Kama Samatta kakwama huko England mashabiki tuambiwe ukweli

AV wanaamini watapata kibali kesho Juma3 na game ya Jumanne dhidi ya WATFORD atakuwemo kikosini
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Genk wameshatoa salamu za kuumuaaga. Mabeberu huwa hawakurupuki kutoa taarifa kama anavyotoaagaa manara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo points anazipata vipi ? Kwani Aston villa before wamu point walikua hawajajua hayo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Babu hakuna wakala mwenye muda wakuangalia huyu mchezaji nikatoka taifa gani ishu ya Tanzania kuwepo kwenye umoja wa jumuiya ya ulaya ni ishu za nchi na nchi. Aston villa wao wananaangaika na work permit kuanzia kesho.
 
Hizo points anazipata vipi ? Kwani Aston villa before wamu point walikua hawajajua hayo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu wenzetu Wana taratibu zao, za Wizara ya Kazi, Uhamiaji na toka kwa Chama cha Mpira....

Kwanza Ili upate nafasi ya kucheza EPL lazima National team yako iwe kwenye Nafasi za juu, kwa hilo ni rahisi kupata Work permit...

Pili Inawezekana National team haiko kwenye nafasi za juu but Kama ni Raia wa Umoja wa Ulaya Una nafasi ya haraka kupata Work permit.

Tatu... Kama huna vyote wanaangalia Points toka kwenye Records zako huko ulikocheza na Mechi za Team ya Taifa...

Mfano...
Wanasema kama ni Mshambuliaji uwe na Wastani wa kufunga sio chini ya Goals 15 kwenye Msimu mmoja....
Uwe umeshacheza Europa league.
Uwe umecheza Uefa...
Uwe umecheza Angalau Mechi kadhaa National team na wastani mzuri wa Mabao National Team...
N.k

Sasa ukija kwa Samatta hana Uraia wa Ulaya, National Team yake Iko nyuma Sana kwa Ubora.... ILA RECORD ZA KULE GENK ALIKOKUA ZINAMBEBA KUWEZA KUPATA POINTS ZA KUTOSHA KUPATA WORK PERMIT UK.

Keshafanya Medical, washakubaliana Dau na Genk, washakubaliana na Maslahi ya Samatta... KINACHOSUBILIWA NI WORK PERMIT ambayo inaweza kutoka week ya Kesho mapema....
 
Imagine huo mpango wa kwenda Aston Villa ukazingua hivi wale walio mpongeza kwenye page zao pamoja na kuweka picha za photoshop wataweka wapi sura zao.!?? Vipi na wale wanao enda kwenye page ya Aston Villa na viswahili vyao vya kejeli?

Lakin leo Genk si wanacheza, vipi Samatta yupo kwenye kikosi.??
 
Mungu abariki tu ili kijana wetu atimize ndoto zake,na sisi tujivunie angalau,hivi Hashim thabit anaendeleaje? Nilimuombea sana kwa Mungu.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mshahara wake ni upi kwa wiki tafadhali.
 
Suala la msingi ni mshahara mkubwa, sio ligi. Wewe unaangalia ligi kwa kuwa ni mshabiki, lkn yeye anayefanya mpira kama ajira haangalii ligi, anaangalia salio

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ni hivyo basi njia nyeupe kwa Samatta
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…