Kama taifa tuna mwongozo wa jinsi ya kulinufaisha taifa letu kwanza tuwapo nje ya nchi yetu!?

Kama taifa tuna mwongozo wa jinsi ya kulinufaisha taifa letu kwanza tuwapo nje ya nchi yetu!?

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
1,968
Reaction score
2,957
Mataifa mengi sana yaliyo serious na maendeleo huwa walishawajengea watu wao wote kwamba ukiwa kwenye mataifa ya watu hakikisha kwa namna yoyote uwezavyo nufaisha taifa lako kwanza.

Nakumbuka nimewahi kufanya kazi na makampuni kutoka Africa kusini yaani walikuwa kila kitu kinachotumika kwenye kampuni lazima kiaguzwe kutoka kwao. Jambo lililomaanisha kuimarisha viwanda vya Africa kusini nchini Tanzania.

Hali ni hiyo kwa mataifa mbalimbali ya duniani watu hujipanga kunufaisha kwao kupitia fursa zilizopo kwenu.

Ndipo nikajiuliza sana maana katika huu utu uzima wangu sijawahi kukuta popote panapotoa mwongozo wa jinsi hiyo.

Jambo ambalo mimi nilidhani lilipaswa kufundishwa kwa nguvu sana ili iwaingie watu kwamba lazima tunufaishe taifa letu kupitia dunia inayotuzunguka.
 
Back
Top Bottom