Kama Taifa tufanyeje ili vijana waweze kuhimili madaraka makubwa wanayopewa?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Vijana wengi tumeaminiwa na kupewa madaraka makubwa sana lakini Madaraka hulevya mno, ukuu tunaopewa unatulewesha na kudhani wengine wasio na madaraka si chochote wala si lolote!

Je, kama nchi tufanyeje ili kuondoa hali hii?

Vijana wengi tumeaminiwa na kupewa madaraka makubwa sana , lakini Madaraka hulevya mno , ukuu tunaopewa unatulewesha na kudhani wengine wasio na madaraka si chochote wala si lolote
Hasa yule aliyekua reporter wa ITV anajiona utafkiri yeye ana akili kuliko watu woooote jamani nchi inavituko hii

Kwanza akiongea lazima afoke hana stara wala busara ya kuwasilisha jambo katika maongezi ya kawaida tu anapoelezea jambo fulani

Haki yeye na Kabudi hawana tofauti lazima macho yawatoke wanasimamisha mishipa ya shingo mtaumia bure tangu mwaka 1961 mpaka leo hii wapi mliona au kusikia kutoa macho na kushupaza shingo ndio uongozi bora

ACHENI USHAMBA!!!
 
Vijana wengi tumeaminiwa na kupewa madaraka makubwa sana lakini Madaraka hulevya mno, ukuu tunaopewa unatulewesha na kudhani wengine wasio na madaraka si chochote wala si lolote!

Je, kama nchi tufanyeje ili kuondoa hali hii?

View attachment 1697892
Haya ni mambo ambayo mtu anatakiwa afunzwe tokea utotoni.

Tabia za kiuongozi anatakiwa awe nazo kila mtu hivyo zinatakiwa watoto wetu walelewe hivyo.

Mtoto asilelewe kuwa mtu wa chuki na majivuno pale anapopata,akikua na tabia hii hata katika uongozi hatokuwa na tabia hizo za chiki na majivuno
 
Unataka kutuambia kwamba wanaopewa uongozi waangaliwa hata jinsi walivyolelewa ?
 
Noo waangaliwe tabia zao sio walivyolelewa.

Mtu kalelewa miaka 50 nyuma utamuinaje sasa.

Angalia tabia zake namna anavyokaa na watu utajua tu kwamba anatabia gani,yaani achunguzwe hasaa.

Wengine wanaweza kulelewa vibaya wakaja kubadilika mbele hivyo kumhukumu kwa alivyolelewa sio jambo la kuzingatia.

Muhimu aangaliwe ana tabia gani sasa hivi.
 
Nakala iende kwa Mamlaka za uteuzi
 
Zamani kulikuwa na chuo cha chama pale Kivukoni. Ndio hico wamekigeuza kuwa Mwalimu Nyerere Memorial University
Nakifahamu saaana. Hapo ndipo walipokosea. Wakuuu wa mikoa, wilaya, wakurugenzi, idara zote na makatibu wakuu wote wanatakiwa kwakweli wawe wamehitimu chuo cha taaluma ya uongozi.
 
Right. Suala hili la upungufu wa kimaadili kwa viongozi lilishwahi kungelewa na Katibu Mkuu wa CCM Dr. Bashiru. Alikuwa anawaongelea Hapi na Makonda, kwamba madaraka yamewazidi kimo kiasi kwamba wanajiona ni miungu watu. Watengeneze kozi kwenye vyuo vingine kwa ajili ya kusomesha watu hawa maana ya uongozi
 
Mwenyekiti wa chama analizungumziaje hili ?
 
Uchaguzi wa demokrasia wa ushindani katika uwanja wa siasa ulio sawa.
Vijana wengi tumeaminiwa na kupewa madaraka makubwa sana lakini Madaraka hulevya mno, ukuu tunaopewa unatulewesha na kudhani wengine wasio na madaraka si chochote wala si lolote!

Je, kama nchi tufanyeje ili kuondoa hali hii?

View attachment 1697892
 
Right. Suala hili la upungufu wa kimaadili kwa viongozi lilishwahi kungelewa na Katibu Mkuu wa CCM Dr. Bashiru. Alikuwa anawaongelea Hapi na Makonda, kwamba madaraka yamewazidi kimo kiasi kwamba wanajiona ni miungu watu. Watengeneze kozi kwenye vyuo vingine kwa ajili ya kusomesha watu hawa maana ya uongozi
Usihofu ccm tutawanoa viongozi wetuu.
 
Back
Top Bottom