Kama tunazalisha jumla ya Megawati 1600 iweje upungufu wa Megawati 300 usababishe mgao mkali hivi?

January Makamba kama waziri mwenye dhamana nadhani akubali tu kuwa kazi imemshinda na sio kwamba yeye ndio shida pekee lakini kama kutoa taarifa sahihi tu nayo shida basi hafai. Mimi napenda kuliongelea hili kwa namna tofauti kidogo. Tuchukulie hii hali ni kweli ok nini la kufanya, hata nyumbani kwako ukiona huna unit za kutosha unazima taa au vifaa ambavyo labda sio muhimu kwa wakati huo. Sasa tuseme ni kweli mapungufu ni 300 kweli kwa akili za kawaida tu huwezi kupanga hizi 300 tupunguze wapi kwa maana Dar na majiji mengine ambayo uzalishaji wa kiuchumi ni mkubwa kwanini wasitolewe kwenye mgao na hiyo 300 zikalengwa maeneo ambayo shughuli za uzalishaji ni ndogo mpaka mambo yakae sawa huwezi kugawa umeme sawa mji Musoma na Dar yako mambo lazima tuambizeni ukweli mambo yanaweza kupangwa tu na sio kwa nia mbaya labda dharau hapana ila ndio ukweli hata kama unagawa Dar usizeme umeme city centre maana ni sehemu ya uzalishaji mkubwa.
 
hakika tanesco hawatutendei haki wananchi wa Tanzania

kama jana toka asubuhi hadi sa6 usiku hakuna umeme

mnatufanya tukumbuke zamani kwa sababu hizi shida tulishazisahau

ni MBAYA haipendezi KABISAπŸ˜•
 
Tubadilike watanzani tuanze kupanda miti tutalaume tanesco mpaka lini.idadi ya watu imeongezeka. watu wanao ingiza umeme ni wengi.Lakin Uharibifu wa mazingira umekidhiri sana.watu wanakatakata ovyo miti ndio chanzo cha chemichemi kukauka.
Bahari ipo tuchepushe maji kwenye bahari yaende bwawa la mwalimu nyerere rahisi tuu au maji ya chumvi hayafai.???
 
Wewe endelea kuwasiliza na kuwaamini wana-siasa wa ccm, ni waongo utafikiri wana ukoo na 'yule mtu'!
 
watanzania tushazoeza fix, na uzuri wetu hatunaga ubishi. So watawala wana enjoy kweli kutawala taifa lisilo na uwezo wa kuhoji kwa vitendo.
 
Serikali ndivyo walivyo, kesho watakuja kukanusha hizo taarifa...
 
Umeme unaozalishwa Tanzania na kupitia vyanzo mbali mbali na kuingizwa gridi ya Taifa ni 1600Megawatts lakini umeme unaotumiwa na viwanda vya samsung ni zaidi ya 2000 Megawatts meanwhile samsung inc ni kampuni inayomilikiwa na familia moja na wanahisa wachache. Aseee tupo pabaya sana
 
watamteka, lile la kwanza tu bado wanahangaika nalo.

Na ndio limeleta hii tafrani yote, ziara, matamko, maelezo basi tu ilimradi ionekane wanawajibika.

Wakimteka itakua wanaongezea mafuta kwenye moto uzidi kuwaka.
 
Kwa hesabu hizo, Megawati 300 ni kama asilimia 20 ya uzalishaji wetu wote. Tulitegemea tupate umeme kwa asilimia 80 ya masaa ya siku. Mgao ulitakiwa kuwa wa masaa matano tu kwa siku, nao siyo kila siku. Serikali ya watu waongo-waongo.
 
Mungu ni mwema sana
Huku niliko leo wamekata mara Moja tu😊😊😊😊
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…