Kama rais Magufuli anaamini kwenye ndondo Cup, Kombe la Dunia Tanzania itabaki ndoto

Kama rais Magufuli anaamini kwenye ndondo Cup, Kombe la Dunia Tanzania itabaki ndoto

tajirijasiri

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
2,863
Reaction score
3,854
Rais kasikika leo akijitapa kushabikia ndondo Cup kuliko ligi kuu kwa kigezo cha wang'oa Viti, basi Tanzania kushiriki kombe la Dunia itakuwa ndoto.

Haiwezakani Kiongozi Mkuu ukalialia matatizo badala ya kutoa mwongozo wa nini cha kufanya.
 
lakn si ameongelea tu kwamba bora kuenda kuangalia ndondo cup.mm sijaona kosa hapo kiongozi
 
Nadhani nia ilikuwa kuonyesha kwamba anajua kitu kinaendelea kwenye burudani na michezo. Anajua habari za fiesta na ndondo cup.
 
Nadhani nia ilikuwa kuonyesha kwamba anajua kitu kinaendelea kwenye burudani na michezo. Anajua habari za fiesta na ndondo cup.
Sasa zaidi ya vijembe kwa Wang'oa Viti, katoa uelekeo gani wa soka la Tanzania?
 
Rais kasikika leo akijitapa kushabikia ndondo Cup kuliko ligi kuu kwa kigezo cha wang'oa Viti, basi Tanzania kushiriki kombe la Dunia itakuwa ndoto.

Haiwezakani Kiongozi Mkuu ukalialia matatizo badala ya kutoa mwongozo wa nini cha kufanya.
watu wengine akili zenu sijui zikoje aisee, ila kuna kamsemo mtukufu rais alikasema "kuna watu hata ukitembea kwenye maji watasema unawatimulia vumbi" ndio kama wewe.
 
Ukikaa na kumuamini yule jamaa lazima utafeli chief nakuhakikishia mwenzio alikua anatania na wala hakumaanisha maana hajui lolote kuhusu michezo na ukimuuliza sasa ivi pale atakushangaa kama hajaongea yeye kama hatukusonga mbele kipindi cha JK basi hatuwezi kufika popote angalau yeye alikomaa na soka.
 
Sasa zaidi ya vijembe kwa Wang'oa Viti, katoa uelekeo gani wa soka la Tanzania?
Kuna mtu aliyemuuliza kuhusu muelekeo wa soka la Tanzania leo? Unataka atoe mulekeo kwani alikuwa anatoa hotuba ya michezo leo. Ungewalaumu waandishi waliotakiwa kuuliza maswali wakashindwa kumuuliza kuhusu soka mpaka akaingizia mwenyewe maswala ya fiesta na ndondo.
 
Siasa za wanasiasa ni tofauti na siasa za wafuasi wa siasa
 
Rais ameonyesha ni mtu wa kukomoa na kususa susa.
 
Vipi kama tukijenga taswira kwamba Rais anafatilia Ndondo Cup kama ndio chimbuko la vipaji vya wachezaji wetu wengi? Na Pengine anataka kuanza kuboresha mfumo wa mchezo wa soka toka ngazi ya chini??
Kimekuwa ni kilio cha muda mrefu kuwa tuwekeze kwa vijana wenye umri wa chini katika michezo kama kweli tunataka kufanikiwa huko. Wachezaji ambao hawajacheza ndondo duniani ni wa kuhesabu na wapo watu wengi wanafanya shughuli nyengine lakini katika ujana wao wamecheza Ndondo
 
Back
Top Bottom