Haki za binadamu zikiwamo za kuishi, usalama, kulindwa, kujilinda, kusikilizwa n.k, si hisani. Anasema beberu: "Human rights aren't negotiable."
Hizo haziombwi. Zaidi sana anasema beberu: "Human rights are enforceable."
Tunataka Katiba Mpya. Ni haki yetu. Haki hupiganiwa.
Hatuwezi kuwa ndumila kuwili katika haki. Haki ni haki hata kama kwako binafsi inaweza kuwa ni kero. Hapo ndipo mambo ya ngoswe huingia.
"Haki za wapenzi wa jinsia moja zinihusu vipi mimi au wewe usiyehusika?"
Nikiwa mhanga wa panya road, nimewahi kuandika uzi nikiitisha kujilinda ikiwamo kwa kutumia nguvu zetu wenyewe:
Dar: Panya road wavamia nyumba 24, wanne wajeruhiwa
Hii nikiamini: "katika utawala usiowajibika, mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe."
Kujilinda huku hakuna maana ya kukiuka haki za msingi za wengine:
1. Mhalifu hawezi kutambuliwa kwa macho yake, rangi yake, umbo lake, mavazi yake, ongea yake, nk.
2. Mtu atabakia kuwa mtuhumiwa hadi mahakama imkute na hatia.
3. Mtuhumiwa asikamatwe pasipo na upelelezi wa kutosha kufanyika, kuweza kumfikisha mahakamani.
CHADEMA (nawaita kwa jina) na wapigania haki wote, mnayo dhima ya kuyasemea haya wazi wazi na bila ya kuchelewa mno.
Kigugumizi chenu kinafanya hadi wajinga sugu (wapumbavu) kujinasibu kuwa wana hoja.
Panya road ni nani?
Kwa hakika hata aliyetokomea na kina Ben, Lijenje, Azory na kuweka watu kwenye viroba naye ni panya road tu!