Kama nyumba ya ibada imenikuta ninapoishi na ibada zao zinasababisha kelele kubwa, ninaweza kuiomba Mahakama kuwaondoa?

Kama nyumba ya ibada imenikuta ninapoishi na ibada zao zinasababisha kelele kubwa, ninaweza kuiomba Mahakama kuwaondoa?

Superbug

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
13,864
Reaction score
35,079
Nadhani kichwa changu kinajieleza.

Mfano msikiti au kanisa wamenikuta mahali ninapoishi na ibada zao mimi kwangu zinanikosesha amani, je naweza kuiomba Mahakama iwaondoe wanipishe? Au ninunue eneo lao?
 
Angalia tu wasije kukuhamisha wewe kwa kununua nyumba yako.
 
Hii kitu huwa inanikera kweli, alafu watu wa mipangomiji huwa wanasema kuna maeneo ya Nyumba za ibada, makazi nk lakn in reality siyo kweli. Mm nikiona kiwanja kiko karibu na msikiti au kanisa(hasa yanayojiita ya kiroho, sijui hili jina la kiroho linatokana na nini), sikinunui labda bei ishushwe sana alafu naweka baa na Kitimoto full! Sitakagi ujinga
 
Vizuri tu mbona hilo halina shida

Kuna kitu kinaitwa "mipaka", dini ni mimani na katiba ya Tanzania imetoa idhini ya kila mwananchi kuamini atakavyo ilimradi asivuruge imani ya mwingine au kuingilia utaratibu wa mwingine.

Hawatakiwi kupiga makelele na mispika yao kwenye vibaraza vya watu maana hata masela wa vijiweni hawajawahi kwenda kunyongea ganja madhabahuni hiyo ni kwasababu ya kuheshimu itifaki.

Kama ni wakristo wakipiga makelele kwenye kibaraza chako wakaushie halafu sikilizia mpaka siku ya xmas nenda church na wahuni kisha katimize lile andiko la jino kwa jino.
 
Jamaa uandishi wako ni kichekesho halafu unajipa no sweat eti 'kichwa chako kinajieleza'[emoji38]
 
Watu wasiopenda kusikia habari za uwepo wa Mungu ndio pekee wanaokerwa na sauti zitokazo kwenye nyumba za ibada.
 
Hiyo hua inakera sana, kuna nyumba nilipanga karibu na kanisa la walokole asee kila ijumaa walikua na mkesha kelele mtaa mzima, cha ajabu ukichungulia ndani hata watu 20 hawafiki!
 
Muombe mungu wako apitishe tetemeko eneo hilo lakini liharibu kanisa/msikiti tuu na majengo mengine yabaki kama yalivyo.
 
Back
Top Bottom