matofali makampuni yetu ya ujenzi yatapata wapi pesa? Oooh! So bora tuwateke na kuwapoteza?
Wakamatwe kisha yapeni hayo makampuni vijana wakafanye vibarua wapate, vijana watapewa percent, serikali inachukua kodi yake na hizo kampuni zinapata pesa.
Kuna mashamba ya mkonge huko ya Mo dewji, pelekeni vijana huko, kuna mashamba ya chai, n.k.
Hiyo ni mifano tuu.
So hakuna umuhimu wa kuteka na kuua vijana ambao ni ndugu zetu ndani ya nchi yetu wenyewe. Huko ni kuharibu nchi na kuiletea matatizo.
d) Rais Samia asiongee mara kwa mara kwa kipindi hiki. Na akiongea aongee mambo kusapoti vijana hasa Gen Z.
Sio uwaambia waache matusi, sijui wawe na maadili. Nope!
Pale Kenya Ruto aliweza kucheza na akili ya Gen Z. Wanamuita Kasongo Yeye. Ruto hata kama jina hilo linamkera au kumshushia heshima lakini aliamua kujishusha na kutochukulia serious sana mambo. Siku moja aliamua kuwaambia wamuwekee wimbo wa Kasonge naye akacheza.
Vijana wanahali ngumu lazima tulitambue hilo. Tuvae viatu vyao. Wakituona sisi wakubwa tunatembelea magari na kujivuna kwa majigambo huku wakijua ni kodi zetu inawakereketa.
Rais Samia asichukulie mambo too personal. Na vyombo vya usalama pia vichukulie hawa watoto ni kama watoto wao nyumbani waliowazaa.
Dawa ya mtoto mtukutu ni upendo, kumuadhibu kwa haki, kumpongeza anapofanya vizuri, kumfundisha na kumuonyesha njia sahihi ya kupita.
Serikali inapaswa ipige marufuku uchawa na mambo ya kipuuzi puuzi yanayotrendishwa mtandaoni na kwenye media.
Na sio lazima itoe kauli au tamko bali kwa kusapoti vijana wenye mchango chanya ndani ya nchi, kuwapromoti vijana wafugaji, wenye viwanda, bodaboda, wavuvi na wale wa entertainment maudhui yao yalenge kuhamasisha uzalishaji kwa mikono, ujuzi na taaluma.
Sio kufikiria ushoga ushoga, umario, kutoka na mishangazi na mitabia ya ajabu ajabu.
e) Lazima wakutolewa Kafara wawepo.
Kile kilichotokea 29 ni kibaya. Hapana shaka bado kina rotate kwenwy mioyo na vichwa vya watu.
Najua kutenda haki kwa asilimia mia moja hilo ni ngumu sana. Huu ni ukweli lakini Kafara lazima itolewe.
Ili kutuliza hali ilivyo.
Mbinu ya kutoa watu ladhaa kafara kwa kuzingatia waliotoa amri na kutekeleza amri hiyo ambao hapa ni askari basi hali inaweza isipoe.
Mbinu hii ni ngumu kwa sababu nani wakumtoa kafara. Na idadi yao ni ipi! Na athari yake ni ipi kwa wengine waliobaki?
Hapo ndipo pagumu.
Askari atasema mimi ulinituma kazi nikatii amri kama kiapo kisemavyo. Huyu atasema lakini ulipaswa kutii amri halali tuu. Haya utamfunga.
Askari waliobaki wataanza minong'ono na kuweka mgomo wa kutotii amri zisizo halali. Je utawala utakuwa tayari?
f) Maandamano ya D9 serikali ijiingize huko na iyaratibu.
Ndio mabadiliko yenyewe hayo. Unajua kukubali mabadiliko ni kazi sana. Na inahitaji muda.
Tunajua kwenye taifa letu hatuna utamaduni wa kuwapinga wakubwa. Tulilelewa na desturi isemayo mkubwa hakosei. Hiyo ndio imetukuza sisi tuliozaliwa nyuma ya Gen Z.
Yaani hata Baba akosee haupaswi kumkosoa. Huo ni utamaduni wetu Afrika.
Lakini kizazi hiki hakikubali mila hiyo. Sisi wenyewe kama wazazi tunajua tunakosea lakini hatukubali kuambia makosa yetu hasa na watoto au wadogo zetu.
Gen Z wao wanataka ukweli na haki. Tusipowapa ukweli kwa njia ya kawaida basi ndio haya ya maandamano yanajiri. Tunapotumia nguvu kuwazuia tunajenga mpasuko na kuvuruga utulivu wa nchi.
Serikali hakuna namna ya kupambana na wakati hiyo namna haipo. Na kama tutajaribu kufanya hivyo tutajikuta kwenty hatari ya kuliangamiza taifa. Na kudondoka chini.
Mataifa mengi yaliyoshindwa kwendana na wakati yamejikuta katika wakati mgumu.
Mtu fulani ataniambia, wewe Robert wewee. Mbona China, Kore kaskazini, sijui Urusi, Saudia n.k. mbona wao serikali imedhibiti wananchi na vijana wapo tuli. Ndugu yangu, sisi tupo mixed culture mpaka sasa. Ni kama kokoro tunachukua tamaduni zozote kutoka nje ya nchi zipo za waarabu humuhumu, zipo za wazungu humu humu, zipo za kiafrika humuhumu, na mataifa mengine.
Serikali kushindwa kudhibiti utamaduni wa jamii yetu ni moja ya kuwapa nguvu Gen Z.
Lakini pamoja na hivyo wakati ni sababu nyingine. Hata hayo mataifa ya Uchina sio kwamba yatabaki hivyo yalivyo siku zote nope! Huu ni wakati wa vijana kuelekea kwenye kutaka uhuru, kweli na Haki.
g) Ahadi ya mabadiliko ya Katiba Mpya.
Hii inaweza kuwa mbinu bora ya kujisafisha ikiwa ndani ya hizo siku 100 itatokea ile katiba inayofuata maoni ya wananchi wote.
Kimsingi hii inaweza kuwa kete muhimu ya kuombea msamaha au kitubio
Kwamba NO MORE BLOOD mnataka katiba mpya hiyo hapo.
Tume ya uchaguzi yenye vipengele vinavyotoa haki na usawa kwa vyama vyote hivyo hapo
Hapo hata zile damu zilizomwagika zitatulia na itakuwa kama kafara la ondoleo la dhambi ya ukandamizaji.
Kuhusu mafisadi wananchi wanaweza kusamehe mafisadi kwa masharti ya kurudisha pesa zote nchini na kuwekeza hapa hapa nchini.
Jambo ambalo bado naliona ni gumu kwa sababu ninaamini yapo mafisadi ya kibeberu na nchi jirani yanayonufaika na wizi hapa nchini au nchi hii kuwa shamba la bibi.
Nawatakia sabato Njema
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam