Kama nimejenga nyumba kwenye kiwanja si changu, kunivunjia nyumba au kuniambia ninunue hicho kiwanja kipi bora?

Kama nimejenga nyumba kwenye kiwanja si changu, kunivunjia nyumba au kuniambia ninunue hicho kiwanja kipi bora?

Navunja nyumba halafu nakuuzia kiwanja.
Halafu kiuze bei yake piga hivi bei ya kiwanja sokoni kwa sasa halafu jumlisha na bei ya jengo lililovunjwa hiyo jumla ya hiyo hesabu utakayopata ndio iwe bei ya kumuuzia minimum Sababu kakuletea usumbufu kiwanja chako hiyo ndio iwe bei ya kumuuzia
 
Unavamiaje kiwanja cha watu? Kwanini hukukinunua kwanza? Kuna mambo mengine ni ubabe wa kijinga hakuna haja ya busara. Unless useme uliuziwa kwa njia za kitapeli hukujua.
 
Kwenye haki ya mtu huwa hakuna kutumia Busara kama mwenye kiwanja amekomaa anataka kiwanja chake. Ukiona mpaka nyumba imebomolewa ujue asie na busara ni yule aliejenga kwenye kiwanja cha mwenzake tena mara nyingi Kunakuwa na hatua kibao zimechukuliwa hata kabla ya kiwanja kujengwa lakini jamaa anakomaa (tena ukute alikuwa anapiga mkwara kabisa unajua Mimi ni nani achilia mbali wengi wao huwa na hati kabisa ambazo Kuna namna wamefanya mpaka wakapewa hati, ukilalamika Kwa kiongozi akienda ardhi anakuta mlalamikiwa ana hati kabisa na ukikutana na anaefuatilia document Kwa document ndo hapo nyumba inashushwa)

Piga hesabu wewe sasa una kiwanja Masaki either cha urithi alafu jamaa anajenga na umepambania hicho kiwanja tangu mwaka 2000 bila mafanikio alafu Leo haki imepatikana Kwa mbinde alafu mtu aje aseme mtumie busara maana jamaa alitumia fedha lakini pia serikali itapoteza mapato bila kujali huyu mwenye kiwanja amesota muda mrefu kutafuta haki.

Hiyo issue huwa inatumika Kwa watu waliojenga Kwa bahati mbaya yaani kiwanja kimeuzwa Kwa watu wawili hivyo mamlaka huwaita wote na kuwasuluhisha na kushauri halmashauri husika kutoa kiwanja kingine Kwa mlalamikaji ambacho chenye hadhi sawa na kile cha awali na lazima akubali (sio kumpa kiwanja chochote tu)
 
hahahaaaaa.kazi ipo kwa kweli.

serikaliinatakiwa ipime viwanja vyote vya makazi na kuviweka kwenye satelite na iwepo sheria kwamba unapotaka kukunua kiwanja ,nenda ofisi za ardhi uapte maelekezo .
Hawa jamaa hata viwanja vilivyopimwa wanapitia mkuu hasa kama kimekaa wazi muda mrefu, mfano kiwanja cha maremu Jaji.

Rutihinda walitumia technique ya kumwabdikia barua afike ofisini na document zake ili hali ni marehemu alafu kwenye document inaonyesha hakuitikia wito na hapo mapekechee ndo yanafanyika either kiwanja kinakatwa katikati alafu anqpewa kibopa mwingine ambae anakuwa anqpewa jeuri na watu wa ardhi
 
Hawa jamaa hata viwanja vilivyopimwa wanapitia mkuu hasa kama kimekaa wazi muda mrefu, mfano kiwanja cha maremu Jaji. Rutihinda walitumia technique ya kumwabdikia barua afike ofisini na document zake ili hali ni marehemu alafu kwenye document inaonyesha hakuitikia wito na hapo mapekechee ndo yanafanyika either kiwanja kinakatwa katikati alafu anqpewa kibopa mwingine ambae anakuwa anqpewa jeuri na watu wa ardhi
Duh
 
Yaani hawana huruma hata na Jaji jamani mashetani hao.

Mahakama ziwakomalie hawa matapeli wa viwanja hata wao majaji waweza dhulumiwa pia hawaogopi hata majaji hao sio watu wema hao

Inabidi kila kona na kila mhimili uwavallie njuga hadi kieleweke watu waogope kupora viwanja vya watu
 
wakati mwingine busara huwa inaitajika unapotoa maamzi. mediation inaweza kutumika .kwani kuna faida gani unapovunja nyumba ya mtu hata kama kiwanja si chake? wewe mwambie kiwanja si chake then akikubari mwambia nunua kiwanja hiki.ziko taasisi zenye kuthaminisha viwanja na majumba .hivyo mhusika au mtuhumiwa ataweza kununua kiwanja hicho au nyumba hiyo kwa thamani halali iliyopangwa na wathaminishaji.unabomoa ghorofa ya mabilioni ili upate faida gani? kwanza serikali inakosa mapato kupitia ubomoaji huo kwa sababu let us say ni nyumba ya kibiashara pale watu walikuwa wanaingiza hela na serikali inapata kodi .sasa nyumba umevunja hapo serikali inapata nini
Muuzie yeye
 
We bwege alikutuma nani kujenga kwenje kiwanja cha mtu? Huwezi kumpangia na kumlazimisha mtu namna ya kutumia mali yake. Ukifanya hivyo wenye pesa watavamia viwanja vya watu vilivyo kwenye site nzuri wakitegemea hiyo unaita mediation. Huo ni sawa na ubakaji
 
Kwetu Sisi wanasiasa wamepewa mamlaka kuliko hata Sheria ya nchi. Hali hii huwa inanifanya kuungana na Chadema kudai katiba mpya kimya kimya.
 
Back
Top Bottom