Nyankurungu2020
JF-Expert Member
- Oct 2, 2020
- 4,170
- 6,757
Kuendelea kushupaza shingo kuwa hakuna makosa yaliyofanyika juu ya uvunjifu wa haki za binadamu hapa nchini kwetu ni kupoteza muda. Maana ni kutaka kujenga taswira isiyofaa kuwa mauaji, ukatili na uvunjifu wa sheria ni jambo la kawaida.
Tukubali kuwa kuna makosa makubwa yalifanywa na vyombo vya dola na yanaendelea kufanywa na vyombo vya dola. Maana mbali ya watu wanaojulikana kama Lissu, Saanane, Alphonse Mawazo bado kuna malalamiko makubwa juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na vyombo vya dola. Mbaya zaidi viongozi wanajua na wanafumba macho.
Tusishupaze shingo, tukubali makosa yalifanyika na tujirekebishe maana kukosolewa au kupata mawazo kinzani ni sehemu ya maisha. Hii nchi ni ya kwetu sote.
Lakini je nani atayafuta makovu yaliyopatikana na udhalimu waliofanyiwa akina Alphonse Mawazo, Tundu Lissu, Ben Saanane na wengine wengi ambao hawajulikani?