Wakuu,
Kama ningekuwa JK pamoja na mambo mengine ningefanya yafuatayo:
1. Ningejenga Multi-purpose Science Laboratories kila wilaya.
2. Ningeongea na vituo vyote vya televisheni hapa nchini ili kila siku kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa 6 usiku, kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na ofisi ya waziri Mkuu, wawe na vipindi vya elimu tu vikilenga zaidi wanafunzi wetu katika ngazi mbalimbali za elimu na Watanzania kwa ujumla wetu kwa ajili ya kutupatia ujuzi katika stadi mbalimbali za maisha.
3. Ningehakikisha kila mwajeshi hapa nchini anakuwa mtaalam mzuri sana wa ICT na Computer kabla ya mwisho wa mwaka 2015.
4. Ningelikabidhi rasmi jeshi letu kazi ya kuhakikisha kuwa barabara zetu zote zinapitika mwaka mzima.
5. Ningefunga VIDEO CONFERENCING FACILITIES katika kila wilaya na tarafa hapa nchini kabla ya mwisho wa mwaka 2013.
6. Ningejenga National Science Retreat and Research Centre pale Butiama kwa angalau gharama ya shilingi bilioni 20.
7. Ningeibadilisha Pemba na kuifanya kuwa kitovu za maendeleo ya ICT hapa nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla ndani ya miaka mitano. Hapa ningeanza na Pemba ICT University.
8. Ningewashawishi viongozi wa Afrika Mashariki kuanzisha kwa pamoja shule za Sayansi za Afrika Mashariki lengo likiwa ni kujenga angalau shule 50 za namna hiyo kila mwaka kwa mgawanyo wa shule 10 kila mwaka kwa kila nchi.
9. Ningependekeza ndani ya Chuo Kikuu cha Dodoma kujengwe EAST AFRICA PhD CENTRE na pia kuanzisha EAST AFRICA PHD SCHOLARSHIP FUND ikiwa na uwezo wa kufadhili angalau Wana Afrika Mashariki wasiopungua 5000 kwa wakati mmoja. Asilimia angalau 70 iwe kwa ajili ya PhD za Sayansi na Teknolojia.
10. Ningefuta ada na michango mingine yote kwa shule za sekondari za Serikali hapa nchini.
11. Ningekopa toka mifuko yetu ya hifadhi ya jamii angalau shilingi bilioni 200 kila mwaka na kujenga High Schools za kisasa angalau 200 kila mwaka na nyingi zikiwa kwa ajili ya combinations za PCM na PCB.
Nawasilisha.