Deus Michael Ndololo
Member
- Jul 26, 2017
- 25
- 48
Ndugu zangu wa-Tanzania mambo vipi? Mko poa? Kama jibu ni ndio basi fresh na kama sio basi hakuna tabu, ila ninamachache ya kuzungumza na ninyi then niende zangu.
Nisikilize sasa,
Hakuna kipindi kigumu wanachopitia watanzania kama kipindi hiki na wengine wameanza kwenda mbali zaidi na kutafuta watu wa kuwatupia lawama, wengine wakimtupia lawama Mh. Mwigulu Nchemba kwa sababu ya tozo, na wakidai kuwa yeye ndio sababu ya kupoyeza amani za watu. Ni kweli kuna "tozo" zimeongezeka lakini niwathibitishie kuwa hakuna kitu ambacho kitadumi milele lakini pia hata kama kitadumu basi njia ya kulitatua tatizo hilo sio kulalamika, njia sahihi ni kutokufuatilia kabisa vilinge, mikusanyiko ambayo watu wanakutana kujadili mambo hayo, badala yake hiyo nguvu inayotumia kulaumu watu na viongozi ingehamishiwa katika kazi hakuna mtu ambaye angeendelea kulalamika.
NINI UFANYE...
Hiki ni kipindi kigumu sana kwa watanzania, hasa watu wanaojikita zaidi katika kufuatilia habari, imagine, unataka kupumzika, mara unasikia Yanga na Simba wako hivi, mara Mandoga kafanya hiki, ujatulia mara tozo ziko juu, ujatulia mara, mishahara haijaongezeka, mwisho wa siku hali hii inakupelekea na wewe kuingia katika kikundi cha walalamishi na hapo ndipo unapoanza kujiua zaidi.
Jambo la Msingi,
Unapaswa kuwaza zaidi ya kila changamoto inayokutokea, kama fedha imekuwa kikwazo, unapaswa kuwaza mara kumi zaidi ya serikari namna ya kujitatulia. Kama tozo, anza kujikata wewe mwenyewe tozo na kujiwekea akiba kwako, i mean ujilazimishe hata kama hupendi, jifanye wewe ndio Mwigulu Nchemba wa maisha yako, usijipe sababu za kijinga jitoze mwenyewe na jiwekee akiba na ikitoke wenzako wanalalamika wewe uko mbali mno. Ujinga mkuu ni kuanza kulalamika hovyo unapoona mambo hayaendi vizuri, sasa sijui unadhani nani atakuja kukutatulia matatizo yako? Hakuna mtu wa kuja kukusaidia usipoamua kithabiti kuwa Mwigulu Nchemba wa maisha yako. Sijui naelewek vile? Eeeh, haya ngoja nikomee hapa kama hujaelewa rudia kusoma, kama umedaka japo machache nipe tano!! Mwigulu Nchemba wa Maisha yako ni Wewe, anza kujitoza tozo katika maisha yako na iweke katika akiba zako, hutajutia.
Thanks All. - Deus Michael Ndololo