Hamza Nsiha
JF-Expert Member
- Jul 25, 2022
- 221
- 197
Ndugu, wana JamiiForums leo ningependa kuwasogezea habari hii kuhusu project inayoendelea ya tajiri namba moja duniani ambaye pia ndiye mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Tesla, Mr. Elon Musk kuhusuiana na kuunganisha ubongo wa binadamu pamoja na kompyuta maarufu kama NEURALINK.
Picha: Elon Musk akielezea namna chip itakavyoweza kufanya kazi.
Muasisi huyo alisema kuwa, endapo project hii itafanikiwa basi ni dhahiri kuwa kutakuwa na urahisishwaji wa utumiaji wa kompyuta au vifaa vingine kama vile simu, Tv n.k kwani mtu ataweza kutumia vifaa hivyo kutumia ubongo wake tu pasipo kutumia viungo vyake vya mwili kama vile mikono.
Mfano, mtu ataweza kuchati pasipo kuandika kwa mikoni yake kwani kitu atakachokifikiria kukifanya pindi atakapotaka basi kitafanyika moja kwa moja katika kifaa chake.
Picha: jinsi mtu atakavyoweza kuwasiliana bila kutumia kifaa chochote.
Ni kweli pia kupitia taarifa aliyotoa bilionea huyo hivi karibuni kuwa mpaka sasa project inaendea kukamilika kwani imeshafanyiwa majaribio kwa baadhi ya viumbe wenye ukaribu na binadamu ambao ni nyani na ilionekana kufanikiwa kwa asilimia nyingi.
Picha: nyani akitumia kifaa maalumu(game pad) kucheza gemu.
Picha: ikionesha jinsi nyani alivyoendelea kucheza gemu mara baada ya kifaa(game pad) kuondolewa.
Lengo la kukusogezea habari hii ni kuamsha mjadala kuhusu nini madhara ya teknolojia hii kwa binadamu?
Je! Mtazamo wa dini upoje katika project hii?
Je! Endapo project hii itafanikiwa kukufikia unaweza kuwa tayari kuwekewa hio chip kwa ajili ya NEURALINK?
karibuni kwa mjadala!