Kama ni wewe utafanya nini!!?

Kama ni wewe utafanya nini!!?

mbwana semsimbazi

Senior Member
Joined
Sep 5, 2013
Posts
196
Reaction score
202
*KAMA NI WEWE UTAFANYA NINI?*

Mke alimuaga mume wake anaenda kumsalimia mam yake mgonjwa kijijini, akaondoka ijumaa na kurudi jumatatu huku akiwa na matunda kibao pamoja na vyakula vingine toka huko kijijini akisema ni mama amenipa kwa ajili yako mume wangu na watoto.

Mume akamuuliza kwa upoooole...

Mama anaendeleaje!

Mke akajibu kuwa amempeleka hospitali ila anaendelea vyema.

Mke aliongezea kwamba;

Mama yake amemsisitiza amtembelee tena baada ya siku chache akae huko naye wiki.

Mke akaendelea kusema; nina hofu na afya ya Mama. Aliyasema hayo kwa uchungu huku machozi yanamtoka.

Mume akamjibu kwa huruma atapona mpenzi usijali.

Mume akamwambia mke wake kwa hekima:

..ingiza vitu ulivyoleta jikoni.

Mke ile anaingia jikoni akamkuta mama yake mzazi aliedai kaenda kumsalimia kijijini akiandaa chakula jikoni.

Kumbe mama yake alikuja kumtembelea pale tangu ijumaa yeye alivyoondoka.

Mke akabaki ameduwaa mlangoni mwa jiko asijue apeleke vitu jikoni au arudi sebuleni kwa mume wake.

*Je afanyeje?*
 
Atakuwa kifuniko cha asali kimefunuliwa halafu atakuwa amejifunza tena bila kumwambia kitu.
 
Namwambia sio mama huyo ni mama mdogo/mkubwa[emoji23]...

Au mama wa shule....
 
Kwanza namwambia aende chooni, maana nahisi haja zote zitakuwa zinagongana hapo
 
Back
Top Bottom