MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Nimesikitishwa mno na habari niliyosoma kwenye ukurasa rasmi wa Askofu wa CHADEMA ndugu Emanuel Mwamakula kuhusu basi la wanawake wa CHADEMA mkoa wa Mwanza waliokuwa wakitoka Dar kupigwa mawe huko Singida. Hiki ni kitendo kiovu kinachopaswa kulaaniwa. Vijana wanaotuhumiwa kufanya hivyo wakamatwe na kufikishwa mahakamani.
Ninawasihi vijana kutoka familia maskini kujikita kupambana kuuondoa umaskini kwenye familia zao badala ya kujihusisha na matukio maovu. Hakuna mtoto wa kigogo wa CCM au upinzani utamkuta kwenye matukio kama haya. Yaani hata kukuta mtoto wa kigogo anatukana mtandaoni ni ngumu. Wazazi wao wanajua kabisa kiongozi unatakiwa uwe na busara na kujiepusha kabisa na jinai.
Tusubiri taarifa ya polisi kwa ufafanuzi zaidi.
www.facebook.com

Emmaus Bandekile Mwamakula
WANAWAKE WA BAWACHA WA MWANZA WAPOPOLEWA NA MAWE WAKIWA SINGIDA WAKITOKEA DAR KUELEKEA MWANZA. Gari ambayo imewabeba wanawake wa Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA) Mkoa wa Mwanza waliotoka...