Kama Rais Mama Samia anahitaji kukuunganisha Taifa turudi kwenye misingi ya Utu, basi Mwigulu Nchemba hafai kuwa VP wala PM

Kama Rais Mama Samia anahitaji kukuunganisha Taifa turudi kwenye misingi ya Utu, basi Mwigulu Nchemba hafai kuwa VP wala PM

Prof Koboko

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2020
Posts
350
Reaction score
2,550
Wasalaam wanajukwaa!

Siku wakati Rais mpya Mama Samia Suluhu anaapishwa kua Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania alisisitiza turudi kuungana kua taifa moja na tuzidi kupenda tusahau yaliyopita na tugange yajayo.

Ndugu yetu Mwigulu Nchemba naye jina lake linatajwa kiasi flani katika wale wanaoweza kupendekezwa kushika nafasi za uwaziri mkuu kama Majaliwa atateuliwa kua Makamu wa Rais au yeye ateuliwe kua makamu moja kwa moja.

Sina chuki yeyote na kijana huyu lakini bado haitoshi katika nafasi kabisa kutokana na mambo yake tangu akiwa waziri wa mambo ya ndani hali iliyopelekea Rais Magufuli kumtumbua na kisha kumrudisha baadae baada ya kuomba radhi.

Ndugu yetu amesemwa sana hata ndani ya chama kutowasikiliza walio chini yake na hata wakubwa zake, siku zote anafanya mambo kwa jazba, kejeli, dharau na kutokujali pia. Ni mtu anayependa asifiwe tu wala hapendi kuambiwa ukweli.

Ndugu yetu ana kauli zisizoweza kuunganisha jamii hata pale ambapo kuna taharuki, yeye anatoa majibu unaweza kufikiri ndio kiongozi wa nchi. Huyu akipewa nafasi anaweza kufanya anachokijua bila kujali nafasi ya aliye juu yake, ni JPM tu ndio alikua anamuogopa sana.

Mwigulu si ndio juzi juzi tu alitoa maagizo kwa polisi kuwakamata wananchi wote waliohoji alipo mpendwa wetu Rais JPM? Anaelewa kua watu wanasita mahabusu kwa sababu yake yeye? Anafikiri Simbachawene hana sauti ya kutoa maagizo hayo? Yeye kilichomsukuma kutoa maagizo hayo ni kitu gani?

Si ndio huyu Mwigulu Tundu Lissu anasema kwamba alikua alimweleza kwa siri kua hakubaliani na utandaji wa JPM Mara baada ya kutumbuliwa uwaziri wa mambo ya ndani? Maana yake hata kesho atamsema vibaya Rais Samia Suluhu.

Kama kweli tunahitaji kulinganisha taifa, tunahitaji watu wenye busara,utu na hekima. Tunahitaji watu wataksoheshimu katiba ya nchi na ambao wana uwezo wa kulia pamoja na jamii na kuipenda nchi yao.

Tusiume maneno kama mtu una shida mahali lazima uambiwe, ni chaguo lako kukubali kushauriwa na kubadilika au uchukie zaidi.
 
Back
Top Bottom