Kama Rwanda ndiyo inaisaidia M23......

Kama Rwanda ndiyo inaisaidia M23......

Daby

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2014
Posts
33,894
Reaction score
76,810
1. Kwanini Jeshi la DRC lisiweke kambi kuzunguka mipaka yote ya Rwanda?
Kama ni kweli Rwanda ndiyo inawafadhili waasi supply yote itaisha ndani ya mwezi mmoja.

Yaani kama tunapigana na waasi wanaosaidiwa na kenya tunahakikisha kuanzia mwanza hadi kilimanjaro mipaka ina jeshi litakao tapakaa vijijini na maporini.

Vivyo hivyo kama Mataifa ya nje ndiyo yanayowafadhili m23.

Sielewi naombeni mnieleweshe.
 
1. Kuna silaha za Rwanda zinapitia bongo
2. Kuna silaha za Rwanda zinapitia Uganda
3. Kuna silaha za waasi ndani ya DRC zinapatikana kutoka kwa wanaolinda amani DRC
4. Kuna silaha zinakuja kwa ndege
5.

Kuna watu hawapendi maeneo Yale yawe na amani. Kukiwa na amani pale halafu pakawa organized ile ni sehemu tajiri sana
 
Unakuwa na jeshi limetanda kuanzia Mara mpaka Tanga kudhibiti waasi wanaotoka Kenya kama mfano wako unavyosema lakini ni less organized, corrupt, not motivated, halina vifaa na mafunzo, mamluki wengii, etc. Haitofaa kitu. Shukuru JWTZ
 
DRC ina jeshi dhaifu. Haiwezi kufanya unavyopendekeza.
 
Shida hilohilo jeshi la kongo kuna wasaliti!, ile vita ki mbinu ni rahisi ila kiuhalisia ni ngumu maana wale majeshi yakongo kuna watu wa M23 wanatoa taarifa za nini kinafuata kwa M23!.

shida ni hilo jeshi la kongo ni dhaifu mno hivyo ni rahisi kuhongeka!, halafu ugopa matajiri wakiona ni kikwazo humalizi muda watahakikisha unasepa! ile vita ukitaka uivunje wajue wale mapapa wanaofadhiri M23, halafu fanya operation ya siri sana uwaue! hapo hakuna jiwe litakaa juu ya jiwe!.
 
Hawa waasi sio kama
1. Kuna silaha za Rwanda zinapitia bongo
2. Kuna silaha za Rwanda zinapitia Uganda
3. Kuna silaha za waasi ndani ya DRC zinapatikana kutoka kwa wanaolinda amani DRC
4. Kuna silaha zinakuja kwa ndege
5.

Kuna watu hawapendi maeneo Yale yawe na amani. Kukiwa na amani pale halafu pakawa organized ile ni sehemu tajiri sana
Rais hajataka kudhibiti uingizwaji wa silaha....

Hawa waasi wapo established kilometa kadhaa za mraba. Monitor ndege zinazoingia weka checkpoints njia zote kuelekea wanapoishi waasi. Ukikata walau 60% ya mawasiliano kati ya waasi na mataifa ya nje ikiwemo Rwanda umemaliza kazi.

Je, AU inataka kuisaidia Congo kweli au nasisi tunafurahia yanayotokea....viongozi hawawezi Kuja na njia mbadala au wanafurahia kina mama wanavyokimbia na vitoto vichanga?
 
Unakuwa na jeshi limetanda kuanzia Mara mpaka Tanga kudhibiti waasi wanaotoka Kenya kama mfano wako unavyosema lakini ni less organized, corrupt, not motivated, halina vifaa na mafunzo, mamluki wengii, etc. Haitofaa kitu. Shukuru JWTZ
Au ndani ya jeshi Kuna M23?
 
Unasemaje jeshi linalopigana kila siku ni dhaifu Mkuu?
Kupigana kila siku sio hoja ,hoja linapata nini kwenye hayo mapigano ya kila siku ndio hoja

Jeshi la Drc haliko well organised kuna vikundi ndani ya jeshi mkipanga hili siku hiyo hiyo kama lilivyo limefika kwa waasi kuna nini fellaaaa?
 
Kazi ya jeshi linaloongozwa na Angola ni nini?
Jeshi linaloongozwa na Angola sijui, ninachojua DRC ina jeshi dogo, lisilo na silaha wala uwezo wowote, Kagame na mamluki wake wanajiingilia DRC wanavyotaka.

Sijafuatilia hilo jeshi linaloongozwa na Angola lina ukubwa na uwezo gani, na majukumu yao ni yapi.
 
Unasemaje jeshi linalopigana kila siku ni dhaifu Mkuu?
Linalazimika kupigana kila siku kwa sababu M23 wanakuwa kwenye offensive, lenyewe linakuwa kwny deffensive.

Namaanisha waasi wanakuwa wanapigana kusonga mbele na jeshi la DRC linalazimika kupigana kujihami, halina uwezo wa kuwafuata kwny kambi zao huko misituni.

Hiyo FARDC, bila kusaidiwa, ndani ya wiki moja waasi wanaikamata Kinshasa, serikali ya DRC inaishi kwa msaada wa majirani tu.
 
Waafrika hawana umoja usaliti njenje unaweza kuta usiyemdhania kumbe ndie
 
1. Kwanini Jeshi la DRC lisiweke kambi kuzunguka mipaka yote ya Rwanda?
Kama ni kweli Rwanda ndiyo inawafadhili waasi supply yote itaisha ndani ya mwezi mmoja.

Yaani kama tunapigana na waasi wanaosaidiwa na kenya tunahakikisha kuanzia mwanza hadi kilimanjaro mipaka ina jeshi litakao tapakaa vijijini na maporini.

Vivyo hivyo kama Mataifa ya nje ndiyo yanayowafadhili m23.

Sielewi naombeni mnieleweshe.
Tacticaly haiwezekan DRC kupeleka wanajeshi kuzunguka rwanda. Wakti adui yupo ndani ya ardhi yake
Logistic zitakuwa ngumu, front lines zitakuwa overstreched
 
Tatizo kubwa la DRC ni "weak state", hata kulipa wanajeshi yenyewe ni changamoto, wakati mwingine maafisa hata wanatokomea na posho za wanajeshi.
 
DRC WAOMBE TZ WAUNGANE WAWE KAMA ZANZIBAR ILA MAAMUZI NA JESHI LIRATIBIWE IKULU DODOMA🤝
 
Back
Top Bottom