Kama Sheria Ziko Wazi, Ya nini kuomba msaada serikalini?

Kama Sheria Ziko Wazi, Ya nini kuomba msaada serikalini?

Naisujaki Lekangai

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
1,340
Reaction score
1,377
Kipo kisa cha udhalilishaji kimefanyika huko Iringa, ila nashangaa baadhi ya viongozi wanaomba serikali eti ichukue hatua kali dhidi ya mdhalilishaji.

Kisa kiko hivi: Mwanamke mmoja kaenda zake kwenye mkutano wa uchaguzi wa UWT. Akiwa kwenye mkutano, mumewe akatinga ndani ya kikao na kumpiga huyo mwanamke (ni mkewe). Viongozi wa kikao hicho walilaani sana kitendo hicho - sawa nakubaliana nao - ila sikubaliani nao wanapoomba eti serikali imchukulie huyu mwanaume hatua kali.

Huyo mwanaume moja kwa moja kavunja sheria kwa kuleta fujo hadharani na sheria zipo za kumpeleka mahakamani, na adhabu za kosa hilo zipo.Kisa hiki hakihitaji serikali bali polisi na mahakama. Hata hivyo serikali iliingilia kiasi kwa dc kumweka huyo mwanaume ndani kwa masaa 48.

Lakini bado mpaka sasa viongozi wa UWT wilaya na mkoa wanaililia serikali kuchukua hatua.

Nauliza: Serikali ichukue hatua gani tena badala ya hawa viongozi walioshuhudia mama akipigwa kumpeleka huyo bwana mahakamani?

Mdau, kama umekisikia kisa hiki naomba uchangie.
 
Utajiuliza uwt iko kwa madhumuni gani? Hata kumtetea mwenzao hawawezi, kazi ulaji tu.
 
Utajiuliza uwt iko kwa madhumuni gani? Hata kumtetea mwenzao hawawezi, kazi ulaji tu.
Kweli sana mdau. Mimi nilitarajia hao wanawake wangekuwa ni binadamu wa kawaida wanaochukizwa na udhalilishaji, wangemrukia huyo jamaa na kumpa makonzi mwili matatu ndio wazungumzie hatua za kisheria za kumchukulia.Nasikitika hawakumgusa wala!
 
Ya Kaisari muachie Kaisari...unaweza kukuta huyo mwanamke amezoea kupigwa na anamsamehe mumewe
 
Back
Top Bottom