Kama taifa kuna umuhimu mkubwa sana wa kufanya maandamano ya amani ya kitaifa Tanzania

Kama taifa kuna umuhimu mkubwa sana wa kufanya maandamano ya amani ya kitaifa Tanzania

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
ni katika kuipongeza serikali hii sikivu, kutambua, kumpongeza na kuunga mkono nia na dhamira ya dhati ya mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Tanzanian Dr. Samia Suluhu Hassan, kwa hatua muhimu za makusudi, kimkakati katika chochea mageuzi na kuwaletea waTanzania maendeleo endelevu, kijamii, kisiasa na kiuchumi...

hivi sasa wakulima na wafugaji wanatabasamu, mavuno ni mengi chakula na maji kwaajili ya mifugo yao ni ya uhakika...

wafanyabiashara ni kicheko tu mazingira ni mazuri ya amani na utulivu sana, masoko ya kisasa na wateja ni kama wote kila mahali nchi nzima..

ulinzi na usalama wa mipaka, watu, mali na makazi yao ni imara na wa kuaminika, lakini pia ni wa uhakika sana..

huduma za maji, umeme, afya, elimu, uvuvi, usafishaji, miundombinu, mawasiliano, haki na uhuru wa habari, siasa na mikutano ya hadhara n.k mijini na vijijini vinatolewa na kusimamia kwa usawa na kwa uhakika zaidi..

wito kwa wanainchi na waTanzania wa makundi yote nchini, bila kujali vyama vya siasa, dini, rangi kabila au urika tujiandae na kuungana na waTanzania wengine kumshika mkono kiongozi wetu kipenzi wa Taifa,

aidha taasisi, idara, mamlaka na asasi za kidini na kiraia, kitaifa na kimataifa, vilabu vya vya soka, Simba, yanga, Azam kuungana na waTanzania katika kupongeza kazi na jitihada hizi muafaka za kiongozi wetu Dr. Samia Suluhu Hassan katika kulinda amani na kuwaunganisha wa Tanzania wote 🐒

unadhani ni muda na wakati gani muafaka zaidi kabla ya uchaguzi ujao, jambo hili kufanyika?

asanti kwa kuunga mkono 🐒
 
Back
Top Bottom