ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 21,643
- 51,642
Achana na hizi kauli kwamba usishike simu ya mumeo/mkeo ikiwa unataka kulinda penzi..hizo ni kauli za watu malaya au wasio waaminifu kwenye mapenzi yao.kimsimgi kama mnapendana na mwenzako inatakiwa hata akusaidie kuchart kwenye ma group funny kama ya classmate..yaani kama umechoka na unaona inahitajika uonekane uko active sio vibaya kumpa simu mwenzi wako aendelee na stori.mimi mke wangu kashajua ninapenda jamiiforum na yeye analipenda jukwaa la MMU ila sio kuchangia yeye anapenda tu kusoma comment zenu.sijaona sababu bado ya kuficha sijawahi kumsaliti hata siku moja na labda ikija kutokea nikalazimika siwezi kutengeneza mazingira ya huyo nyumba ndogo anitafute tafute kwenye simu kiasi nikawa na wasiwasi na hofu kwenye simu mbele ya mwenzangu.