May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,311
- 9,027
Sweden grants 100bn/- for fund TASAF Phase II - IPP Media
https://www.ippmedia.com › news › sweden-grants-100...Nimeona kama Nchi tumepokea Msaada kwa ajili ya Mpango wa kupunguza umasikini Nchini.
Hii inamaanisha ya kuwa kama Serikali tunakiri ya kuwa Sehemu ya Wananchi wetu ni Masikini na Wanahitaji Msaada.
Kama ndivyo ni vipi tena kutoka Serikali hiyohiyo tunaaminishana ya kuwa Watanzania wote tuna uwezo wa kulipa tozo kupitia miamala?
Je, ni kwamba Viongozi wetu Serikalini hawazungumzi lugha moja? wapo wanaoamini kuna Masikini na wapo wanaoamini ya kuwa Wote wana mapato?.
Je, Serikali ya Sweden inajua ya kuwa Masikini wetu wana uwezo wa kulipa tozo?.
Ndio kusema 'Masikini' huyu akipokea kiasi cha shilingi elfu ishirini ya kumuondolea Umasikini iwapo atatumia mtandao kuhamisha pesa hiyo itapunguzwa na Serikali hiyohiyo iliyoamthibitisha kuwa yeye ni Masikini, na hiyo 20000 waliyompa wanaamini ni kubwa sana kwake na inafaa kupunguzwa kama tunavyowapunguzia kina Bakhresa na Mo Dewji?.