Kama tatizo ni katiba mbovu basi marekebisho ya kwamza kabisa ni "Uwepo wa mgombea binafsi"

Kama tatizo ni katiba mbovu basi marekebisho ya kwamza kabisa ni "Uwepo wa mgombea binafsi"

HAKI KWA WOTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2022
Posts
2,783
Reaction score
2,396
Leo tungeona maajabu kwani wagombea wote waliokatwa kinyume na matakwa ya wananchi iwe ndani ya CCM au vyama pinzani basi wangesimama kivyao na wangeshinda kwa vishindo.

Hii ndiyo njia pekee ya kuikomboa Tanzania na kuiondoa CCM madarakani vinginevyo wanaotoka CCM kwa maana ya kwenda upinzani bado wanaenda CCM.

Tutafakarini sana,sana!!
 
vyama vyote vilikataa hoja ya mgombea binafsi sio Fisiemu tu peke yao hadi CDM na washirika wake kwenye warioba
 
vyama vyote vilikataa hoja ya mgombea binafsi sio Fisiemu tu peke yao hadi CDM na washirika wake kwenye warioba
Kama umenielewa ccm ndiyo ilikataa kwani vyama vyote vya upinzani ni ccm.

Katiba ibadilishwe kwa maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla siyo vyama tena
 
Kwa upande wangu mgombea binafsi si shauri sana mambo yana weza kuwa yale yale hapa kuwe na kipengele cha kuwaadabisha wachaguliwa kama hawaja tekeleza ahadi au hawajafanya kazi zao ipasavyo katika kuwatumikia wananchi; na kama itakuwepo hii section tunaingia nao makubaliano wasipo wajibika walicho kihaidi wanabinafsishiwa mali au warudishe mishahara yote waliokuwa wanalipwa na posho ndani ya miaka mitano hapo tutafika ila tukiendelea hivi tutakuwa kama kenya vurugu tuu na wanasiasa wanakula wanaondoka
 
Back
Top Bottom