Pre GE2025 Kama Rais Samia ameufanyia hivi mti mbichi; Je, itakuwaje kwako Mti Mkavu?

Pre GE2025 Kama Rais Samia ameufanyia hivi mti mbichi; Je, itakuwaje kwako Mti Mkavu?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Special Seat

Senior Member
Joined
Jul 21, 2024
Posts
169
Reaction score
301
IMG-20240723-WA0154.jpg
Ushauri wa Bure kwa Waajiriwa wote wa Serikali hasa wale wa Vimemo vya Uteuzi kutoka Kurugenzi ya IKULU kuweni makini zaidi pengine kuliko awamu yoyote ya Uteuzi wenu.

Huenda Rais Dkt Samia Suluhu amegundua wanaomuagusha na kumfelisha kwa kumuibia na kumfisadi zaidi ni watu wake wa karibu (miti mibichi )

Wakati huu tumeshuhudia Mama Samia akitengua vigogo wa karibu yake kabisa ambao wengi wao walifanya sherehe baada ya Kifo Cha Hayati Dkt John John Pombe Joseph Magufuli na Uapisho wake.

Rai yangu kwa mliobaki hasa mliokuwa mnamchezea mama kwa mizaha na kejeli kwenye idara zenu ongezeni umakini kwani Mama kwa sasa ni kama mbogo aliyejeruhiwa na simba

Mbaya zaidi ninyi msio na ukaribu kabisa na Mama Samia mjiulize kama Mama huyu ameutendea mti mbichi ( January na Nape ) namna hii, itakuwaje kwenu kama mtafanya kazi kwa mazoea hasa wizi na ufisadi?

#Mama hakamatiki na sasa kafungua injini mpya stay tuned
 
Wake wa mungu kaamua ugomvi,na bahari imetulia nao wamefikiwa? Bado mmoja,hakuna kauli zilinikeraga Kama hizo,yaani kwa kariba ya viongozi wa CCM niliwakubali sana Nyerere na magufuli,kwa uraisi ,kariba ya uwaziri niliwakubali sokoine na mrema, Sasa kauli za mawaziri wa uma kukejeri umauti wa magufuli,iliniuma mno,binafsi hata Kama kura yangu isingeoongeza chochote,basi niliamua kutoipigia kura CCM na hata upinzani nisingepigia,maana mbowe na zito niliwasikia wakisema tukazikwe nae,Ila Sasa labda huyu mama anatafuta kura zetu tu ,lakini nimefurahishwa na kumtumbua nape na makamba, naanza kutafakari upya uamuzi wangu wa kutohudhuria kituo Cha kupiga kura
 
Ushauri wa Bure kwa Waajiriwa wote wa Serikali hasa wale wa Vimemo vya Uteuzi kutoka Kurugenzi ya IKULU kuweni makini zaidi pengine kuliko awamu yoyote ya Uteuzi wenu...
Team ya ushaudi aliyoipata now mama wako serious sana naona wamemwambia mama kama unaona huruma acha tukusaidie sisi kuwa wakali
 
Wake wa mungu kaamua ugomvi,na bahari imetulia nao wamefikiwa? Bado mmoja,hakuna kauli zilinikeraga Kama hizo,yaani kwa kariba ya viongozi wa CCM niliwakubali sana Nyerere na magufuli,kwa uraisi ,kariba ya uwaziri niliwakubali sokoine na mrema, Sasa kauli za mawaziri wa uma kukejeri umauti wa magufuli,iliniuma mno,binafsi hata Kama kura yangu isingeoongeza chochote,basi niliamua kutoipigia kura CCM na hata upinzani nisingepigia,maana mbowe na zito niliwasikia wakisema tukazikwe nae,Ila Sasa labda huyu mama anatafuta kura zetu tu ,lakini nimefurahishwa na kumtumbua nape na makamba, naanza kutafakari upya uamuzi wangu wa kutohudhuria kituo Cha kupiga kura
Niwazi mama amekonga vyoyo za watu
 
Back
Top Bottom