#COVID19 Kama ni kweli waliochanja chanjo ya Corona hawazidi laki 4 hadi sasa basi Waziri wa Afya na Naibu wake wajiuzulu

Wewe umesha chanja au bado?
Kama bado nenda uongeze udadi tusogesogee wachanjaji.
 
Nilishangaa kuona nesi mtoa chanjo hajui kuchoma sindano !! Unapochoma sindano Intramuscular ( IM ) unavuta kwanza kuona kama kuna damu ,kama hakuna damu ndipo unasukuma dawa.sasa ile nilioiona kwa video mie sikuelewa.Tena nilijawa na hofu sana
 
Hapo ndiyo ujue shida ya upinzani.Lissu anapiga kelele tu juu ya katiba mpya lakini huoni akiwambia wafuasi wake waende vituoni kuchanja
 
Ni wazi watu hawaamini Corona kama ni ugonjwa hatari sana na wengine hawaamini kabisa uwepo wa Corona. Wangekua wanaamini watu wangegombaniana kama wanavyogombania Jersey za Simba na yanga.
 
Tatizo siasa imegubika zoezi zima la chanjo....
 
Unaionea wizara bure kuna vikwazo vingi vinavyosababishwa na wakina gwajima na polepole kurudisha nyuma jitihada za serikali.
 
chanjo sio lazima ni hiari, kazi ya waziri na naibu wake pamoja na serikali ni kuhamasisha watu wachanje...bila shaka wameshafanya hiyo kazi tayari...

Sioni tatizo kwao bali naliona tatizo kwa wanaohamasisha watu wasichanje, naliona tatizo lililosababishwa na awamu iliyopita kwa wananchi kubaki na mtazamo uleule..
 
Eti exposure!!! Ungejua wenzako tumeshaishi zaidi ya nchi 20 na bado hatuna mpango na chanjo ya majaribio. Sisi tutachanja mara baada ya chanjo za majaribio kukamilika mwaka 2023 na kupatikana chanjo halisi. Nyinyi mtaendelea na booster zenu!
 
K
Unaionea wizara bure kuna vikwazo vingi vinavyosababishwa na wakina gwajima na polepole kurudisha nyuma jitihada za serikali.
Kwa nini wewe usihamasishe watu wa chanjwe au wewe huna uwezo wa kuhamasisha kwa kuwa ni nyumbu au?
 
Wakishajiuzulu unapata faida gani ?
 
Sasa kama utawala huu ndio ulisema hivyo na watu wakakubali basi na utawala huu huu ndio sasa unasema chanjo ni salama wamejiridhisha kupitia wataalamu na wao wamekuwa mfano kwa kuanza kuchanja hizo chanjo mubashara kabisa, sasa tatizo liko wapi kwa watu kukubali wanachoelezwa sasa?

Tatizo sio kuwa mwanzo serikali ilisema chanjo ni mbaya au vp bali ni kwamba watanzania wanaishi maisha kana kwamba hakuna kitu kinachoitwa corona anaishi maisha yake kama kawaida bila ya hofu ya corona, sasa katika mazingira kama hayo anaanzaje kukimbilia chanjo kwa kuona ndio usalama wake hali ya kuwa haoni hatari ya kumfanya apate hiyo chanjo na ukizingata wapingaji wa chanjo wapo duniani kote.
 
Walichotakiwa kufanya ni kuondoa masalia ya waliokuwa nyuma kukwamisha mpango wa chanjo na wanafahamika ile comedy crew ya Waziri na Naibu wake walitakiwa kuondoshwa..

Haiwezekani watu wale wale walioshawishi kusema no hao hao ndio leo wataaminika kusema yes.. Dorothea na Godwin hawaaminiki simple as that!
 
Eti exposure!!! Ungejua wenzako tumeshaishi zaidi ya nchi 20 na bado hatuna mpango na chanjo ya majaribio. Sisi tutachanja mara baada ya chanjo za majaribio kukamilika mwaka 2023 na kupatikana chanjo halisi. Nyinyi mtaendelea na booster zenu!
Wala usiwe na shaka. Tuzidi kuomba Mungu uzima ili ifike hiyo 2023. Kama majaribio yatakamilika 2023 kwa sisi tuliochanjwa kufanyiwa majaribio basi najivunia kuwa mmoja wa watu waliojitolea bila woga ili wanadamu waweze kupambana na hao virus. Nikuulize swali: Chanjo zote zinazotumika sasa hivi (ambazo kuna uwezekano mkubwa na wewe umeshachanjwa) kama za tetunus, homa ya manjano, surua, ndui nk unajua kuwa kuna watu walikubali kufanyiwa majaribio na ndiyo wamewezesha binadamu kuyashinda hayo magonjwa ambayo yalikuwa janga kwa dunia yetu? Kuna kitu gani kingine kizuri kama kusaidia binadamu wenzako kuyashinda maradhi? Ningekuwa wewe wala nisingekuwa nawabeza ambao wamekubali kutumika kufanyiwa majaribio kama unavyoamini bali ningewaheshimu sana. Bila wao majaribio wangefanyiwa kina nani? Ina maana hata surua, polio, tetunus nk pengine ingekuwa imewauwa wazazi wako au wangu na sisi tusingekuwepo hapa leo. Au tulipokuwa wadogo tungeshapotezwa na hayo magonjwa.
 
Nani sasa anaaminika wakati kikubwa kilichobadilika hapo ni Samia kutoka kuwa Makamu wa rais na kuwa rais na kubadili msimamo waliyokuwa nao mwanzo kwa kuleta chanjo ila watu wote ndio walewale sasa ajabu mnamuona waziri wa afya tu, nani kasema kuwa ukibadili waziri wa afya ndio watu watakubali kuchanjwa ikiwa wamemuona hadi rais akichanjwa ila bado wamegoma?
 
Kwahiyo unadhani ni sahihi kumfukuza mtu kazi au kumyima huduma fulani kwa sababu kakataa kushiriki majaribio ya chanjo?
 
Walikosea sana walipoanzisha ligi na waliotumia hiari yao ya kutochanja...!! Unapoweka ligi wakati umesema kuchanja ni hiari, UNASABABISHA WENGI WAPATE HOFU. Ni kutokana na nguvu nyingi inayotumika kuwataka watu wachanje wakati hoja zao hazijibiwi wala kutolewa ufafanuzi wa kina
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…