Kama ni suala la kuongeza tija, Serikali, Bunge, Mahakama vibinafsishwe

Kama ni suala la kuongeza tija, Serikali, Bunge, Mahakama vibinafsishwe

Pascal Ndege

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2012
Posts
2,977
Reaction score
1,897
Kama Serikali imeamua kubinfsisha Bandari kuongeza ufanisi.

Mimi mawazo yangu tuanze kwanza kubinfsisha Serikali. Serikali haina ufanisi kusimamia mambo mengi sana. Kususua kwa miundombinu mbali mbali, Kususua kukusanya mapato na upotevu mkubwa wa mapato. Kususua kwa huduma mbali mbali za kijamii mawizarani na Taasisi mbali mbali.

Cha pili ni kubinafsisha ni Bunge
Bunge limepitisha sheria nyingi zisizo na Tija kwa jamii kabisa. Kufikia zingine zinarudishwa tena kufanyiwa marekebisho. Matumizi mabaya ya madaraka kuingilia uhuru wa watu kukosoa Bunge. Bunge Halina ufanisi kabisa.

Cha Tatu ni mahakama
Mahakama imekuwa na ikichelewasha kesi pia kuingiliwa maamuzi na vyombo vingine kama DPP na nk.

Mimi maoni yangu kama ni swala la ufanisi basi kwanza kabisa serikali ianze kubinfsisha na baraza lake lote la Mawaziri. Tulete serikali ya Dubai itujengee miundombinu kwa haraka kama Dubai. Umeme wa uhakika na Usafirishaji. Serikali ya Dubai iangalie upya mikataba ya Madini na Gas. Iwavutie wawekezaji wajenge mabawa makubwa ya umeme. Pia watupe viza watanzania wote tuhamie Dubai.

Nimewaza tu Maana nimevulugwa kama wananchi wengine sielewi. Mnisamehe tu. Haki ya kuwaza upuuzii wa watu wengine ni haki ya kila mtu. Nawewe waaazie tofauti.
 
Back
Top Bottom