Kama nimejenga nyumba kwenye kiwanja si changu, kunivunjia nyumba au kuniambia ninunue hicho kiwanja kipi bora?

Hapo BUSARA ni wewe uhamishe nyumba Yako, Kisha umwachie kiwanja chake.
Mabeberu inabidi yaingie chimbo yaje na Teknolojia ya kujenga nyumba zinazohamishika ili waweze kutuokoa sisi tuliolala.
 
Busara ni kutokujenga kwenye eneo lisilo la kwako.....
Kuna factors nyingi zinaweza sababisha ukajikuta umejenga kwwnye kiwanja ambacho siyo chako.siyo lazima uwe tapeli.lakini pia kwa mfano mtu alipata building permity ,sasa unatoaje building permity bila kujiridhisha kama hati miliki ya kiwanja ni cha mwombaji.tunaitaji mfumo thabiti kuzuia usumbufu wa namna hii
 
Bora ni wewe kuuziwa kiwanja au pia ukubali kuuza nyumba hiyo kwa mwenye kiwanja kwa bei yoyote atakayoweza.😁😁😁😁
 
Bora ni wewe kuuziwa kiwanja au pia ukubali kuuza nyumba hiyo kwa mwenye kiwanja kwa bei yoyote atakayoweza.😁😁😁😁
Sema wengi hao wababe huwa wanajisahau kuwa serikali hubadilika na matapeli wanaokuwa kwenye system wanaoishirkiana nao kuna wakati hufika na wao mtandao hupotea kwa kustaafu ,kubadilishwa vituo kuja raisi mpyya ,serikali mpya uongozi mpya wenye misimamo kuanzia serikalini ,mahakamani ,wizara ya ardhi nk
.utapeli wa viwanja haulipi moto ukiwaka tapeli atakumbuka hadi bibi mzaa bibi aliyekufa akiona ghorofa linashushwa kama kupiga teke mdoli
 
Mara nyingi watu migogoro ya ardhi hujenga uhasama kutokana na watu kutunishiana misuli......mpaka kufikia mwisho watu hukosa busara na kuamua kukomoana.........
 
Nijuavyo,

Nyumba unaweza kuhamisha ukipewa muda, na uharibifu au HASARA ni ndogo sana kuliko kubomoa.
Tuelekeze bloangu sisi vibopa, wezi,mafisadi,wavamizi wa viwanja vilivyopo kwenye lokesheni nzuri

Teknolojia gani inatumika kuhamisha jengo hapa?

Kwenye miti hata ukiwa mkubwa kiasi gani nilisikia inawezekana kuuhamisha,sijajui huku kwenye majengo inafanyikaje fanyikaje.
 
Bora ni kujenga nyumba kwenye kiwanja chako.

Kwa nini ujenge nyumba kwenye kiwanja kisicho chako?

Utategemeaje kitu bora kwa kupitia njia isiyo bora?
 
Bei ya kiwanja huwa haipangwi na watathimini.

Bei ya kiwanja huwa inapangwa na muuzaji wa kiwanja.

Hata akisema anauza kiwanja chake kwa trilioni moja. Hakuna sheria ya kumkataza. Ni uamuzi wake.

Kama unataka akuuzie mpe dau kubwa analotaka. Achana na mambo ya watathimini
 
Kama ulikusudia kufanya dhuruma basi sahihi ni kupokonya nyumba apewe uliye kusudia kumdhurumu
 
hiyo unayoiita busara ndiyo ilitumika sana kupoka wenye uwezo mdogo viwanja au nyumba zao zilizoko kwenye 'prime areas' kwa kisingizio cha kulipa fidia isiyokidhi.
 
Kuuza ni willingness ya mmiliki wa kiwanja na si busara yako
 
Acha Janja Janja akajenge kwake. Kiwanja siuzi.
 
Ukibomolew ni kwasababu ulimuon mwenye kiwanja unamuweza ,atakufanya nini,ashitaki popote ,kiufupi anaye bomolewa ni kiburi jeuri apambane na hali yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…