Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Sabato Njema!
Kambi ya Mbowe ingekaa ikatulia, ikatafakari, ikahesabu kila hesabu na chenchi zake. Hakika kama wangefanya hivi wasingemruhusu Mbowe Agombee tena.
Ningekuwa kwenye hiyo Kambi, ningewashauri; "Tunahitaji Kambi yetu iendelee kuongoza. Sisi ni wamoja. Nasema uongo?"
"Mbowe tayari kaongoza kwa miaka 21 sasa, angeweza kuendelea na sifa za kuendelea anazo, na Katiba inampa fursa hiyo. Lakini vipi, je chama Kitabaki kilivyo baada ya yeye kugombea?
Tunajua Chama ni wanachama, chama ni watu. Sio Sisi tuu tuliomo humu kwenye hiki chumba. Wapo watu Nje, wanachama wetu na wasio na vyama, wapo Diaspora, je watatuunga Mkono.
Vipi mitazamo Yao juu yetu itaimarika maradufu au tutainyong'onyeza? Tunahitaji akiba ndogo ya uaminifu wa watu kuhusu chama chetu ilindwe, na iboreshwe. Hao ndio wateja wetu. Kuangusha Imani ya wanachama wetu ni kuangusha wateja wetu. Nafikiri hatupo tayari kuona chama chetu kikifa mapema hivi mbele ya macho yetu tungali tu hai na wenye nguvu hivi.
Tunahitaji watu wengi. Kuna waliopoteza. Hao tunatakiwa tuwathibitishie walifanya uamuzi usiosahihi kupoteza tumaini na chama chetu. Hii inatupa Kazi hapa tumtafute mtu ambaye ata-meet mahitaji ya watu na wanachama wetu.
Mshindani wetu Lisu tunamfahamu. Hatuna hofu naye kuwa atatushinda, tunajua Hilo haliwezi kutokea hata kwa kujidanganya.
Lakini Hatuwezi kumshindanisha Kaka Yetu Mbowe na Lisu.
Tutawapa watu hoja na nguvu ya kutupotezea wanachama.
Mnafahamu, tulipata hasara kubwa ya viongozi wetu wengi kuhamia CCM kwa mahasimu wetu Wakubwa. Sipendi Hili, kukumbuka maumivu ya wanachama wetu waliolipa gharama za maumivu makali, kwa kutekwa na kuuawa na watu wasiojulikana wangali wameacha majeraha yaliyogoma kukauka katika familia zao na wanachama waminifu WA chama chetu.
Tufikiri kwa HEKIMA tujue Nje ya Mbowe ni Nani atuwakilishe kuchukua uenyekiti. Huyo tutamuunga Mkono. Kama ambavyo tumekuwa tukifanya hivyo kwa Mbowe.
Mtu huyo lazima awe na rekodi Njema. Hata kama kwa Siri ni mbaya lakini iwe anauzika kwa Wanachama.
Chama chetu kinahitaji Kukua zaidi kwa Kupata hiki kizazi cha Gen Z.
Lakini pia Kuna watu Mashuhuri huko Mtandaoni tuliokuwa nao lazima tuiteke Imani Yao. Tunahitaji Watu Wakuu!
Hatupaswi kupuuza yeyote ambaye ni potential.
Hii tutaita Demokrasia na Uwajibikaji kama chama chetu kinavyofahamika. Unajua, tukisema Mzee Mbowe aendelee tunawapa Mashaka makubwa wanachama wetu, hasa wale wenye akili zinazofikiri mpaka mwisho tofauti na wale wenye akili zinazofikiri kisha kuishia njiani.
Mbowe atashinda lakini vipi sasa baada ya kushinda nini kitatokea?
Mwakani ni uchaguzi.
CCM watasema nini? Hatuhitaji kuongeza idadi ya maadui ilhali tulionao wanatutosha.
Tunahitaji kuongeza zaidi watu na sio kuwapunguza kwa namna hii isiyofaa.
Hata kama tutakuwa waongo haipaswi uongo wetu uwe wazi namna hii. Mpaka vipofu wauone ulaghai wetu.
Uongo wetu inatakiwa uonekane Kweli hata kwa WATU Werevu. Hiyo ndio Siasa yaani Uongo Uliokubalika. Tukishindwa Jambo kama hili hiyo itamaanisha hatufai kuitwa wanasiasa na kuwa viongozi wa chama cha siasa. Huyo mtu ni Nani ndugu Wajumbe?
Tusijeleta Kiburi cha Fulani aliondoka, hakuna kilichotokea, Fulani akaondoka hivyohivyo hakuna kilichotokea. Hapana hatutakiwi kupoteza watu wetu kirahisi hivi. Watu tuliowaandaa wenyewe kwa Kipindi kirefu.
Wenzetu CCM wao watu wao wanajua namna ya kuwalinda, wale watu potential hawakubali kirahisi kuwaachia. Kwa nini Sisi tuwaachie?
Mnajua ilivyokazi kumuuandaa mtu kuwa kiongozi. Na sio Kazi ya siku moja au Mwaka Mmoja.
Acha nikale Makande kidogo alafu nitarudi.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es Salaam