Kama Tanzania haifungamani na upande wowote, kwanini hatununui mafuta ya Bei rahisi Urusi?

marine 1

Member
Joined
Jul 29, 2015
Posts
60
Reaction score
67
Nianze Kwa kutoa pole kwa changamoto za kuishi!

Kama kichwa kinavyojieleza, kumekuwa na taarifa kuhusu kupanda Kwa Bei za mafuta na gesi duniani, huku Urusi, Moja ya wazalishaji wakubwa wa mafuta na gesi akishusha Bei ya bidhaa hizo ambapo mataifa makubwa, ikiwa ni pamoja na Yale yaliyomwekea vikwazo yananunua bidhaa hizo muhimu.

Tanzania imejipambanua kutofungamana na upande wowote katika vita hivyo. Hii ni baada ya kutopiga kura kwenye umoja wamataifa kuiwekea vikwazo Urusi.

Sasa swali ni kwanini hatununui mafuta ya Bei nafuu kutoka Urusi?
Badala ya serikali kuwaambia wananchi kuwa bidhaa zitapanda, ambayo ni taarifa inayofahamika, wao wamefanya Nini zaidi kuepusha kuongezekakwa gharama za maisha?

Kwa maoni yangu ni kwamba serikali haijafanya vya kutosha. Haijashughulika vyakutosha kuwasaidia wananchi. Badala yake inawaacha wananchi wake kuangukia kwenye janga ambalo lilijulikana linakuja, na kulikuwa na namba ya kuwasaidia.

Wakati mkuu wa nchi akituambia Bei zitapanda, tunaambiwa Vatikan imetumia mamilioni kununua sarafu ya Urusi ili kuendelea kupata mafuta na gesi, siku moja kabla ya Raisi wa Urusi kusaini Sheria ya kutumia fedha za Urusi kununua bidhaa hizo. Hapo serikali ya Vatikan ilichukua hatua stahiki kusaidia raia wake.

Nitoe Rai Kwa wafanya maamuzi kujaribu kufanya zaidi kuwasaidia raia waliowapa mamlaka. They should do more, using their intelligence, rather than telling us the obvious, which we know!

Nawakilisha.
 
Kumbe Ukraine nako huwa wanazalisha mafuta? Mi nilikuwa sijui, asante kwa kunifumbua macho.
 
Kupanga ni Kuchagua vipaumbele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…