Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 22,168
- 39,118
Jumapili iliyopita nilisafiri kikazi toka Mbeya nilikokuwa kikazi kuelekea Rukwa hususan wilaya ya Nkasi ambako nilikuwa naendelea na majukumu ya kiofisi.
Eneo la kazi Kwa mkoa wa Rukwa ilikuwa ni Kabwe na Kipili Wilayani Nkasi na Kasanga Wilayani Kalambo ambako kuna miradi ya ujenzi wa bandari mwambao wa Ziwa Tanganyika.
Baada ya kuandika habari za bandari ya Kabwe na kisha Kipili Leo majira ya saa 5 asubuhi niliondoka eneo la Kirando nilikofikia Kwa basi dogo nakumbuka limeandikwa MABEST.
Kisa ninachotaka kusimulia kimetokea makao Makuu ya wilaya ya Nkasi mji wa Namanyere eneo la stendi kuu ambapo tulisimama kushusha abiria na kupakia wengine wanaoelekea Sumbawanga ambako ni mwisho wa safari Kwa gari tulilopanda.
Tukiwa hapo stendi ghafla tukasikia kelele vijana wa boda boda wakihimiza mwanamke mmoja asiendelee kuteswa na Wanajeshi watatu wa kiume àmbao baadaye nilisimuliwa na walioshuka kuwa wako kwenye kambi ndogo (Detach) ya hapo Namanyere.
Kisa cha mwanamke yule kupigwa na kuvuliwa nguo hadharani Hadi kubaki na nguo za ndani kinashangaza na hakina uzito wa kupewa mateso yale ya kupigwa, kubuluzwa na kumwagiwa maji huku amefungwa Pingu mikono Kwa nyuma. Naambiwa kwamba chanzo; Jana Askari hao walitumwa na viongozi wao kumtafuta Askari mwenzao mlevi ambaye hajaingia kazini Kwa siku 3 kwa sababu ya ulevi.
Kwamba walimkuta mwanajeshi huyo ndani ya duka la pombe la mwanamke huyo aitwaye Huruma na kumchukua mzobemzobe huku wakifanya vurugu kubwa ndani ya duka hilo kwa kummwagia maji ndani ya duka hilo ambayo yalikuwa kwenye ndoo kubwa humo ndani. Kosa la mwanamke Huyo likawa ni kuhoji kwanini anafanyiwa fujo kwenye Biashara yake wakati yeye hakumuita huyo Askari mwenzao?
Waliondoka na mwenzao lakini wakaahidi kurudi kumtia adabu muuzaji kwa vile yeye ndiye anampa pombe mwenzao. Ahadi hiyo wameitimiza leo mchana kwa kwenda dukani Kwa mwanamke Huyo wakamkamata na kumfunga Pingu kisha kumlowesha maji na kuanza kumpiga na baadaye kuondoka naye kwenda kambini kwao kwa habari nilizopewa japo mpaka naandika hapa sjui hatima ya binti huyo.
Najuà Mkuu wa wilaya ya Nkasi ni Peter Lijualikali, ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya. Nakushitakia hili kwani liko ndani ya uwezo wako.
Fika stendi au tuma vyombo vyako kupata hatima ya mama huyu. Ningekuwa na namba yako ya simu nungekupigia lakini kesho naahidi kabla sijakwenda Kasanga nitamjulisha Mkuu wa mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti.