Kama tumefikia hatua ya kuachia watuhumiwa kwa sababu za kisiasa, Taifa letu linaelekea pabaya sana

ni kweli kabisa mkuu
 
Dpp anaachia matapeli tu,

Yaani hata watoto wadogo wanafahamu kuwa jamaa ni matapeli Ila ndio wanaoachiwa.

Hii nchi ukiwa muungwana unapoteza muda Bure Bora kuwa mwizi utalindwa na mamlaka.
 
Bashite na meko ndo sababu
 
Haki huinua taifa na kama viongozi wa uamshoni innocent taifa litainuka. Haki huinua taifa.
 
Mtuhumiwa mahabusu ana haki na anapswa kwa na heshima nyingi zaidi kuliko mfungwa kama babu Seya.
Hoja sio wao kwenda ikulu bali ni walikuwa wafungwa tofauti na hawa mahabusu. Hilo la kwenda ikulu ni ishu nyingine
 
Kama walikamatwa kisiasa ni lazima waachiwe kisiasa NO MATTER WHAT.
 
Mfumo wa sheria za makosa ya jinai Tanzania ni kandamizi. Umerithiwa kutoka Sheria za kikoloni Kama zilivyoainishwa kwenye ripoti ya Tume ya Jaji Nyalali ya Sheria 40 mbaya zinaopaswa kufutwa.

Sheria hizi na zinazofanana nazo zinaipa nguvu serikali kuwafunga watu kizuizini bila mashitaka, au kuwaweka mahabusu kwa muda mrefu kwa kisingizio cha "uchunguzi unaendelea".

Katib pia inampa mtu haki ya kujitetea mahakamani.

Kwenye sheria kuna msemo " justice delayed is justice denied".

Unapomfunga mtu mahabusu miaka sita au zaidi, bila kukamilisha uchunguzi wala kumpa nafasi ya kujitetea, umemuondolea uhuru wake kwa miaka sita kabla hata hujamuhukumu kwenye kesi.

Hicho tayari ni kifungo cha miaka sita kabla hata ya hukumu.

Kama hujamaliza uchunguzi usipeleke kesi Mahakamani
 
Sheria zote ambazo hamzipendi mwambieni Rais wenu azibadili kwa ''jina la Jamhuri ya Tanzania''.
 
Dpp anaachia matapeli tu,

Yaani hata watoto wadogo wanafahamu kuwa jamaa ni matapeli Ila ndio wanaoachiwa.

Hii nchi ukiwa muungwana unapoteza muda Bure Bora kuwa mwizi utalindwa na mamlaka.
Hata babu seya alikuwa tapeli....
 
Mbona sukuma wenu aliwachia wabakaji walio thibitishwa na mahakama babu seya
 
Mbona hukulalamika mwendazake alivyowaachia akina Sabaya wauaji na majambazi wakubwa wawe huru uraiani na U-DC juu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…