MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 21,387
- 44,030
Nimeona nitoe maoni yangu kuhusu hii fukuza fukuza iliyoanza huko CHADEMA chini ya Tundu Lissu. Ni jambo limeshangaza wengi kwa chama cha demokrasia kukataa maoni tofauti na kutotaka kabisa mjadala kuhusu maamuzi yaliyofanyika.
Kwa upande wangu naona Lissu na genge lake la kamati kuu wako sahihi kuwashughulikia wote walio kinyume na hiyo slogan yao hata kama haina mafanikio. Kuongoza watu ambao miongoni mwao wanahujumu misimamo yenu sio sawa. Lazima ushughulike nao kwanza.
Kinachonipa hofu ni kuwa huenda anachokifanya Lissu ni mihemko yake tu na baada ya muda mfupi atanyoosha mikono. Kama sio nguvu ya soda inabidi Lissu na kamati yake iwafutilie mbali uanachama wajumbe wote wa G55 wakaungane na Covid19.
Lissu ni mwanasiasa mkubwa anayeungwa mkono na wanasiasa wakubwa kama Lema, Heche na Brenda. Lile kundi la John Mrema fyeka lote.