SoC04 Kama Serikali ikishirikiana na wawekezaji kuwekeza kwenye public Wi-Fi, Tanzania tuitakayo itakuja haraka sana

SoC04 Kama Serikali ikishirikiana na wawekezaji kuwekeza kwenye public Wi-Fi, Tanzania tuitakayo itakuja haraka sana

Tanzania Tuitakayo competition threads

Tomaa Mireni

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2015
Posts
2,395
Reaction score
2,391
Kitambo kidogo mtandao wa Internet ulikuwa anasa ila kulingana na maendeleo ya sayansi na teknolojia mtandao umekuwa moja ya hitaji la binadamu.
Kulingana na uchumi wa Afrika bado gharama za internet ni kubwa sana kulinganisha na hali za maisha mtaani.

Mtandao wa Swahili Times ukimnukuu waziri wa mawasiliano na teknolojia Tanzania Nape Mnauye, Tanzania ni ya 6 barani Afrika kwa gharama nafuu za internet. Lakini je hali ikoje mtaani? Yani ukijiunga kifurushi cha internet cha 500 (MB250) zinakutosha kabisa kwa siku?

Vipi ikiwa kutakuwa na huduma ya Wi-Fi maeneo mbalimbali kwa gharama ya 500 na ukapimiwa muda ila megabytes ukapewa isiyo na kikomo? (Unlimited) bila shaka itasaidia wengi sana hata speed ikiwa ya wastani tu.

Wi-Fi ni teknolojia ya mtandao wa Internet isiyotumia waya inayotumia mawimbi ya redio kutoa kwa kasi ya juu. (Kiswahili)
WiFi_Logo.svg.png
📸Wikipedia
Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi wastani wa pato la kila Mtanzania kufikia 2022 ni milioni mbili laki nane na themanini elfu(2,880,000)kwa mwaka.
(Pato la Mtanzania laongezeka hadi kufikia Sh2.88 milioni)

Tugawanye sasa hiyo kwa siku 2,880,000÷360=8000
Matumizi ya lazima kila siku kwenye 8000.
  • Chakula kutwa 5000
  • Kodi ya nyumba 1000(ikiwa chumba ni 30,000 kwa mwezi)
  • Akiba 1000
  • Mahitaji mengine 500
  • Kifurushi cha simu 500. Mpaka hapo 8000 imeisha.
Unaweza kujifunza siku nzima online kwa 500? Dakika 20 tu bila kistream utaona (umetumia 75%ya bando lako) 😁

USHAURI HUU HAPA
Serikali, wawekezaji na makampuni yanaweza kufunga huduma ya Wi-Fi maeneo mbalimbali ya kijamii kwa gharama nafuu.

Miundo mbinu inaweza kutumika iliyopo kama minara ya mawasiliano, majengo marefu n.k na maeneo lengwa hasa yenye watu wengi kama vyuoni, bustani za umma, masokoni, viwanjani, majumba makubwa ya biashara na hata makaazi pia.
IMG_20240426_161426.jpg
📸AliExpress
Kwa kutumia mifumo mtandao kama
Clouds Network Management System (NMS)
Mifumo hii inapatikana sana kwa wenzetu nje ila kwa Tanzania inapatikana maeneo machache ikiwemo, viwanja vya ndege, mahotel makubwa na baadhi ya masoko, basi iletwe kwa jamii yote bila kujali aina ya watu na mazingira yao.

Mifumo hii inasaidia kuondoa ile mtumiaji kupeana nywila(Password) na mtu mwingine, na pia huwezi kuwashiana hotspot, na inakuwa mfumo wa password au vocha ambayo unaweza kununua mwenyewe kwenye mfumo au kwa mwendeshaji, kwa hiyo ili kupata huduma sio lazma utoe simu ili uwekewe password.
IMG_20240501_200204.jpg
📸Lazada edition

Ili ienee kwa haraka Tanzania nzima ni lazma serikali, makampuni makubwa au hata wawekezaji wawekeze kwa kununua miundombinu hiyo sababu ina gharama kubwa kiasi.

FAIDA KWA KILA MMOJA
Hii inaweza kuwa fursa kwa mwekezaji, serikali na jamii pia. Serikali itafaidika kwa wananchi kusogezewa huduma za mawasiliano karibu,jamii itafaidika kwa kupata huduma za mtandao karibu na kwa gharama nafuu na mwekezaji atafaidika kwa sababu atapata watumiaji wengi kwa wakati mmoja.

Faida kwa mwekezaji,baada ya kufunga huduma (installation). Mfano ikiwa unatumia huduma ya supakasi tuseme unalipia speed ya 200mbps ambayo ni 400,000 kwa mwezi.
images (1).jpeg
📸Vodacom
Kwa siku unakapata watumiaji 100×500=50000.(siku)
  • 50000×30=1,500,000(mwezi)
  • 1,500,000-400,000=1,100,000(faida)
  • Matumizi100, 000+mfanyakazi 400,000=500,000
  • Unabaki na 600,000 ni ndogo?
Ukiwa na biashara zako maeneo mawili?
Tanzania tuitakayo bila mtandao haitawezekana safari itakua ndefu sana.
 
Upvote 13
Ewaaaah, unaongelea intaneti.

Sawa sawia

Kuna jambo moja tu ambalo inabidi liangaliwe. Labda serikali ingeweka vipaumbele kwanza inataka wananchi wake wajifunze kipi na kipi.

Kama kuna sites maalumu za mafunzo tu (khan academy, udemy etc) basi ifanye utaratibu wa kuziweka katika zero tarif mode (yaani tusilipie kuingia). Kama ilivyowahi kuwa JF na FB kipindi fulani. Na hata sasa kuna mitandao bando likiisha mtandao wao unafunguka kiotomati. Hivyo inawezekana ushahidi ni huo.

Nina imani hili litasaidia maana tukiachia tu intaneti ya bure, starehe zinaweza kuzidi kazi na kujifunza tukala hasara kama taifa. Kwenye intaneti hakuna mafunzo pekee, kuoe kuna kila kitu bro.
 
Sawa kabisa, mkuu kwenye mifumo ya NMS unaweza kuban, kulimit mitandao unayotaka ifunguliwe na usiyotaka pia. Mfano mitandao ya ponografia unaweza kuamua mtumiaji asipate access kabisa.
 
Mimi napenda internet na movies sana... Shughuli zangu robo 3 zinahitaji umeme na internet kwa wingi ndo nipate connections za pesa..

Kupitia public WiFi serikali inapaswa kuwekeza nguvu kubwa na kwa kasi pia wasiwe wabaguzi wa hiyo huduma..

Changamoto inakuja baadhi ya viongozi wa serikali wanapinga sana hizi huduma kutufikia raia kwa bei nafuu na pia hawataki ushindani kutoka kwingine sababu wana mikono yao kwenye hayo makampuni ya mawasiliano ilihali kazi imewashinda..
 
Asee ni kweli na ukiangalia maeno yote ya kishua kila kampuni ya mtandao inaoikuja inafika huko, ukipiga simu unataka huduma ukiwa Mbagala, Chanika, Buza n.k utaambiwa huko hatujafika. Kwa hiyo kama zilipatikana kote kote itasaidia sana
 
View attachment 2979012
Hapa ni bure kama unavyoiona

Na ktk taasisi kama shule zipo pia buree

Nazani wataenda mbali zaidi zipatikane bure nchi nzima
Hizi hata konokono ana speed! Sehemu kama Dar Internet ni majanga. Wangeweka milingoti (kwa sababu infrastuctures nyingi zimekaa zig zag) wakaunganisha fiber, halafu waache haya ma-ujinga ya vifushi.
 
Kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya simu kuwa na uwezo wa kibenki, na kuanza kutumia hizi free unsecure WiFI ni mwanzo wa watu kuanza kupulizwa masalio yao kwenye simu.

1715096760428.png
 
Hizi hata konokono ana speed! Sehemu kama Dar Internet ni majanga. Wangeweka milingoti (kwa sababu infrastuctures nyingi zimekaa zig zag) wakaunganisha fiber, halafu waache haya ma-ujinga ya vifushi.
Hizi za bure lazma ziwe slow tu sababu unakuta mchango wa serikali labda 50mbps lakini watumiaji 100 lazma iwe konokono
 
Una mawazo mazuri sana…. Tatizo users watakua busy kwenye udaku na ubwege tu

Good ideas mkuu
Mkuu hilo halikwepeki,kama ilivyo mitandao mingine ni moja wapo ya hasara kwa watumiji
 
Kitambo kidogo mtandao wa Internet ulikuwa anasa ila kulingana na maendeleo ya sayansi na teknolojia mtandao umekuwa moja ya hitaji la binadamu.
Kulingana na uchumi wa Afrik

This person has good visions regarding increasing the availability of public Wi-Fi at affordable costs in Tanzania. Considering the current situation of high internet costs, initiatives like this could bring positive changes to society, promote access to knowledge, and boost the economy through investment. It's a good idea for the government, investors, and the community to collaborate to make this happen.
Ikiwa serikali au mashirika mengne Kuandaa semina pamoja na mashirika mbalimbali ambayo yako tayari kusaidia (kwa njia zote) au kutoa elimu kuhusu mambo haya ni jambo zuri sana. Semina kama hizo zinaweza kusaidia kuhamasisha uelewa kuhusu umuhimu wa kuwa na upatikanaji wa Wi-Fi ya umma kwa gharama nafuu na jinsi inavyoweza kuleta mabadiliko chanya kwa jamii. Kuungana na mashirika hayo kutatoa nguvu zaidi kwa kampeni ya kufanikisha lengo hili.
 
Maisha bila internet hayaendi, lakini kipimo cha internet tz ni kidogo ila tukipata ya Unlimited itakuwa poa sana
 
Maisha bila internet hayaendi, lakini kipimo cha internet tz ni kidogo ila tukipata ya Unlimited itakuwa poa sana
 
Back
Top Bottom