Kama tuhuma dhidi ya Kinana zilikuwa siyo za ukweli basi Msigwa ana uwezo mdogo wa akili. Kama zilikuwa na ukweli basi kuna dili lilichezwa

Enzi zile ilikua kama mashindano kwa wabunge wa cdm kuibua chochote ili kujipatia umaarufu zaidi
Sio wabunge tu, hata sisi hapa Jamvini, tulikuwa kila mara tunamuongelea Kinana hivyo! Kila akijitokeza, tulikuwa tunasema anamaliza tembo wetu!
Inawezekana alishindwa kutushtaki, kwani tumejificha. Msigwa, akajilipua, kama Lyatonga alivyokuwa amejilipua ile issue ya milioni 900.
 
Chadema walishapotezxa ueleke pale walipomchukua Lowassa na Sumaye kuwa wanachama wao na kumteua Lowassa kuwa mgombea wao wa utiketi ya urais kwani walionyesha kushindwa kusimamia kauli zao pia watu makini waliachanaa nao sasa hivi wamebaki na watu wanaoitwa nyumbu ambao wanaamini kila linalosemwa na uongozi wao
 
Kwani kwenye hiyo kesi Mh. Msigwa hakuwakirishwa na Wakili Nguli Tundu Lissu? Hata ushauri tu ili ashinde kesi? Ahahahahahahh! Wakili Nguli Tundu Lissu!!!
 
Lyatonga alishinda kwenye Kesi ya Milioni 900!
 
Labda ndiyo Kinana anakaribishwa CDM
 
Tatizo siyo msigwa, tatizo mfumo wa kutafuta info wa makamanda ulimuingiza chaka na sidhan km unajitendea haki kufikia hatua ya kumuita muuaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu achana na utamaduni wa Mabeberu!! Africa kusema uwongo sio tatizo ni utamaduni wetu.

1 . Tuliambiwa ndege ingefuata dawa Madagascar lakini baadaye tukaambiwa sio dawa ni malighafi kwenye utafiti.
2. Tuliambiwa tz haikuhudhuri mkutano wa EAC kwa sababu haikualikwa lakini baadaye waziri wa Rwanda alidai taarifa ilitolewa ila tuligoma kwenda.
Mkuu tambua kuna uwongo mzuri wenye faida na usio na faida. Huu uwongo hapa kwetu tz unafaida.
 
Tatizo siyo msigwa, tatizo mfumo wa kutafuta info wa makamanda ulimuingiza chaka na sidhan km unajitendea haki kufikia hatua ya kumuita muuaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
MWONGO NI MUUAJI!
Leo Kariakoo ni kiasi cha mtu kupiga kelele MWIZI...MWIZI...!
Na kama utadumu na roho yako kwa dk 20 unabahati.
Msigwa ndicho alichofanya lakini hakufanikiwa.
 
Kumbe kuna mchezo wa kuhalalisha matatizo yasiyokuwepo ili kutafuta sifa binafsi za kijinga jinga hv.watanzania wanahitaji umakini wa hali ya juu.
 
Matatizo ndani ya chama chochote cha siasa huwa yanasababishwa na ukosefu wa adabu na ujanja ujanja wa kijinga wa baadhi ya wanachama kuona wao wanajua sana kuliko wangine,hoja inapoletwa mezani hasa ile inayotilia shaka mienendo na uvunjaji wa sheria na kanuni zinazo ongoza chama ni vema sana ikatiliwa maanani na si kuidharau,siku zote ukweli huwa una tabia ya kuchelewa na ukifika watu huumbuka na hata wasijue wapi kwa kuweka sura zao,na badala yake watu hubaki kuwa kama kituko fulani kwenye jamii,tukumbuke ss sote kwamba siasa zetu bado ni changa sana na hivyo basi zinahitaji msingi ulio bora ili ziweze kukomaa na kuleta maendeleo ya kweli katika jamii zetu na taifa kwa ujumla.hivyo basi hatutafanikiwa kamwe kwa kuendelea kujenga siasa zetu kwenye msingi wa Uongo na kuuweka ukweli pembeni,jamii zetu zitaendelea kuishi ktk umaskini wa mali na fikra hata wasijue wanasimama wapi ili kulipigania taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…