SoC04 Kama Serikali ikishirikiana na wawekezaji kuwekeza kwenye public Wi-Fi, Tanzania tuitakayo itakuja haraka sana

Tanzania Tuitakayo competition threads

Tomaa Mireni

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2015
Posts
2,395
Reaction score
2,391
Kitambo kidogo mtandao wa Internet ulikuwa anasa ila kulingana na maendeleo ya sayansi na teknolojia mtandao umekuwa moja ya hitaji la binadamu.
Kulingana na uchumi wa Afrika bado gharama za internet ni kubwa sana kulinganisha na hali za maisha mtaani.

Mtandao wa Swahili Times ukimnukuu waziri wa mawasiliano na teknolojia Tanzania Nape Mnauye, Tanzania ni ya 6 barani Afrika kwa gharama nafuu za internet. Lakini je hali ikoje mtaani? Yani ukijiunga kifurushi cha internet cha 500 (MB250) zinakutosha kabisa kwa siku?

Vipi ikiwa kutakuwa na huduma ya Wi-Fi maeneo mbalimbali kwa gharama ya 500 na ukapimiwa muda ila megabytes ukapewa isiyo na kikomo? (Unlimited) bila shaka itasaidia wengi sana hata speed ikiwa ya wastani tu.

Wi-Fi ni teknolojia ya mtandao wa Internet isiyotumia waya inayotumia mawimbi ya redio kutoa kwa kasi ya juu. (Kiswahili)
📸Wikipedia
Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi wastani wa pato la kila Mtanzania kufikia 2022 ni milioni mbili laki nane na themanini elfu(2,880,000)kwa mwaka.
(Pato la Mtanzania laongezeka hadi kufikia Sh2.88 milioni)

Tugawanye sasa hiyo kwa siku 2,880,000÷360=8000
Matumizi ya lazima kila siku kwenye 8000.
  • Chakula kutwa 5000
  • Kodi ya nyumba 1000(ikiwa chumba ni 30,000 kwa mwezi)
  • Akiba 1000
  • Mahitaji mengine 500
  • Kifurushi cha simu 500. Mpaka hapo 8000 imeisha.
Unaweza kujifunza siku nzima online kwa 500? Dakika 20 tu bila kistream utaona (umetumia 75%ya bando lako) 😁

USHAURI HUU HAPA
Serikali, wawekezaji na makampuni yanaweza kufunga huduma ya Wi-Fi maeneo mbalimbali ya kijamii kwa gharama nafuu.

Miundo mbinu inaweza kutumika iliyopo kama minara ya mawasiliano, majengo marefu n.k na maeneo lengwa hasa yenye watu wengi kama vyuoni, bustani za umma, masokoni, viwanjani, majumba makubwa ya biashara na hata makaazi pia.
📸AliExpress
Kwa kutumia mifumo mtandao kama
Clouds Network Management System (NMS)
Mifumo hii inapatikana sana kwa wenzetu nje ila kwa Tanzania inapatikana maeneo machache ikiwemo, viwanja vya ndege, mahotel makubwa na baadhi ya masoko, basi iletwe kwa jamii yote bila kujali aina ya watu na mazingira yao.

Mifumo hii inasaidia kuondoa ile mtumiaji kupeana nywila(Password) na mtu mwingine, na pia huwezi kuwashiana hotspot, na inakuwa mfumo wa password au vocha ambayo unaweza kununua mwenyewe kwenye mfumo au kwa mwendeshaji, kwa hiyo ili kupata huduma sio lazma utoe simu ili uwekewe password.
📸Lazada edition

Ili ienee kwa haraka Tanzania nzima ni lazma serikali, makampuni makubwa au hata wawekezaji wawekeze kwa kununua miundombinu hiyo sababu ina gharama kubwa kiasi.

FAIDA KWA KILA MMOJA
Hii inaweza kuwa fursa kwa mwekezaji, serikali na jamii pia. Serikali itafaidika kwa wananchi kusogezewa huduma za mawasiliano karibu,jamii itafaidika kwa kupata huduma za mtandao karibu na kwa gharama nafuu na mwekezaji atafaidika kwa sababu atapata watumiaji wengi kwa wakati mmoja.

Faida kwa mwekezaji,baada ya kufunga huduma (installation). Mfano ikiwa unatumia huduma ya supakasi tuseme unalipia speed ya 200mbps ambayo ni 400,000 kwa mwezi.
📸Vodacom
Kwa siku unakapata watumiaji 100×500=50000.(siku)
  • 50000×30=1,500,000(mwezi)
  • 1,500,000-400,000=1,100,000(faida)
  • Matumizi100, 000+mfanyakazi 400,000=500,000
  • Unabaki na 600,000 ni ndogo?
Ukiwa na biashara zako maeneo mawili?
Tanzania tuitakayo bila mtandao haitawezekana safari itakua ndefu sana.
 
Upvote 13
Hakika saiz ni mambo ya kidigital asilimia kubwa hela zinaisha kwenye bando kwaiyo punguzo la ghatama itasaidia Sana hasa sisis wa Hali ya chini serikali wazingatie hilo
 
Kweli kabisa mkuu, semina zingetilewa kwanzia wilayani hatdi kwenye miji mikubwa kuhusu matumizi ya huduma hii ya wifi
 
Asante mkuu, hili wazo la kibiashara kabisa, nalichukua,haya ndio mawazo yanayotakiwa Mungu akubariki.
 
Asante mkuu, hili wazo la kibiashara kabisa, nalichukua,haya ndio mawazo yanayotakiwa Mungu akubariki.
Asante mkuu, kama uko vizuri fanyia kazi utakuja kunishukuru
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…