mimi hata sishangai mambo ya kudai pesa wanaume wamekua "MARIOO". Nina rafiki yangu nae anaishi nchi ya jirani, mume yuko bongo na ni mfanyakazi pia. mke ana rotation ya 9 weeks kazini, 3 weeks likizo, utashangaa akija bongo, hizo 3 weeks, analipa madeni kibao yameachwa dukani na wapi sijui. halafu akiondoka after likizo, ni kwamba anaacha pesa za matumizi ya nyumbani kwa 9 weeks ambazo hatakua nchini, hii ni pamoja na luku, bill ya maji, mshahara wa maid, fuel ya gari ambalo mtumiaji ni mume, na upupu wote mnaojua wa ndani. ana mume huyu ambaye ni muajiriwa pia. nilisema mimi hadi shoga kaninunia kiaina, maana mie niliona ni u stupid na ushenzi fulani. huyo mwanaume kazi yake as a man ni kukuparamia tu au? ujinga mwingine tunaendekeza sisi wanawake, then baadaye kuacha inakua tatizo. wanaume wa siku hizi nao wakipata mteremko ni kwamba gear inawekwa free ateremke taratibu. hivyo huyu baba kudai pesa kwa mkewe, huenda mke alizoea hizo wakati wa malovi davi ya nguvu, sasa yakipungua unaanza kuona kero.
Ladies naomba tusiwazoeshe wanaume tabia ambazo hatutaweza kuendelea nazo. from day one, mwanaume ajue wajibu wake ndani ya nyumba, nikifanya mimi namsaidia tena haste haste. baba ndio kichwa cha nyumba na sio mama, yeye ndio akune kichwa tule, tuvae na tulale kwa raha.