Kama Rais Samia alipongezwa sana shilingi kupanda thamani dhidi ya dola, hatupaswi kumkosoa sasa shilingi inapoporomoka dhidi ya dola?

Kama Rais Samia alipongezwa sana shilingi kupanda thamani dhidi ya dola, hatupaswi kumkosoa sasa shilingi inapoporomoka dhidi ya dola?

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
15,415
Reaction score
29,584
Wale wau ambao kila kitu kizuri kikitokea wanaishia kusema ni kwa sababu Mama Samia anaupiga mwingi, kuna wakati hizo sifa kwa raisi zitawatokea puani na kumuumbua sana raisi wetu.

Juzi hapa thamani ya shilingi dhidi ya dola ilipanda ghafla, toka Shs 2700 kwa dola hadi Shs 2200 kwa dola. Watu wakaishia kumpongeza sana Raisi Samia, kwamba yeye ndio amefanikisha hilo katika utendaji wake, apewe maua yake!

Wenye akili tulikaa kimya, tukijua mabadiliko ya thamani ya fedha yanaweza kuwa na sababu nyingi sana. Leo KLM au Air France wanaweza kusema hawaji tena Zanzibar shilingi ikashuka thamani. Au Trump atashinda uchaguzi USA na dola ikashuka thamani, nk. Geopolitics ni factor kubwa katika mambo ya exchange rates. Kwa kweli nilitarajia Raisi Samia angesema jamani sio mimi, lakini akakusha kupokea sifa na pongezi!

Sasa hivi thamani ya shilingi inaanza kushuka kwa kasi. Hadi sasa imeshuka utoka Shs 2200 hadi 2400 kwa dola.

Sasa nawauliza wale wote mliokuwa mstari wa mbele kumpongeza Raisi Samia thamani ya dola iliposhuka. Raisi Samia amefanya nini kutuharibia thamani ya shilingi yetu? Tunahitaji kumkosoa kwa hilo, sivyo?
 
Ni wazi kuporomoka kwa shilingi kunahitaji uchunguzi wa kindani sana hata wa tume huru. Kuna kila dalili kwamba kuna watu walijua wanachofanya, na matokeo yatkuwa nini
 
mpigeni spana tu kwani anajua nini cha zaidi ya kugawa watanganyika tu na kutujazia mizanzibari kila kona mimi sijawahi kumkubali hangaya katika jambo lolote lile angalia dar es salaam watu wanavyohangaika na usafiri mwendokasi imekufa kifo kitakatifu na yeye yupo tu, kana kwamba haoni angalia maisha ya walalahoi yabavyozidi kuwa maumu, then kinatokea kikaragosi hukoeti kukosoa uhaini kisatu ana pokea vijihela uchwara vya kula wenzie hawana hata mia shenzi kabisa,
 
Back
Top Bottom