KAMA NI HIVI NECTA ITUNGE MITIHANI TOFAUTI KULINGANA NA MAZINGIRA TOFAUTI

KAMA NI HIVI NECTA ITUNGE MITIHANI TOFAUTI KULINGANA NA MAZINGIRA TOFAUTI

Abraham Lincolnn

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2018
Posts
2,754
Reaction score
4,975
Kwa jinsi elimu yetu ilipofiki hakika Inasikitisha sana! Nadhani huyu katibu mkuu anapaswa kujitafakari sana.

Kama wanajua mazingira ya wanafunzi ni tofauti hilo ni kosa la nani? Wakati huo Syllabus na mtaala ni mmoja! Bado haitoshi mtihani ni mmoja Tanzania nzima, Kwa nini serikali isiboreshe shule zao ili kuwe na uwiano kimazingira?

Hizo shule kuboresha mazingira na kufaulu vizuri leo imekuwa nongwa kwao? Pamoja na kwamba kweli ni shule binafsi kibiashara sidhani kama hilo linahusiana as long as wanatoa elimu bora wanastahili sifa! na sio kufanywa kana Kwamba sio shule za Tanzania!,

Inashangaza sana kuona KM anadiriki kusema eti anawatangazia biashara! Seriously? Hiyo ni sawa na kusema IHEFU isishiriki ligi eti kwa kuwa Simba ina mazingira mazuri zaidi yao! wanafunzBasi ili kuwe na uwiano pia iwepo mitihani tofauti kulingana na mazingira!
 
Serikali inachekesha sana! Sasa kama wanaona wanatangaza biashara kwa shule binafsi zinazofanya vizuri zaidi ya shule zao kwa nini waliruhusu sera hiyo? Kama vipi wajitoe kuendesha shule, shule zake zote izibinafshishe ili wamiliki binafsi washindane wenyewe kwa wenyewe kutoa matokeo bora na jinsi ya kujenga miundombinu bora ya shule ikiwemo kuajiri walimu mahiri. Serikali ilianzisha ligi hiyo, sasa shule zake zinaangukia pua inaanza kuona aibu kutangaza shule bora za wengine kwa hoja dhaifu
 
Back
Top Bottom