Hakuna lolote. Kuna amri inakataza kuzini na kutotamani Mali ya mtu mungine. Lakini hizo amri ndio zinaongoza kuvunjwa.Ukizosoma amri kumi za biblia amri nne zinamuhusu mungu, amri sita zilizobaki ndio zinaratibu mahusiano na maisha ya binadamu kati yao.
Fikiria kama amri nne za mungu zinazomuhusu yeye zingeunganishwa kuwa amri moja kisha zingewekwa amri tatu zinazosema
1. Usifanye ubaguzi wa aina yoyote uwe wa rangi, kabila, dini au nchi.
2. Usishiriki biashara ya utumwa
3. Usifanye unyonyaji wa kiuchumi
Fikiria jinsi maisha ya binadamu yangekuwa bora zaidi kwa kuwepo amri hizo katika Biblia.
Hizi amri tatu ndizo zilihitajika zaidi kwa sababu ubaguzi, utumwa na unyonyaji ni mambo ambayo jamii na watu wanaotenda ni wenye nguvu, wababe na ngumu wao kuathiriwa kwa haya maovu matatu.Hata bila kuwepo kwa amri, ule utashi tu na nuture ya binadamu na viumbe wengine ilikuwa inakidhi utaratibu wa maisha.
Kwa mfano amri ya 7. Usiibe. bila hata kuambiwa usiibe. Kwa hali ya kawaida tu kuchukua mali ambayo sio yako si sawa. Mimi nifuge kuku wangu wewe uje uvizie uibe!! Sio sawa.
Na ile usitamani mke wa mtu. Kwa hali ya kawaida kabisa hilo jambo halifai mbele ya jamiii. Madhara yake ni mengi. Kama kupigwa, kuuwawa, na hata kufungwa jela.
1. Unaweza kusababisha ndoa ya mtu kuvunjika na kusabaisha madhara, shida, na tabu kwenye familia.
2. Ukifumaniwa unaweza hata kuuliwa, au kupelekewa moto.
Mambo mengine ni nature tu. Haitaji kuambiwa.